Nimechoka na matusi ya huyu kaka yangu mwenyewe Miaka zaidi ya 40

Nimechoka na matusi ya huyu kaka yangu mwenyewe Miaka zaidi ya 40

Huyo ni Blacksheep aka Chamdeko Kuna Uzi ulipandishwa humu namna ya kudeal na Wapuuzi kama Hao, Huyo anafanya Huo Ujinga Kwasbabu anajua Kuna Watu watamsikiliza au Watumuone Huruma, Mbona mtaani tuna Vichaa kibao tu na hawatembei na Mapanga, Chukueni Bold Decision ndio mtabadilisha Kuendelea kumuona huruma Ndio mtampoteza zaidi mana Kuna siku atajichanganya Watu wamalizane nae au Wamjeruhi Msala atauleta Nyumbani mtahangaika Kumtibu

Huyo Pelekeni Polisi kwa kumshtaki au Hospital za Vichaa akae uko for atlest one year akitoka trust me atakuwa amebadilika sana tena akiwa Huko msiende hata Kumsalimia
Mitaani vichaa hawatembei na mapanga sababu ni vichaa. Huyo ana akili timamu that's why anashika mapanga. Ni mshenzi tu mwenye tabia mbovu.
 
Solution kama walivyoandika wengi. Sober house, hospitali kitengo cha akili, wanajuwa jinsi ya kuwatibia hao watu. Polisi hapana.
Kadata na maisha.
 
Mkandarasi ni nani
Mkandarasi ni Engineer, kozi ya miaka 4 na zaidi. Inabidi uwe vizuri kwenye Mathematics(hesabu), Physics(fizikia) na Chemistry(chemia). Hayo ni masomo magumu yanayohitaji watu wenye akili na utimamu. Na wengi utakuta wanamiliki maghorofa sababu ni serious profession with serious payment.(kazi inayolipa vizuri)

Sasa nashangaa huyo ni Mkandarasi gani anayekaa kwa mama yake, aliyekosa heshima, na utimamu wa akili ya hata kujitambua. Anafanya kazi gani?
 
Fatilieni kwanza matatizo gani yanamsubua, ukute fyuzi zimeruka nyinyi munaona yupo sawa, mwenye akili timamu hawezi kufanya ujinga huo, inawezekana hizo bangi ndizo zinazomsumbu na network imepotea, poleni kwa mitihani ndio maisha yalivyo musimtelekeze tafuteni dawa kama kweli munampenda. Hao machizi wa mtaani munavyowaona walianza hivyo hivyo, watu waliwatelekeza na maradhi yakajenga himaya Yao kwenye miili Yao, jiulize tu utafurahia kumuona kaka yako anaokota makopo mtaani? Tafakari chukua hatuwa kabla hujachelewa. Ambulance zipo kama hamuwezi kumpeleka wenyewe huko hospital [emoji541]
 
Mkandarasi ni Engineer, kozi ya miaka 4 na zaidi. Inabidi uwe vizuri kwenye Mathematics(hesabu), Physics(fizikia) na Chemistry(chemia). Hayo ni masomo magumu yanayohitaji watu wenye akili na utimamu. Na wengi utakuta wanamiliki maghorofa sababu ni serious profession with serious payment.(kazi inayolipa vizuri)

Sasa nashangaa huyo ni Mkandarasi gani anayekaa kwa mama yake, aliyekosa heshima, na utimamu wa akili ya hata kujitambua. Anafanya kazi gani?
Huyu ni anaendesha zile gari za kujenga barabarani.. na ni mbobevu haswa na ndio maana ni rahisi kwake kupata kazi mpk anachagua alipwe Bei gani.. kiufupi ni mtu mwenye kibali cha kupata kazi hawezi kukaa zaidii ya miezi3 hajapata kazi mpya

Kinachombeba ni hizo CV zake but ndio hivyo ni mkorofi mpk kwa mabosi zake alishawah kumchota mchina na kile kijiko cha kubeba mavitu ya barabarani ni mpuuzi
 
Solution kama walivyoandika wengi. Sober house, hospitali kitengo cha akili, wanajuwa jinsi ya kuwatibia hao watu. Polisi hapana.
Kadata na maisha.
Polisi wanasema kwamba sober wanaendaga wale waliokuwa mateja huyu bado bangi hazija muathiri kama anauwezo hadi wa kwenda kufanya kazi tena ana operate yale mavijiko bado anajielewa

Wanasema labda awe anapewa Dawa sasa hizo Dawa unafikiri atazinywa
 
Kwani huyo kaka anaishi nyumbani?
Ndio.. alikuwa na kwake ila karudi home maana walikuwa wanampiga sana huko alipokuwa anaishi ameona watamuua ndio kakimbilia home ili atusumbue sisi
 
Ndio.. alikuwa na kwake ila karudi home maana walikuwa wanampiga sana huko alipokuwa anaishi ameona watamuua ndio kakimbilia home ili atusumbue sisi
Kwa nini walikua wanampiga sana?
 
Ukute ndo alikuwa na ni mtoto pendwa wa mama. 😁

Tafuteni namna, muuze nyumba hiyo, kila mtu achukue chake ila bimkubwa achukue 40%. Bimkubwa mjengeeni sehemu, nyumba ya kiana, aje aishi na mmoja wenu kwenye nyumba atakayoijenga, kufuatia kuuza nyumba hiyo. Huyo bwana Bimkubwa akivuta, atakuja kuwapasua sio kidogo.

Huyo hamuwezi kumnawa kirahisi, mtampeleka jela huyo huyo Bimkubwa "kizazi lkitaanza kuuma" mtamtoa tuu.
Hakuna mama, anaweza vumilia mtoto afungwe jela hata kama mtoto huyo ni kichaa, mwizi au alitaka kumuua huyo huyo mama yake. Mtamfunga kwa hasira, siku mbili tatu Bimkubwa huyo huyo atasahau, ipo siku ataenda kumcheki gerezani, kizazi kitashtuka na mtamtoa wenyewe kwa pesa kibao. 😁

Tatu, maisha ya Bimkubwa hapo sio marefu, umri huo hautakagi masononeko, kimuhemuhe, kuumizwa moyo wala presha. Hayo matusi tuu na aibu zitamuua huyo mama siku si zake.

Tawanyikeni tuu hapo kiaina kwa kuuza kinachomfanya kuwa kwao hapo yaani nyumba, kinachompa kiburi huyo chizi ni "nyumbani hapo kwa bimkubwa". Ukitaka mfukuza chizi tupa makopo na matandiko yake.

Hamna cha kumfanya, na mwisho wa siku mnaikaribia jinai hapo.
Mkuu hapo siyo kwao hapo ni kwa Baba yake wa kambo, sawa na wewe umuoe Single mother mjenge Nyumba na mzae watoto sasa huyoMtoto uliomkuta nae aanze kuwa simba watoto wako wa kuwazaa kwenye Nyumba yako je huyo mtoto ana haki hapo kwenye hiyo Nyumba?
 
Jamani mpk naandika huu uzi hatujalala tunakesha kila siku

Kimsingi huyu ni kaka yangu mkubwa kabisaa wa mwaka 84 tumeshare mama.. Yeye ni mkandarasi.sijajua tatizo ni bangi ama amerogwa.. maana bangi ni chakula kwake na mapombe

Huyu ndugu yangu atakuja kumuua mama yangu na presha kama sio kumchoma kisu.. tumeshaongea nae sana mpk polisi kupelekana lakini Hakuna alichobadilika

Yupo nyumbani tangu mwaka 2023 na hataki kuondoka tena.. alirudi home akiwa hoi kwa kupigwa huko nnje kwa ujeuri wake,, sura imejaa alama za kutosha

Wakuu majirani wapangaji wetu hawana amani, amekuwa akiwatishia kuwakata mapanga na kuwatukana matusi ya nguoni.. anafanya fujo mtaani anatukana kila mtu. Anaweza kuvuta bangi hata ndani na Hakuna wa kumfanya kitu

Kinachoniuma zaidii anamtukana sana mama yaani matusi kabisaa ya nguoni tena akiwa nnje mpk majirani wanasikia
Hii hali namuona kabisaa mama anaumia
Mama yetu mwenyewe umri umeenda yuko na 62

Sasa nauliza tu kama nitaenda kumfungulia mashtaka polisi awekwe hata jera nitakuwa nafanya vibaya???
Huyu mtu anatembea na mapanga barabarani naogopa kuna siku anaweza kutuchinja

Na Kama Kuna mtu ameshawahi kukumbana na janga Kama hili kwenye familia au majirani walitumia njia gani kupambana na mtu kama huyu
Tafuta afande mmoja anaeweza kupiga ngumi halafu uwagombanishe akishammyosha nenda katatue huo mgogoro baada ya kipigo
 
Huyo ni wakupeleka mahakamani anapigwa jela miezi 6 kwa kumtukana mama akitoka huko anapigwa ban hakuna kukajaga nyumbani.
Msipoangalia atakuja kuwaumiza kweli
 
Back
Top Bottom