Mkaa wa mawe
JF-Expert Member
- Jun 28, 2020
- 5,055
- 7,496
Mitaani vichaa hawatembei na mapanga sababu ni vichaa. Huyo ana akili timamu that's why anashika mapanga. Ni mshenzi tu mwenye tabia mbovu.Huyo ni Blacksheep aka Chamdeko Kuna Uzi ulipandishwa humu namna ya kudeal na Wapuuzi kama Hao, Huyo anafanya Huo Ujinga Kwasbabu anajua Kuna Watu watamsikiliza au Watumuone Huruma, Mbona mtaani tuna Vichaa kibao tu na hawatembei na Mapanga, Chukueni Bold Decision ndio mtabadilisha Kuendelea kumuona huruma Ndio mtampoteza zaidi mana Kuna siku atajichanganya Watu wamalizane nae au Wamjeruhi Msala atauleta Nyumbani mtahangaika Kumtibu
Huyo Pelekeni Polisi kwa kumshtaki au Hospital za Vichaa akae uko for atlest one year akitoka trust me atakuwa amebadilika sana tena akiwa Huko msiende hata Kumsalimia
Mkandarasi ni naniHuyo sio mkandarasi huyo ni dreva
Mkandarasi ni Engineer, kozi ya miaka 4 na zaidi. Inabidi uwe vizuri kwenye Mathematics(hesabu), Physics(fizikia) na Chemistry(chemia). Hayo ni masomo magumu yanayohitaji watu wenye akili na utimamu. Na wengi utakuta wanamiliki maghorofa sababu ni serious profession with serious payment.(kazi inayolipa vizuri)Mkandarasi ni nani
Safi sanaDaah ndio hivyo mkuu… jana kakamatwa tunasubiri maelekezo
Huyu ni anaendesha zile gari za kujenga barabarani.. na ni mbobevu haswa na ndio maana ni rahisi kwake kupata kazi mpk anachagua alipwe Bei gani.. kiufupi ni mtu mwenye kibali cha kupata kazi hawezi kukaa zaidii ya miezi3 hajapata kazi mpyaMkandarasi ni Engineer, kozi ya miaka 4 na zaidi. Inabidi uwe vizuri kwenye Mathematics(hesabu), Physics(fizikia) na Chemistry(chemia). Hayo ni masomo magumu yanayohitaji watu wenye akili na utimamu. Na wengi utakuta wanamiliki maghorofa sababu ni serious profession with serious payment.(kazi inayolipa vizuri)
Sasa nashangaa huyo ni Mkandarasi gani anayekaa kwa mama yake, aliyekosa heshima, na utimamu wa akili ya hata kujitambua. Anafanya kazi gani?
Polisi wanasema kwamba sober wanaendaga wale waliokuwa mateja huyu bado bangi hazija muathiri kama anauwezo hadi wa kwenda kufanya kazi tena ana operate yale mavijiko bado anajielewaSolution kama walivyoandika wengi. Sober house, hospitali kitengo cha akili, wanajuwa jinsi ya kuwatibia hao watu. Polisi hapana.
Kadata na maisha.
Daah mkuu seriously mama angu auliwe na sie twashuhudiaMuache amuue Mamaako ili iwe fundisho kwa Wazazi wanaodekeza watoto wao.
Usipende kuingilia pale mtu anapopata matokeo ya kile alichokipanda
Ndio.. alikuwa na kwake ila karudi home maana walikuwa wanampiga sana huko alipokuwa anaishi ameona watamuua ndio kakimbilia home ili atusumbue sisiKwani huyo kaka anaishi nyumbani?
Anajenga mwendokasiMuambieni mwajiri wake amuhamishe mkoa wa mbali na nyie.
Kwa nini walikua wanampiga sana?Ndio.. alikuwa na kwake ila karudi home maana walikuwa wanampiga sana huko alipokuwa anaishi ameona watamuua ndio kakimbilia home ili atusumbue sisi
Ni professional job ...ngumu sana kuwa nahiyo situation huyo bro akoMkandarasi ni nani
Mkuu hapo siyo kwao hapo ni kwa Baba yake wa kambo, sawa na wewe umuoe Single mother mjenge Nyumba na mzae watoto sasa huyoMtoto uliomkuta nae aanze kuwa simba watoto wako wa kuwazaa kwenye Nyumba yako je huyo mtoto ana haki hapo kwenye hiyo Nyumba?Ukute ndo alikuwa na ni mtoto pendwa wa mama. 😁
Tafuteni namna, muuze nyumba hiyo, kila mtu achukue chake ila bimkubwa achukue 40%. Bimkubwa mjengeeni sehemu, nyumba ya kiana, aje aishi na mmoja wenu kwenye nyumba atakayoijenga, kufuatia kuuza nyumba hiyo. Huyo bwana Bimkubwa akivuta, atakuja kuwapasua sio kidogo.
Huyo hamuwezi kumnawa kirahisi, mtampeleka jela huyo huyo Bimkubwa "kizazi lkitaanza kuuma" mtamtoa tuu.
Hakuna mama, anaweza vumilia mtoto afungwe jela hata kama mtoto huyo ni kichaa, mwizi au alitaka kumuua huyo huyo mama yake. Mtamfunga kwa hasira, siku mbili tatu Bimkubwa huyo huyo atasahau, ipo siku ataenda kumcheki gerezani, kizazi kitashtuka na mtamtoa wenyewe kwa pesa kibao. 😁
Tatu, maisha ya Bimkubwa hapo sio marefu, umri huo hautakagi masononeko, kimuhemuhe, kuumizwa moyo wala presha. Hayo matusi tuu na aibu zitamuua huyo mama siku si zake.
Tawanyikeni tuu hapo kiaina kwa kuuza kinachomfanya kuwa kwao hapo yaani nyumba, kinachompa kiburi huyo chizi ni "nyumbani hapo kwa bimkubwa". Ukitaka mfukuza chizi tupa makopo na matandiko yake.
Hamna cha kumfanya, na mwisho wa siku mnaikaribia jinai hapo.
Kwani Kwa Baba yenu mmezaliwa watoto wa kike pekee hakuna Wanaume?Sijajua kwa upande wa kwao mkuu
Wanaume wapo mbaliKwani Kwa Baba yenu mmezaliwa watoto wa kike pekee hakuna Wanaume?
Aaah basi ndio kama nilivyoelezea sijui mtamwita naniNi professional job ...ngumu sana kuwa nahiyo situation huyo bro ako
Mkorofi kamdomo anawatukana matusi yaani kama sisi tunavyo fanyiwa sasa hao sio ndugu zake ndio wanampigaKwa nini walikua wanampiga sana?
Tafuta afande mmoja anaeweza kupiga ngumi halafu uwagombanishe akishammyosha nenda katatue huo mgogoro baada ya kipigoJamani mpk naandika huu uzi hatujalala tunakesha kila siku
Kimsingi huyu ni kaka yangu mkubwa kabisaa wa mwaka 84 tumeshare mama.. Yeye ni mkandarasi.sijajua tatizo ni bangi ama amerogwa.. maana bangi ni chakula kwake na mapombe
Huyu ndugu yangu atakuja kumuua mama yangu na presha kama sio kumchoma kisu.. tumeshaongea nae sana mpk polisi kupelekana lakini Hakuna alichobadilika
Yupo nyumbani tangu mwaka 2023 na hataki kuondoka tena.. alirudi home akiwa hoi kwa kupigwa huko nnje kwa ujeuri wake,, sura imejaa alama za kutosha
Wakuu majirani wapangaji wetu hawana amani, amekuwa akiwatishia kuwakata mapanga na kuwatukana matusi ya nguoni.. anafanya fujo mtaani anatukana kila mtu. Anaweza kuvuta bangi hata ndani na Hakuna wa kumfanya kitu
Kinachoniuma zaidii anamtukana sana mama yaani matusi kabisaa ya nguoni tena akiwa nnje mpk majirani wanasikia
Hii hali namuona kabisaa mama anaumia
Mama yetu mwenyewe umri umeenda yuko na 62
Sasa nauliza tu kama nitaenda kumfungulia mashtaka polisi awekwe hata jera nitakuwa nafanya vibaya???
Huyu mtu anatembea na mapanga barabarani naogopa kuna siku anaweza kutuchinja
Na Kama Kuna mtu ameshawahi kukumbana na janga Kama hili kwenye familia au majirani walitumia njia gani kupambana na mtu kama huyu