Nina mahusiano na mwanamke fulani, lakini kauli hii aliyoitoa mzazi wangu inanipa wasiwasi kwenda kumtambulisha

Nina mahusiano na mwanamke fulani, lakini kauli hii aliyoitoa mzazi wangu inanipa wasiwasi kwenda kumtambulisha

Habari za usiku wana JF,
Niende kwenye mada moja kwa moja, nikuwa ninamwanamke ambaye nampnda sana, na bila shaka nataman nianze nae maisha kama mungu akijalia.

Huyu mwanamke amewai kuzaa miaka 5 iliyopita, anamtoto, alizaa akiwa na 17 yrs, japo hawasiliani na baba wa mtoto na waligombana tangu miaka hiyo.

katika stor 2 tatu na mzazi wangu siku moja aligusia akisema kuwa anahitaji mwanae aishi na mwanamke ambaye hana mtoto kabisa ni kama wote waanze upya pia hataki mwanae azae kwa kutanga tanga, yaani mara huyu mara yule.

kutokana na kauli hiyo napata kigugumizi kwenda kumtambulisha huyu wangu ambaye tayar ana mtoto ambaye sio wangu. Naombeni ushauri!

Ahsanteni.
So humuamini mzazi ama kisa elimu ya kikoloni unajiona mzazi wako hamnazo.yaani tungekuwa tunasikiliza wazazi wakati wa kuoa nadhani tusingekuwa tunasumbuka.

Binafsi nilifuata wazazi sijutii smt mie ndiye naumia kuwa namsumbuaga mke wangu. Elimu pembeni. Kuna swali nilikuwa nikijiuliza hivi nimelala ninaumwa najisaidia kwa beseni ataweza kweli kunilea Kama mama yangu wa utotoni ama aliyenizaa. Huyo ndio mke wako.
 
Ata baadhi ya wanawazuoni wemelionya sana hilo la kuoa mwanamke aliyekwisha kuzaa na mwanaume mingine
 
SIKILIZA NA UTII NA UFUATE Ushauri wa mzazi wako... Otherwise yatakukuta mauzauza ya Ndoa na dunia utaiona chungu... WAZAZI wana macho ya rohoni ya kuona kesho yetu... Ni vile tu tunajifanya wajuaji...
 
Sidhani kama mtu aliyezaa ana ubaya na hichi wengi wanachofanya ni kuwatenga Hawa watu nao ni watu kama sisi

Kitu Cha msingi ni maelewano kati yenu wangapi wameoa freshers na wakapigwa matukio? Nina wadau kama watu hivi ameoa mke Yani kaugomvi kidogo jamaa asubuhi kaenda kazini anarudi nyumba nyeupe amezoa Kila kitu , mwingine hata hawakugombana basi tu mwanamke anasema hamtaki jamaa

Faida ya Hawa single mama: wanakuwa washapitia changamoto wanazijua na hawataki kurudia makosa kwasababu anavuta picha akiachwa na hapo jamii itamuona ni Malaya hata hivyo hakuna atakayemtaka tena


Mengine ni mapungufu ya kibinaadamu wote tunayo , jiulize na wewe unaesema utakubali mwanao aoe single Maza ebu vaa viatu hivyo hivyo vya mzazi ambae mwanae alipata ujauzito mazingira tata mf kubakwa au mumewe alikuwa mwizi au tabia ingine mbovu alafu akaachwa ana mtoto alafu watu wamkatae hivyo viatu vivae utafurahia mwanao kutengwa hivyo?
 
Back
Top Bottom