Ningekuwa Rais Samia, leo ningemtumbua Makonda akiwa uwanja wa KIA kabla hajakanyaga ardhi ya Arusha

Ningekuwa Rais Samia, leo ningemtumbua Makonda akiwa uwanja wa KIA kabla hajakanyaga ardhi ya Arusha

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Mbwembwe zinazofanywa na makonda na tabia yake ya kujifanya yeye ni special kuliko wakuu wa mikoani wote leo ingemtokea puani.

Ashukuriwe Mungu leo Kuna mvua Arusha, lakini mji umesimama! Watu wanalazimishwq kwenda kumpokea makonda kwa misafara mikubwa. Mbona wakuu wa mikoa wanapokabidhiwa ofisi huwa inakuwa kimya kimya kwani yeye ana nini? Yaani Makonda anaenda kupokelewa kia kwa misafara ya magari msururu.

Wakuu wa idara, wakuu wa wilaya leo hawapo ofisini wameendq kumpokea Makonda! Kwakweli Leo ningekuwa rais Samia ningemrudisha Dar akiwa kia, kazi zinasimamq kwa ajili eti anakabidhiwa ofisi Kuna maajabu gani kwenye kukabidhiwa ofisi? Makonda unanini lakini? Kwani ungeenda kama wanavyoenda wakuu wa mikoa wenzako ungekufa? Punguza cheche utachoma nyumba.
 
Hivi huwa mnafikiria kwa kutumia nini nyie upande wa pili???

Kwamba hao watu wamelazimishwa??

Wewe unaweza kulazimishwa kufana jambo usilopenda?.

Acha ujinga mtoa post kuwa na akili japo kidogo basi pia punguza wivu wa kike au achana nao kabisa.
 
Anachofanya huyu jamaa ni utoto wa hali ya juu, leo asubuhi nilikuwa nina kikao na Lema,kufika kwake naambiwa na yeye kaenda kumpokea Makonda.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Makonda anakarisma ya kupendwa.
Nilipita jana karibu na jengo la CCM nikakuta vikundi vya vijana wa CCM na wakina mama nikauliza kuna nini wakasema wanamsubiri Mwenezi mpya wa CCM. Nikauliza Kwa makada flani wakaniambia alipokuja Makonda kulikuwa na mafuriko ya watu walijaa hadi Gandhi Hall na wengine karibu na kituo cha polisi.
Wakasema mpya hana influence.

Tumuache tu huyu jamaa amalize zamu yake kwa namna yake na yeye.
 
Back
Top Bottom