Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia, yupi Rais bora kwako?

Nyerere bado anaongoza, aliunganisha nchi kwa lugha ya kiswahili akatusomesha wengi tu tena bure kabisa.

Akajenga mamia ya viwanda, akakuza umoja wa kitaifa na akafanya mengi tu ambayo waasisi wenzake walishindwa kuyafanya katika mataifa yao. Alitambua umuhimu wa Mungu kuongoza taifa tangu usiku mmoja kabla ya ule ambao bendera yetu ilipandishwa pale uwanja wa Uhuru.

Walifuatia wamejaribu kadri walivyoweza na sasa tunaye mbeijing Samia katika usukani.
 
Jakaya , maana watu walikuwa na mipunga....Yaani Jakaya angepiga miaka 20 tungekuwa mbali ,enzi za jakaya ukitangaza kuuza kiwanja leo ndani ya wiki ushauza ,enzi za jakaya kabla jengo halijaisha nafasi zote zimejaa.
Dah umenikumbusha enzi hizo kakangu alikuwa anajenga ghorofa Magomeni Idrisa, lilijaa wapangaji waliolipa kodi ya mwaka kabla ya kuisha jengo wakawa wanamghasi amalize haraka
 
Kwa hitimisho lako , uzito unalalia wapi?
 
Hongera wewe unayeijua.
Ila mimi nnachokijua Nyerere alidhulumu nyumba za Babangu kwa kisingizio cha Azimio la Arusha.
Hiyo ndo historia ya Nyerere nnayoijua mimi
Zilikuwa mkoa gani??
 
Kwa hitimisho lako, jiandae kupigwa mawe
 
Wapumbavu mnampambanisha rais magufuli aliyedumu miaka mitano na hao waliokaa miaka kumi!? Ebu oneni aibu basi ....lakini pamoja na hayo yote kawaacha mbali sana marais wengi uliowataja
 
Daaa MUNGU anakuona na hata hayati magu pia anakuona c kw tusi ili .....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…