Ongea ya Rais Samia imebadilika tangu sakata la bandari lianze

Ongea ya Rais Samia imebadilika tangu sakata la bandari lianze

Amegundua kuwa kumbe watanzania wanaweza kuamua kufuatilia mambo yao, kuyaelewa vizuri na hata kuyakomalia kwa hoja.
Hapa waondoe wale Nyumbu wa kijani. Wanakubaligi Kila kitu, waondoe pia wabunge (ambao pia wamekua wajinga).
 
huyu mama angejua watz wengi wanamuombea mabaya angekaa atuliee asubili 2025 asepe kwa amani
 
Mliipa wenyewe kura CCM, subirini dawa iwaingie...
 
Mi naisi alijua tunampenda kwa mema mengi anayotutendea kumbe tuko nae tofauti na ilikua tunamtaftia point tumzoofishe. Anapaswa kubadilika atende atakalo analoona ni sawa. Sisi atujui tulitakalo, Wala atuna sababu ya kupenda au kutopenda.
Mama aendelee na kazi tu
 
Kisa alichaguliwa na katiba ndo afanye awezavyo? Hakuchaguliwa na raia yeyote uenda ndo sababu.
 
Niliwahi comment huko nyuma, mama Samia takes everything for granted.
Anawaamini sana wasaidizi wake.
Hakai ofisini kuhoji kama wako makini.
Kila siku yuko huku yuko kule, anafungua sherehe hii na ile.

Niliwahi kujiuliza, NANI ANAFANYA KAZI ZAKE OFISINI?

Suala la bandari is a failure of checks katika the presidential office.
Ingawaje hawezi kulaumiwa kwa asilimia 100 Rais, kwa vile Katibu Mkuu ofisi ya Rais na watendaji wengine, wapo.
Lakini uwajibikaji katika hili linamponza Rais moja kwa moja.

Rais aitupie jicho ofisi yake na kuhoji kwa nini limetokea.
Na je kama alisaini bila kuwaonyesha huo mkataba
 
mambo yamekua magumu kwake pole sana hii kitu mtu huwa anapitia milima na mabonde
 
Wewe utakuwa li CHADEMA au Sukuma gang! Ulikuwa umeanza vizuri lakini ulivyohitimisha na shinikizo kwa Rais kuhusu Katiba mpya nimekupuuza!
Mtu yeyote asiyeona kwamba katiba yetu ni mbovu mno na ndio inayoruhusu mikataba mibovu huyo mtu ni punguani.
 
Huwa najiuliza hivi wakati wa kutuomba kura 2025 atakuwa na ujasiri wa kutoka wapi kama sasa hivi hawajali wamama na wananchi wanyonge (wa hali ya chini) ambao ndo maskini ya Mungu huwa wanapiga kura kwa uaminifu kulinganisha na matajiri ambao kwanza ni wachache na pili wengi wao hawanaga muda mchafu wa kwenda kupiga kura!
Watanzania ni wasahaulifu na wengi ni mbumbumbu...ukipita upepo wa simba na yanga msimu mpya watakuwa wameshasahau madhaifu yake yote na kumshangilia mikutanoni kama mkombozi wao
 
Huwa najiuliza hivi wakati wa kutuomba kura 2025 atakuwa na ujasiri wa kutoka wapi kama sasa hivi hawajali wamama na wananchi wanyonge (wa hali ya chini) ambao ndo maskini ya Mungu huwa wanapiga kura kwa uaminifu kulinganisha na matajiri ambao kwanza ni wachache na pili wengi wao hawanaga muda mchafu wa kwenda kupiga kura!
Anayehesabu kura ndio anaamua mshindi.
 
Kwa anayefuatilia hotuba za Rais Samia atagundua kuwa namna yake ya kuzungumza na hulka yake vimebadilika kwa kiasi flani tangu sakata la bandari lianze. Ile sauti yake ya kurelax na kujiamini imetetereka kidogo. Sina uhakika kama ni hali ya hewa na kibaridi hiki.

Lakini hii yaweza kumaanisha nini?

1. Kwamba ameguswa na yanayoendelea kuhusu bandari

2. Hakutegemea yanayoendelea kufika mbali hivyo

3. Ni dadili ya kusutwa dhamiri

4. Anahisi kupoteza uungwaji mkono na heshima aliyojijengea (loss of trust).

5. Amekuwa kwenye shinikizo (stress) kubwa kipindi hiki

6. Amegundua kuwa kumbe watanzania wanaweza kuamua kufuatilia mambo yao, kuyaelewa vizuri na hata kuyakomalia kwa hoja.

7. Amekuwa defensive na mwenye mipasho kinyume na tunavyomjua.

Ama kwa hakika hiki ni kipindi kigumu kwa rais wetu.

Sasa;

Anapaswa kuwa mkweli kwa nafsi yake na kwa nchi yake.

Anapaswa kuruhusu mchakato wa wazi na wa kizalendo juu ya bandari zetu.

Anapaswa kuepuka wasaidizi wake wanaomsifia kupita kiasi na kumshauri kinafiki.

Tunamwomba rais wetu asibweteke na kuanza siasa za kibabe kama anavyoshauriwa na wanafiki wengi waliomzunguka kwani mkakati huu utakuwa na madhara makubwa kwake na kwa wananchi.

NB: Suala la kupuuzia marekebisho ya katiba litamletea fedheha kubwa zaidi siku zijazo.
Hakuna lolote Dr Samiah yupo cool, na amesha vaa ngozi ngumu, with no stress!
 
Back
Top Bottom