Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Rais Samia ni mrithi wa hayati JPM, asingefariki dunia leo hii angeendelea kuwa makamu.Kwa anayefuatilia hotuba za Rais Samia atagundua kuwa namna yake ya kuzungumza na hulka yake vimebadilika kwa kiasi flani tangu sakata la bandari lianze. Ile sauti yake ya kurelax na kujiamini imetetereka kidogo. Sina uhakika kama ni hali ya hewa na kibaridi hiki.
Lakini hii yaweza kumaanisha nini?
1. Kwamba ameguswa na yanayoendelea kuhusu bandari
2. Hakutegemea yanayoendelea kufika mbali hivyo
3. Ni dadili ya kusutwa dhamiri
4. Anahisi kupoteza uungwaji mkono na heshima aliyojijengea (loss of trust).
5. Amekuwa kwenye shinikizo (stress) kubwa kipindi hiki
6. Amegundua kuwa kumbe watanzania wanaweza kuamua kufuatilia mambo yao, kuyaelewa vizuri na hata kuyakomalia kwa hoja.
7. Amekuwa defensive na mwenye mipasho kinyume na tunavyomjua.
Ama kwa hakika hiki ni kipindi kigumu kwa rais wetu.
Sasa;
Anapaswa kuwa mkweli kwa nafsi yake na kwa nchi yake.
Anapaswa kuruhusu mchakato wa wazi na wa kizalendo juu ya bandari zetu.
Anapaswa kuepuka wasaidizi wake wanaomsifia kupita kiasi na kumshauri kinafiki.
Tunamwomba rais wetu asibweteke na kuanza siasa za kibabe kama anavyoshauriwa na wanafiki wengi waliomzunguka kwani mkakati huu utakuwa na madhara makubwa kwake na kwa wananchi.
NB: Suala la kupuuzia marekebisho ya katiba litamletea fedheha kubwa zaidi siku zijazo.
Hana kipya alichokileta hata hili suala la DPW ni la mtangulizi wake JPM. Na leo angekuwa hai angesaini mkataba pale ikulu Dodoma na hakuna mtu hata mmoja ambaye angekuja kuhoji wala kufungua mdomo wake wote tungepiga makofi na kuimba mapambio mengi tu.
Hii ni biashara waliyoianzisha waarabu waliponunua mali za huko DRC, yeye na Kagame wakaushtukia mchezo na kuungana kama timu moja. Akaenda Kigali na kuongea kirefu juu ya hii deal, Kagame akajenga dry port na JPM akajenga SGR.
Hivyo Samia ni muendelezaji tu wa biashara pana iliyoanza kuandaliwa mazingira ya kufanyika tangu 2015. Ndio maana ya kauli mbiu ya KAZI IENDELEE.