Ongezeko la wanawake kutoa harufu sehemu za siri

Maoni yangu ni haya;
Makungwi uchwara; kumeibuka wimbi la makungwi wenye products mbalimbali za kubana ,sijui kukata harufu mtu unaweka ukoko wa ugali, vanilla , limao , asali sijui pipi kifua wadada wengi hutumia na kuishia kupata magonjwa ambayo hata hayajulikani.

Mavazi ; unakuta mdada anashinda nguo za ndani kutwa nzima mchana jeans,tyt na kufuli usiku analala hivyo hivyo.

Usafi;unapoenda washroom unahitajika ujisafishe usipojisafisha harufu itajitokeza.

Magonjwa; either fungus or uti

Vyakula; unahijika kunywa maji sana ili kusafisha kibofu lakin unaweza kuta mchana mzima mtu anakunywa glass moja na soda soda nyingi.
Nakubaliana na ww [emoji817].... Wanaendekeza kula kula ,hovyo + kutumia midawa tofaut tofaut eti kuutunza uke .... Yan ni balaa ...ukikutana na anayetoa harufu mzuka wote unaisha
 
Iyo kutoa harufu kali sehemu za siri inasababishwa na P.I.D sikuhizi imekua shida kwa wadada wengi pamoja na fungus sugu Aya magonjwa yanasababishwa na kutoa mimba Mara kwa Mara, kutumia dawa za antibiotics Sana haya madawa ya kuzuia mimba pia namna ya kujisafisha wasichana wengi wanadhani kujisafisha kwa Kuingiza vidole na sabuni ndo wanatakata kumbe ndo wanaharibu kabisa tena wanaonuka wengi ni Hawa wadada wa mjini
[emoji817][emoji109] Hawa wanaojifanya wajanja wa mjini ...
 
Ni wakati sasa hili somo lipelekwe mashuleni form four huko au form 3, kwanini wanafunzi wasifundishwe hata kijuu juu tu juu ya afya ya uke? Wavulana na wasichana wadogo wanasumbuka sana juu ya hili, na wengi hawaelewi “what is normal na what is abnormal in a vagina”.

Kwa ujumla ewe mvulana mleta mada nikusaidie, harufu mbaya ukeni husababishwa na magonjwa ya uke ambayo mwanamke yeyote ambaye yuko sexually active hupata walau mara 1 au mbili kwa mwaka na usipokuwa makini yanakuwa ni magonjwa yako ya mara kwa mara, magonjwa hayo ni pamoja Bacterial vagnosis (BV) na Trichomoniasis, Magonjwa mengine ni gono na kaswende. (Gono na kaswende sio common kwa sasa)

Mambo mengine yanayosababisha harufu au shombo fulani lisilokuwa la kawaida ukeni, mimi haya huyaita HALI na si MAGONJWA. Mfano hali ya kuharibika kwa PH ya uke kwa sababu mbalimbali kama vile stress, Shahawa (ndio shahawa huharibu (throw away) PH ya uke, pia; kujisafisha kwa sabuni au kemikali, kujifukiza na uturi au kupaka marashi etc. haya pia husababisha harufu natural ya huko kuharibika sababu ya kupungua au kuzidi kwa bakteria walinzi wa sehemu husika hali inayosababisha ekolojia ya uke kuharibika (PH), hapa naomba nieleweke kuwa hizi nilizoziita HALI ukiziendekeza hupelekea maambukizi ya BV.

Jambo lingine ni matumizi ya dawa za kuzuia mimba, hizi hazileti magonjwa lakini mara nyingi side effects zake ni kuharibu homoni, ambapo kuharibika kwa homoni huhusishwa moja kwa moja na kuathirika kwa PH, tunarudi kule kule paragraph ya pili.

Jambo la mwisho ni kutoa mimba kienyeji na kutokusafishwa/kutokusafishwa kwa usahihi.

NB1: Kule juu sijaitaja Fungus/yeast infection sababu hii haisababishi harufu, tuache kumix mambo, yeast infection husabaisha miwasho, hubadili utoko kuwa mzito kama mafungu mafungu, hubadili rangi ya utoko (discharge) etc Dalili za magonjwa ya uke huwa zinaendana jua una dalili gani ili Dr afahamu anakutibu nini, nasema hivi sababu kwenye hospital zetu za wanyonge hizi mara nyingi hata Dr hafanyi vipimo, wanatumia uzoefu, ukichanganya dalili inakula kwako.

NB2: Magonjwa yote hutibika hospital, mgonjwa awahi hospital aonapo dalili kama , kuwashwa, ngozi ya uke kuwa nyekundu na nyepesi, kupata utoko wa rangi ya maziwa iliyokoza, njano, mawingu au ukijani. Jambo hili si la aibu kinachomtofautisha mwanamke asiye na harufu mbaya na mwenye harufu mbaya ni hali ya kujitambua, wengine wanajitambua haraka wakiona kitu hakiko sawa hivyo kutafuta matibabu haraka sana, na wengine ndio hao hawatambui chochote wanaishia kuishi na hayo magonjwa na wengine hudhani ni hali ya kawaida kuwa na harufu mbaya, tuwafunze mabinti wadogo kwa upendo kuwa si sahihi kunuka chochote katika mwili, tuwaelekeze na si kuwabully, hii ni pamoja na harufu mbaya za kwapa, kinywa na vinginevyo, kabla ya kuwasisitiza usafi tuwasisitize matibabu. Mwili wa mwanadamu ambaye ni mzima/hajafariki hautakiwi kunuka
Kongole kwako,umeeleza vyema niliwahi kuangalia kipindi cha afya siku ya jumanne Startv daktari alieleza hayo uliyoyaandika.

Na kuna kuna wimbi kubwa na madaktari feki huko instagram wanawapiga sana hela wanawake wenye matatizo hayo. Kitu cha muhimu dokta alichosema mwanamke hatakiwi aingize kitu chochote ukeni au atumie makemikali au sabuni zenye kemikali kali kusafisha uke kwasababu ngozi ya uke ni laini sana huathirika na hizo kemikali na hizo sabuni zinatumika kuoshea ngozi ya nje ambayo ni ngumu. Hivyo inaweza kufanyika hivyo kwa ushauri wa daktari maana kuna dawa zingine mwanamke huelekezwa na daktari kuzidumbukiza ukeni.

Alisisitiza kuwa uke unajisafisha wenyewe na kama mwanamke akiona hizo harufu na mengineyo awahi kituo cha afya akapatiwe matibabu sahihi.

Maoni yangu haya madawa ya kupanga uzazi nayo yamechangia sana baadhi ya wanawake kuwa na matatizo haya maana wengine baada ya kutumia hizo njia za uzazi wa mpango uke huwa mkavu hivyo huamua kutumia makemikali kuulainisha hapo balaa ndiyo linapoanzia.

Naomba niishie hapa,wasalam.
 
safi sana mkuu!
 
Mwanamke kaumbiwa mwanamme mmoja tu sasa mwanamke leo unatembea na huyu kaacha shahawa zake kesho umetembea na yule.wenyewe wanaita kudanga sasa kwann sehemu ya siri isinuke KWA halo hiyo????
aisee, inasikitisha sana!
 
Mleta mada alihitimisha kwa kusema kuwa kwenye huu uzi tutajifunza kitu,kumbe alikuwa sahihi.Nimejifunza kitu hapa.Shukrani mkuu!
nililiona hilo kabla mkuu, nikitumia zaidi uzoefu wa michango ya mada mbali mbali zitupiwazo humu kila leo. jf ni pana sana mkuu.....abarikiwe muasisi, wabarikiwe members!
 
Hauko sahihi 100%. Harufu mbaya inayotoka ukeni ni magonjwa,kwani uke hujisafisha wennyewe na hauna harufu.ukiona harufu hata kidogo ujue bacteria(uchafu).

Uke uliosafi,hautoi harufi.

NB: experience zipo ila cwez leta ushahd
sure!
 
Aisee kuna kipindi nilikutana na K moja inatoa harufu balaaa daah ilinibidi nihairishe tu gem njian baada ya kupata kimoko cha mazila na mateso ya harufu mbaya
 
Ni wakati sasa hili somo lipelekwe mashuleni form four huko au form 3, kwanini wanafunzi wasifundishwe hata kijuu juu tu juu ya afya ya uke? Wavulana na wasichana wadogo wanasumbuka sana juu ya hili, na wengi hawaelewi “what is normal na what is abnormal in a vagina”.

Kwa ujumla ewe mvulana mleta mada nikusaidie, harufu mbaya ukeni husababishwa na magonjwa ya uke ambayo mwanamke yeyote ambaye yuko sexually active hupata walau mara 1 au mbili kwa mwaka na usipokuwa makini yanakuwa ni magonjwa yako ya mara kwa mara, magonjwa hayo ni pamoja Bacterial vagnosis (BV) na Trichomoniasis, Magonjwa mengine ni gono na kaswende. (Gono na kaswende sio common kwa sasa)

Mambo mengine yanayosababisha harufu au shombo fulani lisilokuwa la kawaida ukeni, mimi haya huyaita HALI na si MAGONJWA. Mfano hali ya kuharibika kwa PH ya uke kwa sababu mbalimbali kama vile stress, Shahawa (ndio shahawa huharibu (throw away) PH ya uke, pia; kujisafisha kwa sabuni au kemikali, kujifukiza na uturi au kupaka marashi etc. haya pia husababisha harufu natural ya huko kuharibika sababu ya kupungua au kuzidi kwa bakteria walinzi wa sehemu husika hali inayosababisha ekolojia ya uke kuharibika (PH), hapa naomba nieleweke kuwa hizi nilizoziita HALI ukiziendekeza hupelekea maambukizi ya BV.

Jambo lingine ni matumizi ya dawa za kuzuia mimba, hizi hazileti magonjwa lakini mara nyingi side effects zake ni kuharibu homoni, ambapo kuharibika kwa homoni huhusishwa moja kwa moja na kuathirika kwa PH, tunarudi kule kule paragraph ya pili.

Jambo la mwisho ni kutoa mimba kienyeji na kutokusafishwa/kutokusafishwa kwa usahihi.

NB1: Kule juu sijaitaja Fungus/yeast infection sababu hii haisababishi harufu, tuache kumix mambo, yeast infection husabaisha miwasho, hubadili utoko kuwa mzito kama mafungu mafungu, hubadili rangi ya utoko (discharge) etc Dalili za magonjwa ya uke huwa zinaendana jua una dalili gani ili Dr afahamu anakutibu nini, nasema hivi sababu kwenye hospital zetu za wanyonge hizi mara nyingi hata Dr hafanyi vipimo, wanatumia uzoefu, ukichanganya dalili inakula kwako.

NB2: Magonjwa yote hutibika hospital, mgonjwa awahi hospital aonapo dalili kama , kuwashwa, ngozi ya uke kuwa nyekundu na nyepesi, kupata utoko wa rangi ya maziwa iliyokoza, njano, mawingu au ukijani. Jambo hili si la aibu kinachomtofautisha mwanamke asiye na harufu mbaya na mwenye harufu mbaya ni hali ya kujitambua, wengine wanajitambua haraka wakiona kitu hakiko sawa hivyo kutafuta matibabu haraka sana, na wengine ndio hao hawatambui chochote wanaishia kuishi na hayo magonjwa na wengine hudhani ni hali ya kawaida kuwa na harufu mbaya, tuwafunze mabinti wadogo kwa upendo kuwa si sahihi kunuka chochote katika mwili, tuwaelekeze na si kuwabully, hii ni pamoja na harufu mbaya za kwapa, kinywa na vinginevyo, kabla ya kuwasisitiza usafi tuwasisitize matibabu. Mwili wa mwanadamu ambaye ni mzima/hajafariki hautakiwi kunuka
ahsante sana kwa somo na ushauri maridhawa kabisa!

ila hapo uliponiita 'mvulana' umenikosea kwakweli.....ni wa muda sana mimi. hata uletaji wangu wa huu uzi ulisababishwa na utofauti ninaouna sasa nikilinganisha na kipindi kile cha miaka ya 90. ila nimejifariji kwamba huenda umemaanisha 'nisiye na maarifa' katika mada husika, na hilo ni kweli sababu hata bios niliishia kuisoma kidato cha pili tu sababu kwa muda huo halikuwa somo la lazima!
 
Back
Top Bottom