Ni wakati sasa hili somo lipelekwe mashuleni form four huko au form 3, kwanini wanafunzi wasifundishwe hata kijuu juu tu juu ya afya ya uke? Wavulana na wasichana wadogo wanasumbuka sana juu ya hili, na wengi hawaelewi “what is normal na what is abnormal in a vagina”.
Kwa ujumla ewe mvulana mleta mada nikusaidie, harufu mbaya ukeni husababishwa na magonjwa ya uke ambayo mwanamke yeyote ambaye yuko sexually active hupata walau mara 1 au mbili kwa mwaka na usipokuwa makini yanakuwa ni magonjwa yako ya mara kwa mara, magonjwa hayo ni pamoja Bacterial vagnosis (BV) na Trichomoniasis, Magonjwa mengine ni gono na kaswende. (Gono na kaswende sio common kwa sasa)
Mambo mengine yanayosababisha harufu au shombo fulani lisilokuwa la kawaida ukeni, mimi haya huyaita HALI na si MAGONJWA. Mfano hali ya kuharibika kwa PH ya uke kwa sababu mbalimbali kama vile stress, Shahawa (ndio shahawa huharibu (throw away) PH ya uke, pia; kujisafisha kwa sabuni au kemikali, kujifukiza na uturi au kupaka marashi etc. haya pia husababisha harufu natural ya huko kuharibika sababu ya kupungua au kuzidi kwa bakteria walinzi wa sehemu husika hali inayosababisha ekolojia ya uke kuharibika (PH), hapa naomba nieleweke kuwa hizi nilizoziita HALI ukiziendekeza hupelekea maambukizi ya BV.
Jambo lingine ni matumizi ya dawa za kuzuia mimba, hizi hazileti magonjwa lakini mara nyingi side effects zake ni kuharibu homoni, ambapo kuharibika kwa homoni huhusishwa moja kwa moja na kuathirika kwa PH, tunarudi kule kule paragraph ya pili.
Jambo la mwisho ni kutoa mimba kienyeji na kutokusafishwa/kutokusafishwa kwa usahihi.
NB1: Kule juu sijaitaja Fungus/yeast infection sababu hii haisababishi harufu, tuache kumix mambo, yeast infection husabaisha miwasho, hubadili utoko kuwa mzito kama mafungu mafungu, hubadili rangi ya utoko (discharge) etc Dalili za magonjwa ya uke huwa zinaendana jua una dalili gani ili Dr afahamu anakutibu nini, nasema hivi sababu kwenye hospital zetu za wanyonge hizi mara nyingi hata Dr hafanyi vipimo, wanatumia uzoefu, ukichanganya dalili inakula kwako.
NB2: Magonjwa yote hutibika hospital, mgonjwa awahi hospital aonapo dalili kama , kuwashwa, ngozi ya uke kuwa nyekundu na nyepesi, kupata utoko wa rangi ya maziwa iliyokoza, njano, mawingu au ukijani. Jambo hili si la aibu kinachomtofautisha mwanamke asiye na harufu mbaya na mwenye harufu mbaya ni hali ya kujitambua, wengine wanajitambua haraka wakiona kitu hakiko sawa hivyo kutafuta matibabu haraka sana, na wengine ndio hao hawatambui chochote wanaishia kuishi na hayo magonjwa na wengine hudhani ni hali ya kawaida kuwa na harufu mbaya, tuwafunze mabinti wadogo kwa upendo kuwa si sahihi kunuka chochote katika mwili, tuwaelekeze na si kuwabully, hii ni pamoja na harufu mbaya za kwapa, kinywa na vinginevyo, kabla ya kuwasisitiza usafi tuwasisitize matibabu. Mwili wa mwanadamu ambaye ni mzima/hajafariki hautakiwi kunuka