Kaka nipe info kidogo zinaweza saidia kaka..
Kaka kuna malaya na kuna mwanamke aliyewekwa ndani .
Maisha ni kubashiri kaka ila ni dhahiri ukimuweka mwanamke wa aina yoyote ndani kwako ni dhahiri shahiri umeona mnaendana tabia ,hulka na sifa hivyo mtawezana na mtavymiliana .
Kwanini tunaoa kaka ? Tunaoa ili kuwa na maisha binafsi na mtu mwingine ,kuongeza kizazi chetu ila zaidi ni tamaduni za heshima tulizorithi kutoka kwa mababu zetu ,sasa ukiamua kufanya hivi iwe kwa kupitia kanisani ,mila au hata serikalini ni wazi huyo mtu unampenda sana ,unamuamini na uko tayari kuwa upande wake leo na hata kesho vivyo hivyo kwake pia .
Sasa ni ngumu na ni ukichaa uishi na mtu ,ulale naye uchi ,ahangaike labour kuleta kiumbe chako ,ateseke kukupikia ,kukufulia ,kuwaza pamoja mipango ya maendeleo yenu hii kulingana na mila zetu alafu useme kuna vitu unatakiwa kumficha hautakuwa sawa kichwani kaka .
Sasa nasimama wapi mimi ? Mimi naamini mtu mpaka unaamua kuoa ni wazi huyo mtu na partner wa maisha yako kwa kila kitu ikotikea kubaadilika kwake basi ni ajali kazini kama ilivyo kifo kwasababu wakati mnaamua hayo yote hakuna anayejua ni lini kifo kitawatenganisga na mipango yenu baadhi haitatokea kaka ,hivyo mwanamke wa ndoa ni zaidi ya mwanamke ni wewe upande wa jinsia ya pili .
Nakupa mfano kaka ,mimi nilioa mfanyakazi ,mdada mwenye elimu yake na mwenye kujielewa na kujitambua ,ila alikuja kunigeuka baada ya kupata changamoto kazini (kuuwa pasina kukusudia ) ,hakuwa na mimi bega kwa bega ninapohangaika kuayweka sawa mambo haya na uwezo wa kuwa upande wangu ulikuwepo kwasababu cheo cha walau kunipambania alikuwa nacho kaka .
Nikawekwa ndani ,nikaa keko magereza ,finally asili ikashinda utumwa nikatoka ,nikiwa sina hata wiki nikaletewa talaka whether nakubali kusaini au nakataa ,nikakubali kusaini talaka ,siku chache akaolewa na mtu wa karibu yangu sana na watoto wakabadilishiwa kila kitu kuwa si wangu ( hapa sina ushahidi wa kusema walikuwa wangu au hapana sikuwahi kupima DNA )
Kwanini nakupitisha kwenye haya mambo yangu ni vile najaribu kukuonesha kuwa niliplay part yangu kama baba kwa kila kitu ila mwisho niliyeplay naye part hakuwa upande wangu ,sasa hii hainipi sababu kuamini kila mwanamke yupo hivyo na isitoshe simlaumu kwa kufanya hivyo ila naelewa kuna some arrasment aliwahi kupitia kutoka kwenye familia yangu hivyo naweza kusema yawezeakana alifanya hayo kwa kuhofia kuwa na mimi nipo upande wa ndugu zangu .
We made many issues kaka, tuliwekeza vingi ila baada ya talaka ilibidi nikubali baadhi viondoke kwa lugha ya kisheria ati vileee watoto hivyo hivyo ambavyo kabla ya wiki baada ya talaka naambiwa watoto si si wangu .
Kwahiyo anachojaribu kuzungumza kaka kinagoma kwasababu ukioa ukamficha mdada wa watu hivyo vitu na bado kumbe akawa ni mdada anyejitambua na likaja kukukuta jambo hauoni kama utakuwa unaiumiza familia yako mwenyewe .?
Ndiyo maana hapo awali nimesema ndoa ni Bashiri ila siku zote uwa tunabashiri upande wa mazuri pasina kuwaza upande wa ubaya hivyo kaka kama kuoa mtu akimua kuoa na aoe ila zaidi akae ajue hakuna ndoa ya mfumo anaojaribu kutusimulia mleta mada labda kama ni mkutaniko wa malaya wawili wenye lengo la kuzalisha viumbe duniani .
Ni hivyo kaka ,mpende mkeo muoneshe upendo wa kila kitu ,kwasbabu mimi naamini mwanamke akipenda anapenda kweli ila akiacha anaacha kweli .
Mwaka 2009 nilikuwa nje ya nchi ,niliwahi pendwa sana na mdada mmoja wa uingereza ila ni vile mimi sikumpenda na sikuwahi waza kuishi na ngozi nyeupe ndani kwangu sababu nina uswahili mwingi ambao niliona nitamtesa mtoto wa watu ila kichekesho ni kuwa mpaka hivi leo nazungumza na wewe bado natumiwa email mara kibao akinihitaji kwenye maisha yake lakini sasa nitasema nini kama sio hoja yangu ile ile kuwa mwanamke akipenda anapenda kweli ndugu ?
Kwa leo niishie hapa ndugu.
WABILLAH WATAUFIQ 🙏🙏