Orodha ya vitu kadhaa ambavyo Wewe Mwanaume Mkeo hapaswi kujua kabisa kuhusu Wewe

Orodha ya vitu kadhaa ambavyo Wewe Mwanaume Mkeo hapaswi kujua kabisa kuhusu Wewe

Bwana mdogo manup! Nipo kwenye ndoa zaidi ya miongo miwili.
Huna cha kunifundisha inapokuja kwenye masuala ya kuhandle ndoa yangu.
Sijakupinga kabisa mkuu, na upo sahihi kabisa kwa upande wako wala sijakuingilia kinyume na mtazamo wako
 
Hoja za andiko lako baadhi zimekaa kivulana.
Siio kweli, hii ninakupinga kwa asilimia zote 100, hakunaa uvulana kwenye hoja zangu maana zina mafunzo, utapingana nazo ila zina ukweli halisi sio wa kuchongesha maana ni kitu kimetokea na kimeshuhudiwa ndio nikaamua nikuelezee ukiona inakufaa chukua ukiona haihusiani na wewe achana nayo ishi na yako ila usiishi humo nilimokueleza yatakukuta huko mbele ya safari kuna barabara ina utelezi usiwacheke wanaoanguka mbele yako ukawaona km hawakua na akili kukuzidi wewe
 
Maisha hayana formula mkuu!
Sijakataa na wala sijakupinga, hakuna formula ila hapaswi kujua, utanishukuru ukifanya hivyo hutaki mwambie kila unachofanya, jiulize kwanini yakivurugika mambo hua wanafuta picha zote kwenye social media na kuamua kuishi low key? Jibu hujalipata haya nenda kamjulishe
 
Na yeye akikuficha kuhusu vitu vyake, Mnakuja kulalama huku JF.

Mara mke wangu mbinafsi. Unasahau hata wewe ni mbinafsi vilevile kwa kuficha ficha vitu.

Kama hutaki mkeo ajue vitu vyako, Unaoa kwa nini?

Wewe tafuta mwanamke mzae watoto tu, muwalee, kila mtu abaki na chake.
Mkuu,nitatoka nje ya maada kidogo hivi ni nini mtazamo wako kuhusu ndoa.
 
Hili nimeshatolea ufafanuzi huwajui Wanasheria? Unaishi km upo 1900 hii ni 2026 tafuta Mwanasheria wako, acha kuishi kijima
Wewe siyo nwanaume, usije kwenye vikao vyetu
 
Naunga mkono hoja

Napingana na hoja, labda side hustles ndio unaeeza kumficha.

Hii inafanana na namba mbili. Side hustles ndizo mke hapazwi kujua

Napinga hoja. Kabla ya kuoana kila mmoja aweke wazi kama ana mtoto/watoto. Na kuoa/kuolewa halafu kuzaa nje huo ni upumbavu

Naunga mkono hoja na katika hili ni muhimu kuwe na mtu wako wa karibu anaezijua hizo assets, in case of suddenly death mzigo usipotee. Asset anayotakiwa kuijua mke ni nyumba mnaylishi tu

Naunga mkono hoja. Mkeo anatakiwa kujua tu una maex lakini hatakiwi kujua ni wa kina nani
Asante sana mkuu, hizo hoja ulizopinga nahisi unachohitaji ni ufafanuzi zaidi kwanini nimesema hapaswi kujua nitazitolea ufafanuzi, kuhusu kuzaa hilo ni pigo ndani ya ndoa ikitokea umezaa nje unasema ni upumbavu ila inatokea mwanaume umezaa nje hutakiwi kukurupuka tu na kwenda kumwambia mkeo unaua ndoa ndani ya sekunde chache sana, take time before hujafungua kinywa chako na angalia unaongea nini na kwanini, sio unaongea na mkeo km shost yake Mwamtumu wa Goba atakutoa nje ya reli haraka sana, be a man & man up

Kuhusu kazi nimeshafafanua vizuri tu haina haja ya kurudia mara nyingi sana, ninaposema kazi simaanishi kazi moja, hakuna mwanaume anaeishi na kazi moja, mkeo atajua unafanya kazi hii ila una kazi zingine pembeni hizo ni kazi zako sio kazi za mkeo, hope hapo tumeelewana vizuri km unavyoziita side hustles kwa mimi naziita kazi
 
List ni ndefu ila nitataja vichache vingine wataongezea wengine hapo chini.

1. Mshahara Wako.
Mkeo hapaswi kujua wewe unapokea Mshahara kiasi gani. Fanya unavyofanya usije ukathubutu ukamwambia mkeo napokea kiasi fulani sijui nini hivi na vile, imekula kwako. Nakusanua.

2. Kazi unayofanya.
Mkeo hapaswi kujua unafanya kazi gani hata iweje wewe kikubwa una hudumia familia masuala ya kazi yako ni wewe na kazi yako mkeo haimuhusu, yeye ahudumie familia ndipo mpaka wake ulipoishia masuala ya kazi yako yeye haimuhusu na hapaswi kujua unafanya kazi gani. Nimekusanua.

3. Unapofanyia kazi. Mfano: Unafanya kazi Wapi?
Mkeo hapaswi kujua unafanya kazi wapi, unaingia saa ngapi, unatoka saa ngapi, boss wako ni nani, boss wako jina lake nani, mawasiliano ya ofisi yenu ni yapi, unafanya kazi na nani, mkeo hapaswi kujua yeye abakie na masuala ya familia masuala ya ofisini hayamuhusu maana wewe ndio unaefanya kazi hapo ofisini sio mkeo masuala yako na ya mkeo usiyapeleke ofisini utaharibu kazi. Nimekusanua.

4. Mtoto Wako au Watoto wako wa Nje ya Ndoa.
Haijalishi unao wangapi ila Mkeo hapaswi kujua uliwahi kuzaa na nani, una watoto wangapi kabla ya kumuoa au baada ya kumuoa, umezaa na nani, huyo nani yupo wapi, huyo nani mnawasiliana vipi. Mkeo hapaswi kujua.

5. Idadi ya Assets ulizonazo.
Umejenga Assets ngapi, nyumba, maduka, na Assets zingine mashamba and so on, kuwe na mipaka ya Assets anazozijua baadhi Mkeo hapaswi kujua fanya mwenyewe sio kila kitu unamwambia Mkeo, Mkeo hapaswi kujua. Nimekusanua.

6. Wanawake Uliowahi kua Nao kimapenzi.
Acha kabisa Mkeo hapaswi kujua sijui ulikua una-date na Anna, Diana, Asha sijui Amina, Ashura, Fatuma, Mwajuma, Jesca, Prisca, Joyce, etc hatakiwi kujua km uliwahi hata kufanya mapenzi na mtu mwingine yeyote kabla haujamuoa, Mkeo hapaswi kujua hio ibakie kua Siri yako wewe na Mungu wako usimwambie Mkeo, itakula kwako. Nimekusanua.

7. Nakuja kuelendea....

Kama una kingine ongeza hapo chini, sijui umetoka na limalaya gani huko Mkeo kajua jana ulilala na Malaya sehemu fulani na akaja akakuona ukiwa unamtoa sehemu huyo Malaya huku wewe hujamuona, imekula kwako. Nimekusanua. Mkeo hapaswi kujua.
Pumba tupu.
 
Sasa wewe maskini Una kitu gani cha maana Sana cha kumficha mkeo, kwenye mshahara hapo sawa lakini hayo mengine ni ujinga na utoto. Assets zenyewe ndo hizi hizi nyumba na viwanja vyenye hatua 15x20 vilivyo nje ya mji au kuna vingine kibongo bongo!!!?😀
Km hujaelewa omba ueleweshwe, una maswali unajiuliza na unauliza omba ujibiwe swali utajibiwa ila usianze na kusema sasa wewe masikini... halafu unaanza kujiuliza maswali yaan hapo masikini uliem-mention ni wewe na ukajielezea uhalisia wako na akili yako ilipoishia.. mkeo hapaswi kujua hilo pia
 
Sasa kama hutaki mkeo ajue kila kitu kwa nini umeoa? Upuuzi mtupu.
Unamuoa ili awe mkeo sio Secretary wako huyo kwamba kila mgeni anaekuja ofisini kwako yeye lazima ajue, huyo ni mkeo life partner sio business partner, copy?
 
Back
Top Bottom