Hili swali ni la kipuuzi sana.
Mimi sio Mkazi wa Dar lakini siungi mkono anayehoji upuuzi kama huu.
Ukimtaka Raia aanze kupambana na Mhalifu kwa mapanga au mikuki huko ni kuhalalisha vita kati ya Raia. Sasa utanitofautishaje mimi na Mhalifu, sio lazima nishiriki Uhalifu eti ndio nikidhi takwa la kuonekana shujaa.
Kumbuka Mhalifu yeye tayari ni Mtu aliyekwisha kata tamaa na amejiandaa kwa anachotaka kukifanya, sasa ni vipi unamtaka Daktari au Mtaalamu wa Computer naye avae character ya kihalifu ili amdhibiti Mhalifu?. kwamba unataka siku moja aende kazini amekatwa kiganja cha mkono na Mhalifu ili mumuite shujaa? hata kama yeye atakuwa amemkata huyo Mhalifu shingo lakini bado aliyepoteza ni huyu Daktari ambaye uzima wake una manufaa kwa wengi. kuna wakati tutofautishe ushujaa na ujinga.
Kama Wahalifu wamekuvamia na wanataka kuiba, uamuzi wa busara ni kuwaacha wafanye hivyo ali mradi tu wasikudhuru wewe au familia yako...na huo ndio ushujaa na sio uishie kupigwa mapanga na bado kukuibia wakuibie.
Hata hizi changamoto za kuzagaa silaha inayowakabili taifa kubwa kama Marekani ni matokeo ya kutafuta jibu la "lazima nioneshe mimi ni Mwanaume"...Wakaona suluhisho ni kila Mwananchi aruhusiwe kumiliki silaha ili ajilinde...kwenye msafara wa mamba Kenge nao wapo, sasa hivi Mpaka hao Wahalifu nao wana silaha, kule Marekani hata Kibaka tu ana bastola mkononi...ndio mnataka tufikie huko?.
SULUHISHO hapa ni kwa Jeshi la Polisi kuwekeza kwenye kupata taarifa sahihi, kwa wakati na mapema kadri inavyowezekna, sambamba na uadilifu ndani ya hilo jeshi lenyewe.
Raia wafundishwe au watafute maarifa ya namna ya kuishi kwa tahadhari na kujilinda, na sio ujinga wa kunitaka Mimi nisiyependa au nisiye na uwezo wa kufanya uhalifu nibebe panga na mimi niwe Mhalifu.
Huenda ikawa ni ngumu kutokomeza kabisa uhalifu lakini tukitumia akili na busara tutapunguza kwa kiasi kikubwa.