Panya Road waua mtu mmoja Kawe na kujeruhi wengine watatu
Shida nyingine hawa madogo ndo wadogo zenu wa daslam je unaweza choma moto mdogo wako?
 
Ndio haujawa na hautakua rais sasa kwa sababu una maamuzi ya kichoko, wewe unafikiri kua rais ni kufanyafanya tu vile unavyojisikia wewe?
Ukiwa humu JamiiForums jitahidi sana kuvumilia hata Baba yako au mjomba wako anapokosolewa. Hakuna haja ya kukasirika, Ofisi ya umma unajua siku ya kuingia lakini hujui siku ya kutoka.

Kabla hujaja kujadili humu na kujibu watu,nenda nyumbani ule uwe mtu mzima kidogo. Pole!
 
Ukiwa humu JamiiForums jitahidi sana kuvumilia hata Baba yako au mjomba wako anapokosolewa. Hakuna haja ya kukasirika, Ofisi ya umma unajua siku ya kuingia lakini hujui siku ya kutoka.

Kabla hujaja kujadili humu na kujibu watu,nenda nyumbani ule uwe mtu mzima kidogo. Pole!
Wewe Akili zako zimeganda yaan Akili zako hazina Akili... Sorry for that ila maelezo yako yanajidhihirisha wazi wewe kichwani Akili hazimo​
 
Wewe Akili zako zimeganda yaan Akili zako hazina Akili... Sorry for that ila maelezo yako yanajidhihirisha wazi wewe kichwani Akili hazimo​
Haya mkuu, pole sana, najua inauma ila itabidi uzoee tu! Utazoea taratibu.
 
Huo mji hauna wanaume?
Hili swali ni la kipuuzi sana.

Mimi sio Mkazi wa Dar lakini siungi mkono anayehoji upuuzi kama huu.

Ukimtaka Raia aanze kupambana na Mhalifu kwa mapanga au mikuki huko ni kuhalalisha vita kati ya Raia. Sasa utanitofautishaje mimi na Mhalifu, sio lazima nishiriki Uhalifu eti ndio nikidhi takwa la kuonekana shujaa.

Kumbuka Mhalifu yeye tayari ni Mtu aliyekwisha kata tamaa na amejiandaa kwa anachotaka kukifanya, sasa ni vipi unamtaka Daktari au Mtaalamu wa Computer naye avae character ya kihalifu ili amdhibiti Mhalifu?. kwamba unataka siku moja aende kazini amekatwa kiganja cha mkono na Mhalifu ili mumuite shujaa? hata kama yeye atakuwa amemkata huyo Mhalifu shingo lakini bado aliyepoteza ni huyu Daktari ambaye uzima wake una manufaa kwa wengi. kuna wakati tutofautishe ushujaa na ujinga.

Kama Wahalifu wamekuvamia na wanataka kuiba, uamuzi wa busara ni kuwaacha wafanye hivyo ali mradi tu wasikudhuru wewe au familia yako...na huo ndio ushujaa na sio uishie kupigwa mapanga na bado kukuibia wakuibie.

Hata hizi changamoto za kuzagaa silaha inayowakabili taifa kubwa kama Marekani ni matokeo ya kutafuta jibu la "lazima nioneshe mimi ni Mwanaume"...Wakaona suluhisho ni kila Mwananchi aruhusiwe kumiliki silaha ili ajilinde...kwenye msafara wa mamba Kenge nao wapo, sasa hivi Mpaka hao Wahalifu nao wana silaha, kule Marekani hata Kibaka tu ana bastola mkononi...ndio mnataka tufikie huko?.

SULUHISHO hapa ni kwa Jeshi la Polisi kuwekeza kwenye kupata taarifa sahihi, kwa wakati na mapema kadri inavyowezekna, sambamba na uadilifu ndani ya hilo jeshi lenyewe.

Raia wafundishwe au watafute maarifa ya namna ya kuishi kwa tahadhari na kujilinda, na sio ujinga wa kunitaka Mimi nisiyependa au nisiye na uwezo wa kufanya uhalifu nibebe panga na mimi niwe Mhalifu.

Huenda ikawa ni ngumu kutokomeza kabisa uhalifu lakini tukitumia akili na busara tutapunguza kwa kiasi kikubwa.
 
Nimeandika mara kadhaa na kufuta lakini acha nitoe maoni yangu bana nikikosea mtanisamehe bure.
Maoni yangu yatafuatia baada ya kujiuliza maswali:-

1. Kwani hawa panya road si wanajulikana? (they can be well identified)
Kama jibu ni ndio wakusanywe pamoja ikibidi wawekwe kwenye mifuko ya sandarusi na watupwe baharini. Sina maana lifanywe waziwazi (naomba nisilaumiwe kwa maana natural rule of thumb ni kwamba anaeuwa au kukusudia kuua naye anastahiki kuuawa). Watu wa haki za binadamu mufahamu ya kwamba tushapoteza watu kadhaa na wengine wamejeruhiwa ama kupoteza mali zao kutokana na hawa panya road. Na kama hawatambuliki hakuna budi kuwatafuta kwa kuangalia sifa na mienendo yao na kuwapeleleza ipasavyo juu ya tuhuma za upanya road na wakithibitika hiyo adhabu ya hapo juu itekelezwe.

2. Kwani hawa panya road si wana ndugu zao?
Kama jibu ni ndio wakamatwe hao ndugu zao ili watoe taarifa za vijana wao i.e wanaishi wapi na taarifa nyingine zitazosaidia kuwapata kirahisi. Iwapo wataficha kutoa taarifa sahihi na ilihali wanazo washtakiwe kwa kosa la kuwaficha wahalifu.

3. Kuna haja ya kulipa michango ya sungusungu wakati kila siku tunateseka na panya road?
Iwapo jibu ni ndio serikali za mitaa simamieni vizuri hawa vijana siyo kukusanya pesa zetu halafu watu wanaibiwa kila siku. Na nyie askari wetu (Sungusungu) mukiwapata hawa na ikathibitika kweli wahalifu chomeni moto (kwa kuzingatia natural rule of thumb ; ''he who kills intentionally must be killed''

4. Kwa nini hawa panya road wamerudi kwa kasi sana awamu hii ya mama, je ni mind set ya kuwa nchi inaongozwa na mwanamke?. Je, mama anahujumiwa ili asipate urais awamu inayofuata? Kama jibu ni ndio (kwa swali la mwanzo) na kwa kuzingatia kuwa urais ni taasisi naomba dola iamke fanyeni kitu tupunguze athari kubwa ambazo zinaweza kutokea kwa kuwalea hawa panya road. Na iwapo ni hujuma dhidi ya urais basi wanaohujumu waache its not fair. Kiukweli inauma sana tumempoteza jirani yetu siku chache zilizopita kutokana na hawa panya road.
Nimalizie kwa haya:-



Mzaha mzaha hutumbua usaha
Liwezekanalo leo lisingojewe kesho
Mtoto umleavyo ndivyo akuav
yo
Mkaidi hafaidi mpaka siku ya idi
Mchuma janga hula na wa kwao

Usipoziba ufa utajenga ukuta


Kwa kumalizia, serikali kupitia jeshi letu la polisi mutambue ya kwamba mna uwezo mkubwa kudhibiti hawa panya road kama mlivyo na uwezo mkubwa mno kudhibiti mikutano ya kisiasa kwa wapinzani (naomba nisieleweke vibaya lengo siyo kuwachafua bali kuonesha you are strong enough) ongezeni juhudi kutokomeza hawa watu mapema kabla mambo hayajaharibika. Rejeeni methali ya Usipoziba ufa utajenga ukuta.

Kodi za miamala ya simu tulipe, PAYE na SDL tulipe, kodi ya kuhifadhi pesa bank tulipe, kodi za kwenye nishati tulipe,kodi za majengo tulipe na nyingine kibao halafu mnashindwa kutulinda ili tuzitafute kisha tuwalipe vizuri.

Ng'ombe hulishwa na kupewa sehemu salama ya kulala ili azalishe maziwa ya kutosha.
NILIOMBA KUSAMEHEWA MWANZONI KABISA KAMA NITAKUWA NIMEKOSEA.
 
Kwa maeneo ya kawe na mengineyo yoyote vijana wahuni huwa wanajulikana na hata masjani zao. Jitahidi mwenyekiti wa serikali ya mtaa,mjumbe na wananchinwapige kura ya siri kuwataja nani wezi na panya road.

Itakuwa kazi rahisi sana. Tunashauri polisi ivunje na kukamata vijana wote wanaokaa chini ya miti bila kazi au kwenye maduka na magenge kucheza draft muda wa kazi. Hao ndio wezi wenyewe.
 
Back
Top Bottom