Paul Makonda: Rais Samia anarogwa sana na watumishi wake

Huyu mjinga alitumia staili hii kumtisha Magufuli kuwa anasumbuliwa na majini aliyoacha JK pale ikulu hadi Jiwe akamuamini na kumpa kandarasi ya kumletea jopo la waganga na ndiyo ilipelekea Magufuli kumuamini sana. Sasa naona anakuja na gia hiyo tena kwa Samia. Makonda ni mshirikina wa kiwango cha juu sana .
 
Mbona Hilo la kuwataja watu wanaombujumu Rais alishajibia kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa alishamtajia Rais na hakumaanisha kutaja hadharani.
 
Anakemea Washirikina wakati yeye mwenyewe anayoyafanya hapo ni ushirikina mtupu. Huyu Konda Boy Wana Arusha wasipokuwa makini atawavuruga kwa kuwatisha kuwa Arusha kumejaa washirikina.

Kwanini anazungukazunguka tu pale Arusha Mjini?? Why not Monduli, Longido au Ngorongoro?? Kuna Jambo lake pale ni suala la muda tu. Ndiyo maana anahangaika kufanya ushirikina wake kwa kuwalaghai Viongozi wa Dini. Mungu adhihakiwi.
 
Kumbe ndio wanavyopata vyeo.
Hatukujua hayo.
Yeye vipi alienda kwa mganga kuupata ukuu wa mkoa huo?
 
Kurogwa kunapimwa je sasa? Mbona huu ni uchonganishi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…