Petroli na Diesel bei Juu. Dola yaelezwa kuwa sababu ya bei kupaa
Ndugu zangu tunapaswa kufahamu kwamba, kupanda kwa dola duniani ndio chanzo kikuu cha kupanda kwa bei ya mafuta.

Tatizo la dola sio lwa kwetu Tanzania pekee yake. Ni tatizo la kidunia. Muhimu kuzingatia hilo.

Kupanda kwa dola duniani kote kumesababisha:
✅Kuongezeka kwa gharama za ununuzi kwenye soko la dunia

✅Kuongezeka kwa gharama za usafirishaji

✅Uhaba wa dola duniani kote
 
Mwanzo walisema dollar inashuka thamani ila kwa siku chache imekuwa tofauti. Hiki kikundi kinacho-control mifumo ya dunia kinazingua
 
Nchi zinazolalamika Dollar ni Africa tu, kipindi kama hichi ilibidi tutumie hata dhahabu kwenye manunuzi lakini BOT hata reserve ya dhahabu hawana.

Tunaoteseka kwenye suala la Mafuta ni Africa na Europe ila mabara mengine mambo safi.
 
Mwanzo walisema dollar inashuka thamani ila kwa siku chache imekuwa tofauti. Hiki kikundi kinacho-control mifumo ya dunia kinazingua

Kilichofanyika ni wame-hike interest rate kutoka 0.5% - 6% ndomana sarafu za Africa zimeshuka thamani against dollar. Kwa US hili linawasaidia ila linapelekea dependence ya dollar kupungua maana watu watatafuta plan B.

Tusubiri BRICS watakuja na Agenda ipi ndo mwenzi huu wanakutana.
 
Sasa naelewa!

Jana saa 1 usiku nilipita kituo kujaza wese nakuta nyomi la kutosha pump mbili tu zinafanya kazi ilhali wana pump 8 petrol ambazo hutumika kila siku hadi weekend.

+450/litre hii ni record tangu uhuru.

Na utashangaa mapendekezo ya TABOA kupandisha nauli yanakataliwa na LATRA.

"Banchi banafunguka"
 
Ni hayo tu wapendwa! Maana naona wazi kabisa hili jambo limefanywa makusudi,Ili kututoa kwenye reli tuache kujadili mkataba wa bandari,tuishie kulalamikia bei ya mafuta kupanda.
 
EWURA wamewakumbatia Bulk suppliers wako takribani 5 na wengi wao wana asili ya India. Hawa wazabuni hukaa na kupanga bei ya kuuza mafuta kwa bei waitakayo na hivyo kutufukarisha lakini baadhi ya wenzetu walioko EWURA na Wizara ya Nishati wamevuna utajiri wa kutisha.

Maswali yafuatayo EWURA kamwe hawawezi kuyajibu nayo ni:-
Kwanza, EWURA watupe sababu za mafuta kuagizwa kutoka India ambao ni wachuuzi tu wa mafuta kutoka Urusi?

Pili, kwanini EWURA hawanunui mafuta moja kwa moja kutoka Urusi ambapo pipa moja la lita 100 lauzwa dola 30 chini ya bei ya dunia?

Tatu, kwanini EWURA ni walaini sanaaaaaaa kuitia hasara taifa kwa kununua mafuta bei ambayo ni juu ya bei ya soko? India inaponunua mafuta ya Urusi kwa punguzo la dola 30 hilo punguzo hawalipeleki kwa walaji bali hubaki nalo. Pia, wanaweka kodi zao sasa ukichanganya na ufisadi uliomo humo na kodi zetu bei ya mafuta kwa mlaji lazima iwe ya juu kupindukia!

Nne, kwanini wazabuni wanaoshinda zabuni hujirudiarudia makampuni yaleyale kama hayajajijengea mtandao hapo EWURA na Wizara husika?

Tano, kwanini EWURA wao wenyewe wasiagize mafuta kutoka Urusi na kupata punguzo la dola 30 kila pipa na kuachana na kodi za India na ufisadi wao?

Sita, kwanini serikali bado imeweka kodi za EWURA katika ankara za umeme wakati wanao uwezo wa kujiendesha yenyewe? Tunasema ruzuku kwa EWURA kumechangia sana kuuwa ubunifu maana wanashawishika kuweka mbele ufisadi wao na masilahi ya taifa baadaye wakijua tutawazawadia kwa kufanya hivyo kupitia ruzuku za kodi mbalimbali.

Saba, hivi ni wahindi tu ndiyo wenye uwezo wa kuagiza mafuta?

Nane, kwanini tununue mafuta kwa dola wakati Urusi wako tayari tununue mafuta kwa hela zetu za madafu? Hivi kwanini bado tunaongelea dola wakati tupo dunia ya BRICS?

Ninawakilisha.

Pia soma: Petroli na Diesel bei Juu. Dola yaelezwa kuwa sababu ya bei kupaa
 
JamiiForums

Kupanda bei ya mafuta siyo dola kupaa bali ni ufisadi wa kutisha​

Na mimi nipo kujiuliza kwanini dola ya marekani wakati mafuta hatununui kwa mmarekani hapa wataalamu watueleweshe zaidi
Ni dola ya marekani kwa sababu bado sisi tunaitumia kama medium of exchange kwenye kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Hatuna rais wakuu
 
Huyu majaliwa alikuwa Moscow wiki hii ina maana ameshindwa kumwambia putin tununue mafuta kwa shiling vs rubble?
Wakiendaga hakuna wanachoongea zaid ya kuwakilisha tu...hawawez tumia ziara kurob....wanaenda kwa ajili ya kuwakilisha na kuongeza namba
 
Ingawaje ni kweli kuna uadimu wa USD lakini BOT ndio taasisi ya fedha inayopaswa kutolea tamko suala la uhaba au uwepo wa USD, hao wengine wanakupeni kiswahili tu...

Ni kama watu waliokuwa wanahusisha uzorotaji wa kila biashara na uwepo wa UVIKO 19
 
Ingawaje ni kweli kuna uadimu wa USD lakini BOT ndio taasisi ya fedha inayopaswa kutolea tamko suala la uhaba au uwepo wa USD, hao wengine wanakupeni kiswahili tu...

Ni kama watu waliokuwa wanahusisha uzototaji wa kila biashara na uwepo wa UVIKO 19
Kwa nini wafanyabiashara wa mafuta wasingizie Dola wakati kumbe zipo? Kwa nini bei ipandishwe ?
 
Back
Top Bottom