Petroli na Diesel bei Juu. Dola yaelezwa kuwa sababu ya bei kupaa
mkuu Tanzania viongozi wanaraha sana kuongoza makondoo. watatoa sababu VITA YA UKRAINE

Nape ata ropoka mnatumia vibaya demokrasia, mama atasema ameziba masikio, mchezo utakuwa umeisha.
 
Nawakumbusha kuwa jana Polisi wamesema hakuna ruksa kumsema Rais, hivyo ndugu zangu kila kinachotokea kifanyeni kama kimesemwa na mfanya maombi...itikieni tu EIMEEN [emoji22]
 
Huyu mama hana control tena na hii nchi maana ishamshinda watu wanafanya wanavyotaka.
Kuwa control Wafanyabiashara wa Mafuta inabidi Rais uwe mbabe Kama Magufuli, ukiwachekea imekula kwako, maana watakupa Kodi yako vizuri tu,sema na wwe usiwapangie bei ya kuuza Mafuta waacha wauuze wanavyotaka!!
 
Wadau nawasalimu.Ewura Wametangaza kuwa BEI ya MAFUTA imepanda na Kupanda kumesababishwa na DOLA kuadimika.
Je Kwanini DOLA IMEADIMIKA?
Je Kuadimika kwa DOLA Kumesababishwa na NINI?
Je ni HATUA GANI Serikali inachukua juu ya UHABA wa DOLA?
Ni vema SERIKALI ikatoa na SABABU isiishie kusema ni DOLA kuadimika.
globaltvonline_1690957703512688.jpg
 
aposto kuna muujiza………[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787]
Muujiza gani?: bei ya petrol na disel zimelipuka badala ya kupanda

Aiseee huu ni mlipuko sio mfumuko….
Sema mlipukooooooo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787]

Samia uchumi umemshinda kabisa
Lakini na Mishahara Samia si kapandisha!? Waacha na Wafanyabiashara nao wapaendeshe bidhaa zao!!
 
Hali inazidi kuwa Tete,tunarudi Kwa mwaka Jana

======
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei mpya za mafuta ambazo zinaonesha Petroli imepanda kwa sh. 443 huku Dizeli ikipanda kwa 391 kwa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa bei mpya zilizotangazwa leo na EWURA, Petroli iliyokuwa inauzwa sh. 2,736 imepanda hadi 3,199 huku Dezeli iliyokuwa inauzwa sh. 2,544 imepanda hadi 2,935, kwa Dar es Salaam bei ambazo zitaanza kutumika kesho Jumatano, Agosti 02,2023 saa 6:01 usiku.

Aidha EWURA imesema sababu za mabadiliko ya bei hizo kwa mwezi Agosti 2023 ni changamoto za upatikanaji wa Dola za Marekani, mabadiliko ya sera za kikodi, kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta.

Imesema kwa mwezi Agosti 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mikoa ya Tanga yatauzwa sh. 3,245 na Mtwara ni sh. 3,271.
Tuliandika sana kuhusu uhaba wa dola, wewe ChoiceVariable na maroboti mengine yakapinga.

Sasa mnakubali kuwa kuna uhaba wa $$$$!!??
Mficha maradhi,kifo humuumbua.
 
Huu mlipuko wa bei ya mafuta unaenda kupandisha kila kitu, halafu mishahara ya watumishi imebaki ileile kiduchu.....nchi hii imeharibiwa sana na hawa wanasiasa wachumia tumbo wasiokuwa na vision wala ubunifu wowote, empty set!​
"Lile Jambo letu liko pale pale Watumishi msijali"
 
Hapo kuna watu wanapata mabilioni ndani ya siku 1 maana kama mtu alikuwa na lita milioni 2 tayari faida kapata na hii ilitegemewa maana mafuta yalifichwa mapema mno, maana bei ilishajulikana itapanda
Mwezi unaokuja itapanda tena maana dollar itakuwa imefika 2700 hivyo lita itafika 3500 hadi mwaka uishe mafuta yatakuwa 4000 huko

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Lita 500,000 nikizitoa, mwezi ujao nafungua vituo viwili vya mafuta huko kuelekea Kusini.
 
Bei ya mafuta iachwe ipangwe na soko, serikali iingilie pale inapoona imezidi sana.
Soko huria laweza kushusha bei kwa zaidi ya 20% kwa kuondoa ukiritimba na rushwa inayoweza kujitokeza.
Siku hizi hakuna Soko huria tena, ni mwendo wa Soko holela, Wafanyabiashara hawashindani bali hukaa na kukubaliana bei ya kuuza na kiasi Cha Mzigo kitakacholetwa kwenye soko kwa ajili ya mauuzo!!
 
Back
Top Bottom