Petroli na Diesel bei Juu. Dola yaelezwa kuwa sababu ya bei kupaa
Kwa utawala wa mama, hilo ni ongezeko la kawaida na haguswi na hali zetu. Sana sana atamuuliza Madilu kama kuna namna ya kuweka tozo mpya wakusanye hela za kujengea miundombinu waliyoikopea mikopo.

Tuendelee kusali maana kadiri tunavyosogelea uchaguzi ndivyo mkwamo unavyozidi kutufungua akili
Ndio tuna mwanasesere pale hatuna raisi walllahi
 
Duh! [emoji849] hii ni maajabu!
Hadi unaambiwa jana nilikuandikia ki-memo bado unaamua kumlinda huyo wa ewura?
Amani chanzo chake ni haki!
Hakuna lisilo na mwisho.
Kila la kheri speaker!
 
Kama una bundle jionee mwenyewe. ...
View attachment 2707883

IMG_4024.jpg

Tulia unaulizwa huku na waziri
 
Duh! [emoji849] hii ni maajabu!
Hadi unaambiwa jana nilikuandikia ki-memo bado unaamua kumlinda huyo wa ewura?
Amani chanzo chake ni haki!
Hakuna lisilo na mwisho.
Kila la kheri speaker!
Yule wa Ewura Dr Mwainyekule ndio mume wa Tulia
 
Hali inazidi kuwa Tete,tunarudi Kwa mwaka Jana

======
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei mpya za mafuta ambazo zinaonesha Petroli imepanda kwa sh. 443 huku Dizeli ikipanda kwa 391 kwa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa bei mpya zilizotangazwa leo na EWURA, Petroli iliyokuwa inauzwa sh. 2,736 imepanda hadi 3,199 huku Dezeli iliyokuwa inauzwa sh. 2,544 imepanda hadi 2,935, kwa Dar es Salaam bei ambazo zitaanza kutumika kesho Jumatano, Agosti 02,2023 saa 6:01 usiku.

Aidha EWURA imesema sababu za mabadiliko ya bei hizo kwa mwezi Agosti 2023 ni changamoto za upatikanaji wa Dola za Marekani, mabadiliko ya sera za kikodi, kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta.

Imesema kwa mwezi Agosti 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mikoa ya Tanga yatauzwa sh. 3,245 na Mtwara ni sh. 3,271.
Team Russia ivi sarafu yenu inakuja lini tuipindue dola ya marekani?
 
Back
Top Bottom