Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Jiji Dar es Salaam, jimbo la ukonga ambalo limebahatika kufikiwa na mradi wa kimkakati wa ujenzi barabara ya mabasi ya mwendo kasi, wananchi wake wanateseka na kutaabika na foleni
Foleni hii ambayo inasababishwa na ubovu mkubwa wa barabara kuanzia maeneo ya njia panda ya segerea na mlima wa magereza uliosababishwa na mkandarasi kung'oa na kuharibu mtandao wa barabara uliokuwepo awali na hivyo kufanya magari yasipite kwa urahisi na mengine kuharibika kutokana na mahandaki na mashimo makubwa ya barabarani.
Kwa sasa kutoka Ukonga Mombasa mpaka ufike Banana unaweza kutumia masaa manne hadi sita kila siku
Cha kusikitisha ni kwamba wakandarasi wa mwendokasi wameharibu mfumo wa barabara uliokuwepo lakini hakuna shughuli inayofanyika. Swali ni kuwa kwa nini waliharibu eneo ambalo hawakuwa na matumizi nalo?. Na hata baada ya kuona kuna adha hivi kwa nini hawachukui hatua kuirekebisha?
Ina maana mamlaka hazioni? Je hii ni dharau kwa wananchi wa ukonga? Mbunge wa Ukonga hata kama hukai jimboni, huna watu wa kukupa taarifa ya hali ilivyo usaidie kutetea wananchi wako?
View attachment 2805624View attachment 2805625