Picha: Tupatie update ya eneo lako husika- El nino 2023/2024
Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Jiji Dar es Salaam, jimbo la ukonga ambalo limebahatika kufikiwa na mradi wa kimkakati wa ujenzi barabara ya mabasi ya mwendo kasi, wananchi wake wanateseka na kutaabika na foleni

Foleni hii ambayo inasababishwa na ubovu mkubwa wa barabara kuanzia maeneo ya njia panda ya segerea na mlima wa magereza uliosababishwa na mkandarasi kung'oa na kuharibu mtandao wa barabara uliokuwepo awali na hivyo kufanya magari yasipite kwa urahisi na mengine kuharibika kutokana na mahandaki na mashimo makubwa ya barabarani.

Kwa sasa kutoka Ukonga Mombasa mpaka ufike Banana unaweza kutumia masaa manne hadi sita kila siku

Cha kusikitisha ni kwamba wakandarasi wa mwendokasi wameharibu mfumo wa barabara uliokuwepo lakini hakuna shughuli inayofanyika. Swali ni kuwa kwa nini waliharibu eneo ambalo hawakuwa na matumizi nalo?. Na hata baada ya kuona kuna adha hivi kwa nini hawachukui hatua kuirekebisha?

Ina maana mamlaka hazioni? Je hii ni dharau kwa wananchi wa ukonga? Mbunge wa Ukonga hata kama hukai jimboni, huna watu wa kukupa taarifa ya hali ilivyo usaidie kutetea wananchi wako?View attachment 2805624
 
Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Jiji Dar es Salaam, jimbo la ukonga ambalo limebahatika kufikiwa na mradi wa kimkakati wa ujenzi barabara ya mabasi ya mwendo kasi, wananchi wake wanateseka na kutaabika na foleni

Foleni hii ambayo inasababishwa na ubovu mkubwa wa barabara kuanzia maeneo ya njia panda ya segerea na mlima wa magereza uliosababishwa na mkandarasi kung'oa na kuharibu mtandao wa barabara uliokuwepo awali na hivyo kufanya magari yasipite kwa urahisi na mengine kuharibika kutokana na mahandaki na mashimo makubwa ya barabarani.

Kwa sasa kutoka Ukonga Mombasa mpaka ufike Banana unaweza kutumia masaa manne hadi sita kila siku

Cha kusikitisha ni kwamba wakandarasi wa mwendokasi wameharibu mfumo wa barabara uliokuwepo lakini hakuna shughuli inayofanyika. Swali ni kuwa kwa nini waliharibu eneo ambalo hawakuwa na matumizi nalo?. Na hata baada ya kuona kuna adha hivi kwa nini hawachukui hatua kuirekebisha?

Ina maana mamlaka hazioni? Je hii ni dharau kwa wananchi wa ukonga? Mbunge wa Ukonga hata kama hukai jimboni, huna watu wa kukupa taarifa ya hali ilivyo usaidie kutetea wananchi wako?View attachment 2805624View attachment 2805625
Mbunge wenu si kapewa Uwaziri Kuzi au Sio Slaa?
 
hapo swala lilikuwa rahisi tu kwa sababu njia ya kuingia na kutokea banana ni moja inayosababisha gari kusubiriana hapa mlima wa gereza,traffic polisi waweke ratiba kwa magari kupita,dakika 20 gari zinaenda,dakk 20 gari zinarudi.

kuliko sasa ukifungiwa majumba 6 na ist yako ujue una masaa 4 ya kusubiri hapo,na wao wapo wanalowana na mvua bila matokeo.
 
Nchi ipo tepe tepe
 
Back
Top Bottom