Picha: Tupatie update ya eneo lako husika- El nino 2023/2024
Mvua ni balaaa ni balaaa sana niki riport kutoka katikati ya eneo lenye mishe mishe Mingi Tanzania (Kariakoo)hali sio shwari.....

Inanikumbusha Eli-nino ya 97/98 nikiwa Mwanza Tz
 
Wakati wa jua huwa inatamanika ukilinganisha na wakati wa mvua.
Jana usiku nimepita kwa "dada zetu" hapa sokoni maji yamejaa mpaka milangoni.

Ajabu ni kwamba Dar ndio inachapa kweli...lakini mikoani hali nzuri...capital city as of now
 

Attachments

  • Screenshot_20231102_154805_Gallery.jpg
    Screenshot_20231102_154805_Gallery.jpg
    184.8 KB · Views: 7
Aisee
Hii mvua ni kiboko

Ipo kutunyoosha yaani
Chaah

Napita pale Mbezi mitaa ya crdb kule
Ni maji,tope


Hii mvua Mungu hamishia mikoani aisee

DSM ni heri kuendelee kuwa na joto kuliko hii mvua.
 
Kwa wazee wenzangu wa makamo, mnakumbuka ile el nino ya mwaka 1998, jiji nusura lizame, barabara na madaraja yaunganishayo nchi yalibomoka na kuondoka kabisa. Zama hizo kupeana taarifa ilikuwa kwa barua, fax, telex, radio call (simu ya upepo), telegram, nk.

Tusirudie makosa yale, tulipoteza ndugu zetu wengi kwa kuwa hawakuwa na tahadhari ya usalama wa huko waendako.

Leo mambo yamebadilika, taarifa, tahadhari na habari vyaweza kusambaa kwa kasi ya mwanga. Karibuni tuutumie uzi huu kulashana taarifa kwa lugha ya picha na video, eleza eneo na kinachojiri, utamsaidia ndugu, jamaa, na hata rafiki yako pia
 
Back
Top Bottom