Picha: Tupatie update ya eneo lako husika- El nino 2023/2024
Mvua kwa Dar ni kuivua nguo hapafai ni kero tu ila afadhali joto limepungua
 
Wakuu, tujuzane huko ulipo hali ikoje kwa picha na video, na kama kuna sehemu ina changamoto toa taarifa haraka kwa mamlaka husika kuepusha athari kubwa.

Bila kusahau, tuchukue tahadhari kipindi hiki chote cha mvua.

Mzazi, kama mtoto wako anasoma mbali na miundombinu ni mibovu ni bora ukaacha leo apumzike, asije kukutana na majanga ukaishia kujuta.

Wengine wamekutana na majanga asubuhi asubuhi, jamaa kanasa kwenye mtaro maeneo ya Tegeta

Tangu jana usiku mpaka sasa ni mvua Tanga mjini. Naelekea Dar nione hali ikoje maana kuna makazi bondeni kidogo
 
Hasa kule kwenye mabwawa ya majitaka
Natoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Jiji kwa kukosa maadalizi ya mvua miaka yote. Hii inatokana na hali ifuatayo barabarani;
1- Mifereji kujaa taka ngumu na mchanga isiyoruhusu maji kupita na kusababisha kujaa mitaani.
2-Chemba za mifereji kutokua na mifuniko migumu inayo sababisha watu, magari na pikipiki kutumbukia. Hizi utazikuta hata katikati za barabara za lami.
3- Uchafu wa chemba zilizofukuliwa kuachwa pale pale ili irudi tena au kuzagaa kote.
4- Kutokufunika mifuniko ya chemba vizuri na ibaki upande na wazi ili tairi za pikipiki au gari zigote pale hadi kuvunjika.

Natafakari sana usimamizi wa vitengo hivi hadi hali kuwa hivi. DAR ni mji wa Mega City na sura ya Tanzania
 
😂😂Au ndio yule alisema sijui mkono ✋ ulitoka wapi nilisikia tu paaa nikaona jua linachomoza wakati ilikuwa jioni
🤣🤣🤣🤣🤣
Tuache masihara popoma ameadhibiwa sana na wajeshi pale Kawe🤣🤣🤣
 
Kwa utabiri inaonekana wiki hii tutashinda na mvua na tutalala na mvua sasa ukubwa wa kiasi gani na wapi zaidi itanyesha sijui ila tujiandae.
 
20231102_133059_HDR.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom