Kwa wazee wenzangu wa makamo, mnakumbuka ile el nino ya mwaka 1998, jiji nusura lizame, barabara na madaraja yaunganishayo nchi yalibomoka na kuondoka kabisa. Zama hizo kupeana taarifa ilikuwa kwa barua, fax, telex, radio call (simu ya upepo), telegram, nk.
Tusirudie makosa yale, tulipoteza ndugu zetu wengi kwa kuwa hawakuwa na tahadhari ya usalama wa huko waendako.
Leo mambo yamebadilika, taarifa, tahadhari na habari vyaweza kusambaa kwa kasi ya mwanga. Karibuni tuutumie uzi huu kulashana taarifa kwa lugha ya picha na video, eleza eneo na kinachojiri, utamsaidia ndugu, jamaa, na hata rafiki yako pia