Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,439
- 145,410
- Thread starter
-
- #81
I am for whatever it takes.Bodycam inakusanya data na kuzituma kwingine on a real-time basis? Kama sivyo, wakikupoteza unapotea na data zako!
Hujaeleweka.Naona watu wengi sana hapa mnachangia comments zenu lakini bila ya kujua kwa undani kuhusu uzito wa tatizo ambalo Wananchi wa Tanzania wanakabiliwa nalo kwa Sasa.
Hali iliyopo hapa nchini kwa Sasa ni sawa kabisa na hali jinsi ilivyokuwa kule nchini Afrika Kusini enzi za Utawala wa Ubaguzi wa Rangi mara tu baada ya Chama Cha Upinzani Cha ANC wakati huo kufutiwa Usajili wake kama Chama Cha Siasa na kisha Chama hicho kilipigwa marufuku na Utawala wa Makaburu na mwisho kabisa chama hicho kutangazwa kuwa ni Kundi la Kigaidi.
Watu hao waliokwenda nyumbani kwa Mdude Nyagali na kumteka kwa nguvu wanaonekana walikuwa ni Task Force.
Siyo rahisi kueleweka na kila Mtu, haiwezekani.Hujaeleweka.
Camera zipo kila kona ya nchi hii wewe.Wewe huko kwenu usukumani umeweka cctv nyumbani? Au unajisemea tu kwa kuwa uko majuu maboxini kwa hiyo unaona kila kitu ni rahisi?
Kijiji cha Nkotokwiana, Newala vijijini.Unaishi wapi wewe? Zizini?
Watu mna mindset za kichovu na kiunyonge sana.Polisi wetu hata waliyoyafanya hadharani wanayakataa, sasa ukiweka kamera ndiyo watakubali? Juzi hapa wamebeba watu mchana kweupe kwenye magari yao hapa mahakam ya kisutu, na wakaenda kuwapiga na kuwadhuru wanachadema.
Siku hiyi hiyo Jeshi la Polisi walikataa kwamba sio wao na video zipo zikiwaonyesha wao wakiwakamata watu kisutu na kuwaweka chini ya ulinzi na kuwapandisha kwenye magari yao ya polisi.
Sasa nini kitawafanya wakubali kwamba wao ndio wahusika wa kila uovu nchi hii.
Wote tunaelewa anakingwa Mamaaaa ashinde, lakini huwezi kuwa mwehu kusema kwamba kwasababu Nyumba ya Mdude Nyagali haina kamera basi polisi hawahusiki.
Tundu Lisu aliposhambuliwa Dodoma waliondoa video wao hao hao polisi, na walikana hawahusiki.
Hoja kama hizi hazina faya yoyote, wananchi wantekwa majumbani na barabarani na polisi wamekanusha zote.
Nchi hii itapona tukipata jeshi letu wananchi, viongozi wakabaki na majeshi yao naamini tutawashinda.
Haya, acha basi waendelee kuuliwa na kuumizwa tu kiboya boya.Kuhamasisha watu kujichukulia sheria mkononi ni ushamba wa kitoto.
Kiongozi ulinzi na usalama wako unaanzia kwako binafsi, hata Yesu mwenyewe hakukaa hivi hivi alikuwa anatembea na kakikundi wamejizatiti kiulinzi.. kwa maana walijua wanawindwa na tawala ya kipindi hiko...Naona watu wengi sana hapa mnachangia comments zenu lakini bila ya kujua kwa undani kuhusu uzito wa tatizo ambalo Wananchi wa Tanzania wanakabiliwa nalo kwa Sasa.
Hakika! …Sijui watawala wanaipeleka wapi hii nchi. Bila mass (popular) uprising, I am afraid, hii nchi haitarudi kwenye mstari!I am for whatever it takes.
Nadhani zipo ambazo zinahifadhi data kwingineko kiasi kwamba hata bodycam ikiharibika, bado data zako zitakuwepo mahala.
Mimi nina dashcam inayorekodi ndani na nje. Hata kama siendeshi gari, camera ina uwezo wa ku detect impact na kuanza kurekodi.
Na inahifadhi kila kitu kwenye app/ account.
Na hata kama bodycams hamna zinazopeleka data kwingineko, ni bora kuwa nayo kuliko kutokuwa nayo.
I am for anything that can help.
Sitaki watu wawe helpless kabisa.
Mfano huyo Mdude hata hatujui hao watu waliompiga wanafananaje.
Interesting… Nilikuwa sijui kwamba wanaoteka na kutesa/kuua watu wanafuata sheria!Kuhamasisha watu kujichukulia sheria mkononi ni ushamba wa kitoto.
Hao polisi na wanajeshi ana uhakika gani kuwa ndio watekaji? Msukuma mmoja akiwa mwizi wa ng'ombe ina maana wasukuma wote ni wezi wa ng'ombe?Interesting… Nilikuwa sijui kwamba wanaoteka na kutesa/kuua watu wanafuata sheria!
Hivi umeelewa hata nilichokiandika wewe?Hao polisi na wanajeshi ana uhakika gani kuwa ndio watekaji? Msukuma mmoja akiwa mwizi wa ng'ombe ina maana wasukuma wote ni wezi wa ng'ombe?
Basi siku nyingine andika kiswahiliHivi umeelewa hata nilichokiandika wewe?
Unazidi kunitoa usingizini. Nilikuwa sijui kwamba April 24, 2025 pale Kisutu vilikuwepo vyombo vya dola sanjari na wale watekaji ambao wamekuwa wakitafutwa na polisi kwa muda mrefu bila mafanikio. Siku ile tena watekaji walifanya yao mbele ya polisi na kuwapeleka mateka wao kwenye pori la Mabwepande! Isn’t this interesting?Hao polisi na wanajeshi ana uhakika gani kuwa ndio watekaji? Msukuma mmoja akiwa mwizi wa ng'ombe ina maana wasukuma wote ni wezi wa ng'ombe?
suala limetoka katika level ya utashi wa watu na kuonekana ni wa kitaasisi, hata kama sio wa kitaasisi, Polisi au Mtumishi yeyote akifanya mambo ambayo ni kinyume na kiapo chake anatia doa taasisi nzima hata kwa wale walio wasafi. Samaki mmoja akioza ni woteHao polisi na wanajeshi ana uhakika gani kuwa ndio watekaji? Msukuma mmoja akiwa mwizi wa ng'ombe ina maana wasukuma wote ni wezi wa ng'ombe?
Afu anachosha content zake za Jina lake havifanani kabisaHivi umeelewa hata nilichokiandika wewe?
Acheni uhuni,unajua mama amekuwa mpole sana ila kuna watu wachache wanataka kumkwamisha.Utani utani tu Kuna siku hii nchi itakuwa si sehemu salama kwetu wote.Mama kakausha,ni kama vile mzanzibar aliyetumwa kuiharibu Tanzania bara.
Angekemea hivi vitendo kujiepusha na hizo lawama, Polisi wanatumia nguvu kupita kiasi kwa watu ambao hawana silaha yeyote, anaepukaje hizo lawama?Acheni uhuni,unajua mama amekuwa mpole sana ila kuna watu wachache wanataka kumkwamisha.
Sasa ujue mtu mwema anaweza kuwa na watu wanampambania na yeye hawajui kabisa.
Kuna Mwaka kipindi cha Nyerere yalitokea mambo kama haya Waziri mwenye dhamana aliwajibika kuonyesha kuwa lilikuwa jukumu lake kusimamia vyombo vitimize majukumu yao kwa mujibu wa sheria, Yaani mtu anayesimamia sheria anayetakiwa awafundishe wengine utekelezaji wa sheria yeye ndo anazivunja.Acheni uhuni,unajua mama amekuwa mpole sana ila kuna watu wachache wanataka kumkwamisha.
Sasa ujue mtu mwema anaweza kuwa na watu wanampambania na yeye hawajui kabisa.