Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 42,525
- 74,605
Bora kidogo kidogo......huu mwaka utaishaje sasa kama akimaliza yote?Afunguke nae, asilete mambo robo robo.
Bora kidogo kidogo......huu mwaka utaishaje sasa kama akimaliza yote?Afunguke nae, asilete mambo robo robo.
asikupotezee muda huyo zwazwaWewe na nani? Kwa Nini husemi unataka kujua aliko Mdude na wengine? Kwani ambaye kapotezwa ni Ben tu?
Ukisema huna interest na hayo mengine jisemee wewe! Mimi nataka kusikia yote maana ni ya muhimu. Kama unaona hilo unalotaka si miongoni mwa atakayozungumza, usimsikilize, wengine acha wasikilize.
Tulia usiwe na haraka kila kitu kitakua wazi kamanda.Safari ya JPM Moro ndiyo iliyoleta shida?
Kipindi cha kampeni hiki mtandao wazeime kwa nini?Sina hakika kama huo muda mtandao utapatikana! Hizo dondoo alizo ainisha hapo ni kubwa mara kadhaa kuliko zote alizo wahi kuelezea.
Nimeona kuna makontena nadhani ni Kibaha bandari kavuWazee wa code background ya alipo kaa polepole ni America au ulaya?
Mwaka huu wanaisoma! Wakamfungia Lissu milango ya gereza akaibukia kufungua shule mahakamani wakagwaya na kuzuia.
Heche akakiwasha kwa moto wa gas kabisa naye wakamzimia mic eti hastahili kusema chochote.
Mungu kamuibua Polepole hawajui hata yupo mtaa gani, sasa wanajuta hata kwa nini wamemkorofisha huko Ubalozini wakati anayajua mengi ya CCM kuliko hata Wassira!
Sijamsikia Polepole akisema lolote kuhusu haja ya katiba itakayokuwa ya vyama vingi kwa dhati. Katiba isiyoweka vipengele vya kulinda chama kimoja. Katiba isiyompa msajili uwezo wa kukwamisha vyama.
Yeye ni Samia asigombee. Kana kwamba asipogombea ghafla demokrasi yetu itakuwa imeimarika. Vipi mbele ya safari tukipata Samia mwengine.
kwanza hyo HP asingejalibu kufungua hlo bakuli..Magu alikuwa hataniwi..Mama ni Mpole sana ila natarajia hatokuwa hvo awamu ya pili kwani kisha wasoma wanaomzunguuka.Shida yake ni Samia, mchakato ukirudi tena mezani na akapatikana mgombea anayemtaka yeye hata kwa msaada wa RA kwake haitakuwa shida.
Leo hii angekuwepo JPM amejiongezea muda agombee tena sidhani kama ingekuwa shida Kwa HP na sidhani kama CCM ingekuwa mbaya kwa HP.
Tunahitaji kuwa makini kuliko Umakini wenyewe ili kuwe na consistency.
ndani ya mitaa ya Khartoum Sudan
Kabisaaa, aseme wazi hapa.Siku Magufuli anafariki, Saa100 aliibukia Ziara ya Mkoa wa Tanga !
Pole pole tuambie Saa100 alikuwa likizo huko kwao Unguja, aliibukia wapi na kwenda ziara wakati mwenzake anakata moto ???
Noma sana, pole pole amekuwa media kamili.View attachment 3456894
Miongoni mwa atakayozungumza:
1. Biashara za Rostam Aziz
2. Ziara ya Magufuli Morogoro, na mazungumzo yao kuhusu Rostam
3. Kashfa ya Uniform za Jeshi la Polisi ambayo kesi yake ilikuwa stori nyingine baada ya Magufuli kufariki
4. Wezi wanakoficha pesa
5. Kashfa ya kukomboa ndege Afrika Kusini
6. Code aliyotoa JK Kawe kwenye uzinduzi wa kampeni
7. Miradi 4 ya 2020
8. Tathmini ya deni la Taifa
9. Kiini macho cha ahadi za CCM kwenye uchaguzi wa mwaka huu na utekelezaji wake
10. Uteuzi Haramu wa Rais Samia
11. Uhuru wa vyombo vya Habari
Muda: Saa 3:00 Usiku