GE2025 Polepole: CCM wanakwenda kwenye Uchaguzi sababu wana uhakika kushinda kwakuwa kuna mifumo inawabeba

GE2025 Polepole: CCM wanakwenda kwenye Uchaguzi sababu wana uhakika kushinda kwakuwa kuna mifumo inawabeba

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Sio kwamba zimedukuliwa, zimeunganishwa rasmi kuwa kama mfumo mmoja kwa sasa.

Kwahiyo CCM wana access na mifumo hiyo mingine ya NIDA na tume ya uchaguzi na wanapewa ushirikiano wa kutosha na hizo taasisi anavyosema Polepole.

Kwenye mazingira kama haya unahitaji mtu kama Jaji Warioba kufanya uchunguzi wa kina.
Uchunguzi gani tena ndugu???
Kuelewa kwako kuna.......
 
Hayo maswali sita niliyoulizwa mpaka sasa sijapata majibu na hata Polepole hana majibu yake
 
Utaishtaki kwa mahakama ipi dawa ni kuwaachia waliopewa baiskeli na pikipiki za bure wakapige kura wao wenyewe
 
Wajanja tunajua hizi njama kitambo sana! Umesikia wanasema wamejiandikisha watu milioni sijui ngapi. Wale ni watu wa NIDA. [emoji16]

Hii nchi ukishaijua, haikusumbui yaani. Werevu wengi hatupigia kura since 2000. Naam
Eti watu wazima wote wamejiandikisha haiwezekani
 
nimekuelewa hapo kuna kikwazo unashauri nini kifanyike ?
Ni katika mwendelezo ule ule. Wamekataa kufanya "REFORMS"; na hawana sababu ya kufanya hayo anayo pendekeza Polepole; kwa sababu hizo ni njia za kuwaondoa madarakani kistaarabu.

Sasa utaniuliza kama hawataki njia za kistaarabu, waTanzania wamebakiwa na njia zipi za kuwaondoa?
 
Mifumo ya hiyo NIN na NEC inawiana na sasa naelewa kwa nini ili mtu awe mkurungenzi wa taasisi inayotoa NIN lazima awe afisa kipenyo na huku kwenye NEC anakuwepo jaji kipenyo.

Nikuulize mleta mada unafikiri kwanini kulikua na haja ya CCM kurekebisha sheria za uchaguzi na kuweka vipengele hivi.

Simu hazitoruhusiwa kwenye kituo cha kupiga kura isipokuwa polisi na wasimamizi wa uchaguzi[ hawa ni CCM waliojivika vazi ]

Matokeo kutangazwa mahali popote na msimamizi wa uchaguzi.

Kura zinaweza kuhesabiwa kokote ambapo msimamizi wa uchaguzi ataona panafaa[yaani kura za A+B+C zinaweza kusanywa na kubebwa na polisi kwenda station Z kuhesabiwa na kufanyiwa majumuisho]

Hebu jibu hayo maswali tuone kama hakukua na nia mbaya

Note: uchaguzi wa Kenya IEBC wanaruhusu wakala kuingia na simu na anaweza kupiga picha fomu ya matokea katika kituo na kuituma bila tatizo lolote.

Msikie hapa Kikwete akielezea uchaguzi wa Kenya halafu akashindwa kushauri yafanyike Tanzania mnasubiri hadi machafuko kama Kenya ndio mrudi kwenye drawing board?


View: https://youtube.com/shorts/nYIC70_Tzl0?si=rVMotKaff2Fo0QEJ
 
Si huwa nawaambia msishiriki chaguzi zinazoendeshwa na kuratibiwa na tume ya uchaguzi iliyoundwa na CCM lakini huwa mnaniona hamnazo!

Hadi aseme Polepole ndo muamini kwamba mnajisumbua?

Where is your common sense?
Samahani mkuu,tulichukuliwa msukule tukawaamini wahuni.
Way forward ni kusubiri mchakato wa reconciliation ili Tanzania ianze upya ,tusonge mbele!
 
Yaani kuna mambo yanahuzunisha sana yaani inafika kipindi unaweza akukufuru Mungu Kwa baadhi ya vichwa vilivyokuwepo humu ndani na wenyewe wanajiona wako sawa kabisa
 
Una hoja Sana ila wanavyojibu ndo maana tunaitwa nyumbu

Hata Mimi nimebaki kujiuliza how mfumo uibe wakati kura zinahesabiwa ndani ya chumba mbele ya mawakala
Najua CCM wanaibaga kura Ila labda uniambie kwavituo hewa,rushwa kwa mawakala n.k

Hili la inec na NIDA sijalielewa

Nyumbu ni wewe stupid. Huwezi kuelezea kitu bila kutoa lugha ya matusi. Stupid idiot
 
Wakuu, Kuna jambo Kalisema Polepole, ila linapuuzwa ili kuonekana halina maana, ukweli ni kua UCHAGUZI HAUNA MAANA TENA KWA JAMBO HILI.

Wakuu kuanzia Leo nimemaini TUNDU LISSU ni NABII WA MUNGU , kama alivyokus Mussa.

LISSU amekomaa sana kwenye Mkutano kuhusu Servers za Tume ya Uchaguzi, LISSU kasema tunataka Vyama vya Siasa turuhusiwe kukagua , inawezekana LISSU alikua analisema bila kujua chochote na bila utaalam wowote.

Leo POLEPOLE kaliweka wazi hili , CCM walotengeneza Mfumo wa kikomoyuta ambao una Link Taarifa za Mfumo mitatu yaan CCM +NIDA+NEC , Kwa kuunganisha Mifumo hii mitatu, CCM WANAUHAKIKA WA KUZALISHA USHINDI WA KURA MAPEMA KABISA HATA KABLA YA UCHAGUZI.


Polepole ameomba Mungu amsamehe kwani Kwa Sasa ni kiumbe Kipya .


WAKUU ITOSHE KUSEMA, TUMEUMIZWA SANA NA CCM, LEO NMESHIKWA NA HASIRA SANA, KUMBE WATANZANIA WANAPOTEZA MUDA KWENDA KUPIGA KURA, KUMBE KURA YA MTANZANIA NI TAKATAKA MACHONI MWA CCM, KUMBE CCM MPAKA MIDA HUU TAYARI WAMESHASHINDA UCHAGUZI MKUU.


Kiufupi Ndugu zangu, HAKUNA UCHAGUZI, CHADEMA TUKOMAE NA NO REFORMS NO ELECTION!!!
Nyie c mmesema hampigi kura 😃
 
Kuna vitu Havi hitaji hata Kuitumia Nguvu kujua. Jibuni hoja za pole pole.

Hivi pale kwenye tume inayoitwa Huru wale makada wa ccm Ambao ni makamishna wa tume wanafanya Nini?

Sasa wewe una mkabidhi paka Akulindie Safuria la samaki Utegemee Atakuwa Mwadilifu?

Yaani Mzee Mapuri Aone ccm imekataliwa Alafu Akubali?

Hivi yule Bwana Jecha Kule Visiwana Alipokataa kutangaza Ushindi wa Mzee Maalim Shariff Alafu Mwaka 2020 Akachukua fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar kama Mwanachama wa ccm hapo haiitaji Akili ya darasani kujua ccm inachezea kura za Watanzania.

Pole pole yupo sahihi kabisa.
 
Kuna maswali hapa nimeulizwa ambayo yametokana na alichosema Polepole:

1. Tupo kwenye zama za kidigitali ,je kuna kosa vyama kulink taarifa za wapigakura wake na mfumo wa NIDA ili kurahisisha utambuzi ?

2. Utaratibu wa kupiga kura na kuhesabu ni kwa kutumia karatasi , je mifumo hiyo imesaidia vipi ushindi kwa CCM?

3. Je Kuna tatizo gani CCM kulink mfumo wake na wa NIDA ikiwa hata taasisi nyingine zinafanya hivyo? Je, tatizo ni kwa CCM?

Akamaliza kwa kusema Polepole kwa sasa hajui asemalo ,amepuuzwa kabisa
CHAWA. Umelipwa TSH. 7,000/= kuja kuandika haya!
 
Yaani jamaa anawatazamaje watz?
YAANI
WAKATI MWINGINE TUNATAFUTA PA KUROPOKEA .
 
Back
Top Bottom