Polepole: Kuna mtu alikuja kuniambia kuwa kiongozi wa awamu ya 5 atakufa

Kumeanza kupambazuka, soon kila kitu kitakuwa wazi
 
At
Atuambie TAL alishughulikiwa na nani???
 
Ni maamuzi yake
Ni maamuzi yake lakini yanaonesha contradiction kwamba yeye anataka power hataki kuweka ukweli wazi.

Angetaka kuweka ukweli wazi angeuweka wote.

Ukimsikia mwanasiasa anasema ana mambo mengi na wakimuandama atasema mengine zaidi, ujue huyo nia yake si kusema ukweli nia yake ni mashindano ya kisiasa kupigania wafuasi na madaraka.

Mtu mwenye nia ya kusema kweli atakwambia ukweli wote mara moja tu.
 
Polepole ni mwanasiasa mwenye mikakati (political strategist). Unachokitaka hutokipata kwa haraka, hivyo tulia upokee dozi hatua kwa hatua. Hata dawa hutolewa kwa ratiba maalum, huwezi kunywa dozi yote kwa wakati mmoja.
 
Polepole ni mwanasiasa mwenye mkakati?

Anataka Samia asiwe rais.

Niambie mkakati wake wa kuhakikisha Samia asiwe rais ni upi?

Kamwambia Samia asichukue fomu za kugombea urais.

Samia akichukua fomu, Polepole atafanya nini? Strategy yake ni nini?
 
Ulimsikiliza Polepole kweli? Sasa unataka aweke mikakati yake hadharani!? Hahaha, huwezi kuwa serious kabisa.
 
Pengeni ndiyo atatoa bomu alilonalo vile pengine nae alihusika kwenye kifo cha mzee kwahiyo ataweka ukweli wote wazi sasa sijui itakuwaje
 
Ukweli unajulikana ila hauko wazi, kuna mtu anataka kuuweka wazi, watu hasira zimepanda, matumbo yanauma, presha juu, umaarufu chini, ni kuruka na kukanyagana, wanyonge tumekaa pembeni kushuhudia mtanange, kisasi cha Mungu kinakuwaga polepole Ila kwa uhakika. No retreat no surrender!!!
 
Ulimsikiliza Polepole kweli? Sasa unataka aweke mikakati yake hadharani!? Hahaha, huwezi kuwa serious kabisa.
Kwa hivyo unaamini Polepole ni stategist, lakini hizo strategy huzijui?

Unaamini katika mikakati ambayo huijui na haiko hadharani?

Sasa kama Polepole anakudanganya tu ana bluff hana mpango wowote wa maana wa kumzuia Samia utajuaje?
 
Ukitaka kumuelewa Polepole jitahidi sana kuyasikiliza asiyoyaongea ,hapo utafanikiwa kumuelewa kwa sura yakutisha sana .
Hata hayo tunayofanikiwa kuyaelewa ni vile tu tunaakili ila jamaa anatumia code mnoo.

Jamaa anakitu tena kizito na siyo wakugusika hovyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…