Huu ni mchakato wa wanasiasa na sio watanzania. Sijasikia jambo litakalomsaidia mtanzania bali mawazo ya wanasiasa kutafuta namna bora ya kuendelea kula keki ya Taifa.
wanasiasa ndio wameipigania katiba, hao wananchi wanaosubiri kusemewa tu ni wananchi wa aina gani? Maana nijuavyo hakuna mwananchi amezuiwa kudai katiba.
 
Uzuri wanafahamu fika! Siku wakikubali tu uwepo wa Katiba Mpya, na yenye tija, basi na siku zao za kukaa madarakani; zitafikia tamati.
Ata me mwanzo nilikua nawaza kitu kama icho ila nimegundua kwa jinsi Tz ilivyo na wajinga wengi ccm bado inayo miaka mingii mnooo yakutawala watz
 
Mama ana uchu sana wa madaraka, lazima atakwamisha mchakato mpaka baada ya uchaguzi mkuu ujao, tusubiri tuone
 
Na nyie watu wa siasa mjichambue, ni kazi ya jaji mtungi na watu wake. Nakubailiana na hoja ya 40% ya wanawake kwenye vyama vya siasa.
Hili kalitoa wapi, sikuliona likitajwa kuwa pendekezo. Kwani wanawake hawawezi kuwa asilimia sitini?

Ni wazi kwamba Samia hayupo tayari kutekeleza mapendekezo, maana tayari ameanza danadana isiyokuwa na mwisho.
 
Kuona uwepo wa msajili wa vyama na Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam kwenye picha ya pamoja nimedharau kila kitu hapo. Hao viumbe ni kichefuchefu sana
 
Namuona mchungaji wangu George Fupe
 
  1. Tume ya taifa ya Uchaguzi isilazimike kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote, idara yoyote ya serikali, chama chochote cha siasa, taasisi au asasi yoyote na utendaji wake uruhusiwe kuhojiwa kwenye mahakama ya juu ili kuongeza uwajibikaji wa tume.
kwenye hii no.4

hapo kwenye no. 4 hili ni gumu kutekelezeka na na hii ndio ROHO YA CCM ukiilazimisha CCM hili litekelezwe utaona jinsi hali ya hewa itakavyoanza kuchafuka maana inaeleweka na ipo wazi kabisa hata Pascal Mayalla analijia hili kuwa ccm haina uthubutu wa kukubali hili suala litekelezwe. tume ya taifa hapa haihusiki ila anaehusika katika hili ni mhusika ambae ni mtu binafsi mteule wa Mteuaji. mteule huyu iangaliwe je anapatikanaje mpaka kufikia kuwa ndie kiongozi wa tume na anatokea wapi. hivyo ukijua hili hapa huyu kiongozi wa tume otomatiki 😜 anajua kabisa ameteuliwa na bosi wake yaan mkuu wa kaya hivyo yeye kama yeye hapa ni lazima kwanza alinde ugali wake na pili maslahi ya aliemteuwa. tatu CHAMA.
hii kamati kama haikuangalia hili kwa umakini na kama bado uteuzi wa kiongozi wa tume ataendelea kuteuliwa na mwenyekiti wa chama tawala hili bado litakuwa ni tatizo na ndio ccm wanaposhikilia hapa pasibadilike ili waendelee kum'bana huyu mtumishi mkuu wa tume. hivyo tume kama tume haiwezi kufanya lolote na mkuu wa tume ataendelea kumtumikia aliemteuwa.
 
Hkn kitu hapa
 
Uzuri wanafahamu fika! Siku wakikubali tu uwepo wa Katiba Mpya, na yenye tija, basi na siku zao za kukaa madarakani; zitafikia tamati.
Sijui mkuu 'Tate Mkuu'!

Una maana na waTanzania hawa waliopumbazwa na CCM watageuka mara moja na kuwa na uelewa wa kukutia matumaini hayo uliyonayo?

Kunatakiwa kuwepo na 'brush' maalum ya kusafisha akili za waTanzania zilizochafuliwa na CCM kabla ya kufanya hayo unayoyategemea.

Haijulikani nani ataleta hilo li 'brush' ikibidi pamoja na JIK kali kuifanya kazi hiyo.

Kwa hali iliyopo sasa, nina mashaka makubwa sana juu ya waTanzania kuhusu msimamo huo unaouwaza wewe.
 
Rasimu ya Warioba siyo yote yaliyomo ni kupitisha lazima iangaliwe upya kutokana na muda. Tatizo siyo rasimu ya warioba jambo kubwa ni serikali ya shirikisho, hapa ndipo kwenye utata.
 
Very WEAK statement....

Unapendekezaje kuwepo kitu ambacho tayari kisheria?!

Kikosi Kazi "Kinapendekeza Kuruhusiwa" au Kikosi Kazi "KINATAKA MIKUTANO ya hadhara iendelee" pasipo na masharti yoyote?
Ndiyo maana na Samia mwenyewe kawaambia hapo hapo kwamba mapendekezo yaliyowasilishwa siyo amri kwa serikali
Serikali itachambua na kurekebisha ionavyo yanayowafaa wao, na siyo lazima yanayoifaa nchi.

Sioni jinsi CCM itakavyokubali mapendekezo yanayoiondolea uhakika wa wao kuendelea kuwa madarakani bila ya kulazimishwa kwa nguvu.

Wataendelea kutafuta njia za kuchelewesha, kupindisha wakati wakiendelea kuwa madarakani.
 
wanasiasa ndio wameipigania katiba, hao wananchi wanaosubiri kusemewa tu ni wananchi wa aina gani? Maana nijuavyo hakuna mwananchi amezuiwa kudai katiba.
Sawa, ni vyema na waendelee kuipigania peke yao..!
 
Mimi ningefurahi Kama angeanza mchakato kwa kuruhusu rasimu ya warioba ipite.
Mkuu HIYO ILIKUWA YA WANAHARAKATI-Warioba na wenzake walijinasabu kusikiliza watu na makundi yote. Sawa ila wakaishia kutoweka haki za wanaume
 
Nadhani kuna haja ya kuliangalia upya swala la idadi ya vyama vya siasa. Hakuna sababu ya kuwa na utitiri wa vyama na kusababisha watu kuto kufanya kazi za uzalishaji kwa ajil ya uchumi na kugawa ruzuku nyingi bila sababu. Tume ingeperndekeza vyama 3 tu tosha kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…