Profesa Assad: Hakuna bandari inayouzwa, ni uelewa mdogo wa watu

Profesa Assad: Hakuna bandari inayouzwa, ni uelewa mdogo wa watu

Ni kweli kabisa hakuna palipoandikwa inauzwa lakini pia hakuna palipoandikwa inakodishwa wala kupangishwa hivyo basi.

Kama haiuzwi
Kama haikodishwi
Kama haipangishwi

Maana yake ni moja tu inatolewa bure...

Zaidi Assad naye anataka kugeuka mchumia tumbo.

Maana yeye anazungumzia bandari moja tu wakati IGA inasema bandari zote Tanzania na miundombinu yake.

Mwambie kachelewa kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe huna ujualo zaidi ya kuwashikia akili wale wote unawaongopea humu kuhusu mambo yakufikirika ya uchawi na ushirikina,haya mambo waachie wenye akili zao,nenda kwenye thd zako zakichawi watakufuata huko watu wako wanaokuabudu kwa huo ujinga ujinga.
 
Inaelekea huelewi msingi wa wananchi kusema Bandari inauzwa!!
Ccm na Samia wamehongwa fedha nyingi na DpWorld ili kutekeleza huo mkataba wa kifisadi na huko ndio kuuza bandari zetu. Najua utabisha kwa hulka yako!
Sasa mbona unasema hayo nyuma ya keyboard? Kama unaelewa mtu kahongwa, mahakama huzijuwi? Wanasheria wenzako huwajuwi?
 
Wewe unaandika kijuha, kama kawaida ya ujinga wako. Ulitaka mkataba wa maendeleo uandike mambo ya upangishaji?

Kondoo hata ukiwa kwenye kundi la mbuzi unajulikana tu.
Mkataba wowote baina ya consenting parties lazima uwe very clear leaving no room for doubt!
Lazima utamke wazi kama ni mkataba wa mauziano, kukodishana au kupangishana!
 
,(1)Unategemea Asad awe kinyume na mkataba wa DP WORLD kivipi, Wakati yeye ni Mzanzibari.

Kwenye huu mkataba hakuna bandari ya Zanzibar hata moja inayobinafsishwa.Ina maana Zanzibar wao hawataki jambo hili kama lina faida?

Lingekuwa na faida lazima wangeshalalamika kwamba kwa nini tuwatenge kwenye huu ubinafsishaji Wakati ZNZIBAR ni sehemu ya Tanzania.

(2) Wananchi wanapolalama kwamba Bandari IMEUZWA,hawana maana kwamba tumewauzia DP WORLD kama vile tunavyouza shamba.HAPANA ! maana yake ni kwamba kwenye huu mkataba kuna vipengele ambavyo Tanzania inakuwa imelaliwa sana na hivyo vipengele hivyo vinatubana mno wakati sisi ndio wenye Mali hivyo virekebishwe.

UKIFUATILIA HAYA MALUMBANO, HAKUNA MWANANCHI HATA MMOJA ANAYEPINGA UBINAFSISHAJI ila wanataka ubinafsishaji WENYE FAIDA, na hata hawa viongozi wetu wanotoa ufafanuzi kwa wananchi wanalijua hili,ila kwa makusudi, either na wao wanatoa ufafanuzi wa kuuzwa au kutokuuzwa kwa Bandari na kuukwepa unwell unaoulizwa wa kurekebisha vipengele vibovu vya kwenye mkataba.

Wafafanuzi wanatoa elimu kwa uoga na unafiki kuelezea kitu ambacho hata nafsi na roho zao binafsi kwa ndani zinawakatalia, Ili kuwaridhisha baadhi ya viongozi wa juu wenye nia OVU waliowatuma na wana maslahi machafu katika vipengele vya kwenye mkataba vilivyokosewa kwa makusudi.

Ushauri wangu ni kwamba, vipengele vibovu virekebishwe,kuwe na uwazi,na Ubinafsishaji uendelee na tuachane kabisa na UBINAFSI WA BAADHI YA HAO WAKUBWA..wanaoendeleza mabishano badala ya kurekebisha hivyo vipengele vibovu,na mkataba uwe bora kwa pande zone mbili ,ili tuendelee na maisha mengine,Badala ya kuendelea kupoteza fedha, muda nk kwa kuandaa mikutano na makongamano yasiyoisha kwa ajili ya ufafanuzi unaozidisha malumbano.
Sikubaliani na maoni ya Prof. Asad, lakini siyo Mzanzibari. Ni mtu wa Tanga.
 
Kaongea vizuri na credibility yake ni nzuri huyo Shivji alisema nini kuhusu ubinafsishaji wa mabenki na muda ukamuumbua kama sio mtaalamu wa uchumi na uwekezaji akae pembeni.

Unachoongea hapa ni pumba kama za Musa Assad
 
Huyu naye ni mdini balaa
Sasa mbona Shivji katoa maelezo yake hatujayaafiki na hatukumsema kama mdini hatumsemi na uislamu wake wa dhehebu la khoja ila kwa Assad ndio udini kwa kuwa kasema tofauti na mawazo yako kama ingekuwa ajenda ya udini basi Shivji naye si angeunga mkono maana wote dini moja ila ni utofauti wa fikra ambao unakubalika tu ndio maana mchele mmoja unakuwa na mapishi mengi hembu tulizeni hadaa.
 
Sasa mbona Shivji katoa maelezo yake hatujayaafiki na hatukumsema kama mdini hatumsemi na uislamu wake wa dhehebu lq khoja ila kwa Assad ndio udini kwa kuwa kasema tofauti na mawazo yako kama ingekuwa ajenda ya udini basi Shivji naye si angeunga mkono maana wote dini moja ila ni utofauti wa fikra ambao unakubalika tu ndio maana mchele mmoja unakuwa na mapishi mengi hembu tulizeni hadaa.
Shivji ni mwanasheria, Assad ni mhasibu, yupi ambaye anaweza kusoma na akaelewa mkataba?
 
Back
Top Bottom