,(1)Unategemea Asad awe kinyume na mkataba wa DP WORLD kivipi, Wakati yeye ni Mzanzibari.
Kwenye huu mkataba hakuna bandari ya Zanzibar hata moja inayobinafsishwa.Ina maana Zanzibar wao hawataki jambo hili kama lina faida?
Lingekuwa na faida lazima wangeshalalamika kwamba kwa nini tuwatenge kwenye huu ubinafsishaji Wakati ZNZIBAR ni sehemu ya Tanzania.
(2) Wananchi wanapolalama kwamba Bandari IMEUZWA,hawana maana kwamba tumewauzia DP WORLD kama vile tunavyouza shamba.HAPANA ! maana yake ni kwamba kwenye huu mkataba kuna vipengele ambavyo Tanzania inakuwa imelaliwa sana na hivyo vipengele hivyo vinatubana mno wakati sisi ndio wenye Mali hivyo virekebishwe.
UKIFUATILIA HAYA MALUMBANO, HAKUNA MWANANCHI HATA MMOJA ANAYEPINGA UBINAFSISHAJI ila wanataka ubinafsishaji WENYE FAIDA, na hata hawa viongozi wetu wanotoa ufafanuzi kwa wananchi wanalijua hili,ila kwa makusudi, either na wao wanatoa ufafanuzi wa kuuzwa au kutokuuzwa kwa Bandari na kuukwepa unwell unaoulizwa wa kurekebisha vipengele vibovu vya kwenye mkataba.
Wafafanuzi wanatoa elimu kwa uoga na unafiki kuelezea kitu ambacho hata nafsi na roho zao binafsi kwa ndani zinawakatalia, Ili kuwaridhisha baadhi ya viongozi wa juu wenye nia OVU waliowatuma na wana maslahi machafu katika vipengele vya kwenye mkataba vilivyokosewa kwa makusudi.
Ushauri wangu ni kwamba, vipengele vibovu virekebishwe,kuwe na uwazi,na Ubinafsishaji uendelee na tuachane kabisa na UBINAFSI WA BAADHI YA HAO WAKUBWA..wanaoendeleza mabishano badala ya kurekebisha hivyo vipengele vibovu,na mkataba uwe bora kwa pande zone mbili ,ili tuendelee na maisha mengine,Badala ya kuendelea kupoteza fedha, muda nk kwa kuandaa mikutano na makongamano yasiyoisha kwa ajili ya ufafanuzi unaozidisha malumbano.