Profesa Assad: Hakuna bandari inayouzwa, ni uelewa mdogo wa watu

Kwanza prof kaamua kutoa mawazo yake. Sasa asiseme tuna uelewa mdogo. Amesema hivyo vitu vitatu, mtaji, watu na mfumo.

Inashindikana nini kuleta watu wenye huo mfumo tukaumiliki wakatrain watu wetu wakafanya?

Mtaji sio shida maana biashara ya bandari inalipa kwa nini tusikopesheke? Mbona zipo kampuni za ndani zikipewa zinamudu? Kwani share zikiuzwa hatutanunua?

Kukataa jambo haimaanishi uelewa ni mdogo.
 
Ona sasa unabishana na aliyekuwa mdhibiti na mkaguzi wa mahesabu ya serikali yaani mashirika yote anajua kwa undani hali ya fedha ya serikali kuliko hata wewe ila sasa unambishia 😂
Akishasema Shivji, Mh. Warioba na kidogo Butiku hiyo itakuwa imekwisha. Yaani kwenye issue za Sheria nimsikilize Prof. Assard badala ya Prof. Shivji? Huo utakuwa uzuzu usio kiwango.
 
Naomba kujua qualifications zako za elimu, coz unaonekana umemzid hata huyo professor [emoji23]
 
Hapa ndugu yangu Profesa Asad ametoka kapa.
 
Profesa Assad husimama kwenye ukweli sio mtu wa kuyumbishwa. Shivji na wenzake hawajawahi kuiunga mkono serikali yoyote ya CCM. Kinachonisikitisha ni nyumbu kuanza kumrushia maneno ya hovyo Profesa Assad.
 
,(1)Unategemea Asad awe kinyume na mkataba wa DP WORLD kivipi, Wakati yeye ni Mzanzibari.

Kwenye huu mkataba hakuna bandari ya Zanzibar hata moja inayobinafsishwa.Ina maana Zanzibar wao hawataki jambo hili kama lina faida?

Lingekuwa na faida lazima wangeshalalamika kwamba kwa nini tuwatenge kwenye huu ubinafsishaji Wakati ZNZIBAR ni sehemu ya Tanzania.

(2) Wananchi wanapolalama kwamba Bandari IMEUZWA,hawana maana kwamba tumewauzia DP WORLD kama vile tunavyouza shamba.HAPANA ! maana yake ni kwamba kwenye huu mkataba kuna vipengele ambavyo Tanzania inakuwa imelaliwa sana na hivyo vipengele hivyo vinatubana mno wakati sisi ndio wenye Mali hivyo virekebishwe.

UKIFUATILIA HAYA MALUMBANO, HAKUNA MWANANCHI HATA MMOJA ANAYEPINGA UBINAFSISHAJI ila wanataka ubinafsishaji WENYE FAIDA, na hata hawa viongozi wetu wanotoa ufafanuzi kwa wananchi wanalijua hili,ila kwa makusudi, either na wao wanatoa ufafanuzi wa kuuzwa au kutokuuzwa kwa Bandari na kuukwepa unwell unaoulizwa wa kurekebisha vipengele vibovu vya kwenye mkataba.

Wafafanuzi wanatoa elimu kwa uoga na unafiki kuelezea kitu ambacho hata nafsi na roho zao binafsi kwa ndani zinawakatalia, Ili kuwaridhisha baadhi ya viongozi wa juu wenye nia OVU waliowatuma na wana maslahi machafu katika vipengele vya kwenye mkataba vilivyokosewa kwa makusudi.

Ushauri wangu ni kwamba, vipengele vibovu virekebishwe,kuwe na uwazi,na Ubinafsishaji uendelee na tuachane kabisa na UBINAFSI WA BAADHI YA HAO WAKUBWA..wanaoendeleza mabishano badala ya kurekebisha hivyo vipengele vibovu,na mkataba uwe bora kwa pande zone mbili ,ili tuendelee na maisha mengine,Badala ya kuendelea kupoteza fedha, muda nk kwa kuandaa mikutano na makongamano yasiyoisha kwa ajili ya ufafanuzi unaozidisha malumbano.
 
hivi profesa kama huyu unaweza kumweka meza moja na shivji? huhu ni kama hajasoma vile. just a good zanzibaris.
 
Asad mzanzibar ashukuru tu Mungu Tanganyika ilimwajiri na amepata ugali tokea Tanganyika, la sivyo angekuwa mvuvi kule nungwi.
 

Usishangae akisema kwa sasa Bunge sio dhaifu.
 
Bora umesema wewe. Ningesema mimi nimgeambiwa chawa
 
Sio appropriate authority so atulie.

Sisi kugezo 1. Iwe mwanasheria
2. Leta hoja kulingana na andiko lenyewe na si kubuni mambo yako.
 
Ndio kwaheri ya mama?!
Inazidi kudhihirisha labda viatu kweli vilikuwa vikubwa mno...
Hata wam promote kivipi hawezi, hata waanze campaign mapema haisaidii...
LAZIMA KURA ZIIBIWE TU MAMA AENDELEE...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…