TANZIA Profesa Honest Ngowi afariki dunia kwenye ajali Mlandizi Pwani. Alikuwa mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe

TANZIA Profesa Honest Ngowi afariki dunia kwenye ajali Mlandizi Pwani. Alikuwa mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe

Kifupi njia ya Dar, Morogoro au Dar chalinze ilipaswa kuongezwa walau njia zisizopungua mbili hadi tatu.
Tukipata hata dual carriageways za 2 by 2 inatosha , tatizo lipo Tanroad , hawajifunzi
 
Nimesikia hii taarifa nikatamani lisiwe ni jina hilo....lakini wapi.

Pumziko La Amani Apate.
 
Nimeumia sana prof hukunifundisha darasani but mafundisho kupitia chambuzi mbalimbali ni zaidi ya darasani RIP Prof. Honest Ngowi.
 
Mmefukuza madereva wazuri kwa sababu za kipuuzi za vyeti fake mara sijui dereva naye awe form four wakati mbunge ni darasa la saba, pumbavu kabisa.

Qualification ya driver ni driving license na siyo hawa waliokosa ajira kwenye soko la ajira na kukimbilia udereva, kuendesha Passo yako ni tofauti kabisa na professional driving.

Ukiwa unasafiri jihadhari sana na hizi plate namba za STL, DFP na SU, hakuna madereva humo siku hizi ndio mitambo ya kupeleka watu kuzimu.
Makasiriko yote haya ya nini??
 
Requiescat in pace Prof. Ngowi.
Eternal rest, grant unto his soul, O Lord, and let your perpetual light shine upon him. May he rest in peace. Amen.
 
Jamani jamani. Watu wa maana wanaondoka. Tunabakiwa na .....

R.I.P Prof Honest Ngowi
We ulitaka aondoke nani ambaye si wa muhimu? Binadamu wote ni wa muhimu ila tumegawana tu majukumu. Hata bodaboda,mamantilie wote ni muhimu. Prof.kamaliza kipande chake alichopangiwa Mungu amuweka mahali anapostahili.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Anaongelea defensive driving , ambayo haswa ni package mahsusi unapoendesha executives.
Unaweza kuona tu ni lori limeangukia hiyo land cruiser , lakini dereva mahiri hawezi kuingia kwenye akward situations kirahisi.
Speeding inahusika pia
 
namjua tu kwakua nishawai muona ITV kwenye masuala ya kiuchumi
RIP boy
 
Kuna watu wenye taaluma kubwa kama hizi,wakiwa hai,hatupati habari zao,sisi wananchi wa kawaida.Tungeomba hapa JF,kuwe na platform,ya kutufahamisha ,Watu muhimu kama hawa,wako wapi,na tutawapata vipi,ili kutupa ushauri wa kuchanganyua changamoto tulizo nazo.
 
Pole kwa familia, jumuiya ya Mzumbe, vyombo vya habari alivyokuwa anashirikiana navyo na watanzania waliokuwa wanamfuatilia kupitia vyombo vya habari. Maisha ya Prof Ngowi yameisha kwa ghafla sana, kama kwa kukatizwa hivi,kweli Mungu una siri kubwa. tunafajikika kuwa kazi zake zitaendelea kuishi
 
Duh,kumbe ndo ajali hiyo ,kuanzia madafu mpaka mlandizi kulikua na bonge la folebi,tukachepukia old morogoro road,.Apumzike mahala pema
Hafi mwanaadamu mpaka ajali yake ifike. Haya mambo si ya bahati mbaya. Yalipangwa hivi toka Honest Prosper Ngowi yumo tumboni mwa mama yake. Tumshukuru Mungu Mwenyezi na kuwaombea dua maiti.
 
Prof Ngowi. Umeondoka kimasihara. Tumefanya KAZI nyingi pamoja. Sijawahi kuona binadamu msomi aliyeweza kutumia vipawa vyake Kwa umma Kwa upendo na weledi kama wewe. Msomi uliyejikita kwenye Elimu Kwa vitendo.

Mchapakazi Kitaaluma na binafsi. Uliiongoza Mzumbe Dar Campus kwa weledi mkubwa mno, humbled leader down to Earth. Tanzania tumempoteza MTU ambaye alikuwa tajiri wa Moyo na umefikia wengi mno.

My brother nitakukumbuka kwa mengi personal na kikazi tulipoweza kufanya KAZI nyingi pamoja na tumeishia kuwa marafiki. Ninaumia mno moyoni. Akili imetulia kwa muda natafakari sipati majibu.
 
Back
Top Bottom