Rais anapofia madarakani, utaratibu ni upi kwa sheria za nchi yetu?

Rais anapofia madarakani, utaratibu ni upi kwa sheria za nchi yetu?

Rais - Makamu wa rais - Waziri Mkuu - Jaji mkuu - uchaguzi wa dharula.
 
Akifariki chama chake kitaendelea kuongoza hadi ifike miaka kumi au yule mgombea mwenza ataongoza nchi je wakifariki waote kwa pamoja ,pengine wanasafiri kwenye ndege moja,unajua mabadiliko tabia nchi siku hizi hayatabiriki ,na ni vyema wananchi wakaelewa katiba yao inasemaje

Mwiba,

Badilisha heading ya Thread yako.
Siyo sahihi kusema, ''RafikiAfariki''! Mtu anapoona heading hiyo anapata mshtuko kuwa kuna Raid amefariki dunia!! Ulitakiwa uandike.''RAISI AKIFARIKI"

Hata hivyo swali lako linajibiwa na Katiba ya JMT. Unachotakiwa ni kuitafuta, kuisoma na kuielewa KATIBA ya nchi yako. Tatizo la Watz wengi ni wavivu wa kusoma.
 
Rais akifariki Makamu wake anakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano.
Hii katiba ya 1977 kweli haitufai. Ingebidi makamu wa rais akabidhiwe mamlaka ya rais kwa kipindi cha siku 90 huku nchi inajiandaa kufanya uchaguzi, badala ya kumuachia makamu atawale.
 
Sio Kufariki tu hata akiwa Nje ya Nchi Makamu anakaimu nafasi yake, ila nadhani akifariki kwa Nchi kama yetu Makamu anakaimu Nafasi yake Mpaka uchaguzi utakapofanyika!
 
Back
Top Bottom