Rais anapofia madarakani, utaratibu ni upi kwa sheria za nchi yetu?

Rais anapofia madarakani, utaratibu ni upi kwa sheria za nchi yetu?

Nilipoiona hii post ndiyo ya kwanza nikadhan jamaa tayari. Nilkuwa nmepata kaftah ghfla
 
Katiba inasemaje kuhusu hili,wajuzi naomba kujua iwapo Rais atafariki kabla ya kumaliza muda,nini kinafuata!!!
Kiutaratibu mkuu wa majeshi hushikilia kitu kwa muda hadi tume ya uchaguzi itakapoamua au mpaka miaka ambayo ilikuwa ndio mwisho wake kura zipigwe tena..
 
Eeeeh mjomba mjomba

Utasukumwa ndani ....kwa swali hili
Salalee!
 
Kwa kadiri ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) ; Rais anapofariki, basi makamu wake ataapishwa kuwa Rais.

Makamu anapoapishwa kuwa Rais, atashauriana na chama chake na kisha atamteua mtu mmoja ndani ya chama kuwa makamu wa Rais, ambaye atapaswa kuthibitishwa na bunge.
 
Kiutaratibu mkuu wa majeshi hushikilia kitu kwa muda hadi tume ya uchaguzi itakapoamua au mpaka miaka ambayo ilikuwa ndo mwisho wake kura zipigwe tena..
Majibu napata tofauti, wengine wanasema PM ndio anashika nchi! Unaweza kutuwekea kifungu cha katiba
 
Kwa kadiri ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) ; Rais anapofariki, basi makamu wake ataapishwa kuwa Rais.

Makamu anapoapishwa kuwa Rais, atashauriana na chama chake na kisha atamteua mtu mmoja ndani ya chama kuwa makamu wa Rais, ambaye atapaswa kuthibitishwa na bunge.
Asante, nahisi uko sahihi japo sijapata kifungu husika
 
Ki protokal wewe ndo kuna kitu umefikiria hapo
Mkuu mimi nafikiria yeye atakuwa kapatwa na maswahiba gani mpaka kufikilia hivyo ila siku zote mtu hupenda, anayemchukia apotee ili akae kwa amani.
 
Asante,nahisi uko sahihi japo sijapata kifungu husika
Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 37 (5); inasomwa pamoja na ibara ya 40.

Ambapo, Rais mteule (makamu wa Rais) kama atashika nafasi ya Urais kwa muda wa chini ya miaka mitatu ataruhusiwa kugombea kwa awamu mbili zingine.

Ambapo, Rais mteule (makamu wa Rais) kama atashika nafasi ya Urais kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu, ataruhusiwa kugombea tena kwa awamu moja tu.
 
Back
Top Bottom