Dini na siasa ni Chanda na Pete. Tena zamani viongozi Wa kisiasa ndio walikua viongozi wa Dini. Mabadiliko yalikua kutokea hasa Ukisoma Agano la kale pale wana wa Israeli walipotaka Mfalme wao pekee asijiungamanishe na mambo yote mawili ndipo hapo utawala unaanza rasmi kwa Sauli.

Lakini kabla huko nyuma Musa alikua kiongozi wao wa Dini na kisiasa, Yoshua, etc. na hii ikawa hivyo hivyo kwa Dola za Rumi, Babeli, e.t.c

Na hata leo hii tawala zote za Dunia siko chini ya tawala za kiimani. Kama sio nguvu za Giza basi ni Mamlaka ya Mungu. Huwezi tenganisha Haya mambo Neverr…

Mimi nasema hivi, Imani ina nafasi kubwa sana kwenye tawala hizi tulizonazo
 
Waende wakafanye kazi za kuchunga kondoo za bwana wasituletee firimbi hapa.. kwani sadaka na misa zimeisha ? au kondoo wao wamekosa nyasi? wadini wakubwa
Umesoma mkataba wenyewe? Watanzania tuache uvivu wa kutopenda kusoma - soma kila sentensi hapo utajua mbivu na mbichi.
 
Huyu mzee angejua anavyotafsiliwa na watanzania ilitakiwa akae kimya!!
 
Kiongozi wa kisiasa amealikwa kwenye shughuli ya kidini (mchanganyiko maalumu)... Alafu anawaasa wenye dini wasichanganye siasa na dini!
Hivi watu wanashindwa kuelewa kuwa dini na siasa vyote vinawahusu watu! Na kadri unavyojitahidi usivichanganye ndivyo vinachanganyika!??
Kule Makumira Arusha nimeona bango Rais SSH aalikwa kwenye shughuli ya kidini!

ccm iache mind games kwenye masuala ya kitaifa!
 
Hio hatari naitamani sana ili tugawane mbao vizuri
 
safi sana Mzee hapo umeongea.

ifikie kipindi wachague Dini au Siasa hatuwaelewi kenge hawa maana hata Yesu aliwambia ya Mungu mpeni Mungu na ya Kaisali mpeni Kaisali.
 
Uislamu hauruhusu udikteta, rejea zake ni Qur'an na Sunnah.
Bandiko lako limejaa hasira, kisasi, chuki, husuda, roho mbaya, uzandiki n.k. Hivi vitu humfanya awe na ukuta katika kuliendea jambo na pia kufanya maamuzi sahihi.

Naomba nikuulize maswali yafuatayo:

1) Unahisi ni kwa nini mtume hakumuandaa mrithi wake?


2) Mazishi ya mtume yalichelewa, unahisi sababu ni nini?


3) Makhalifa wakuu wengi waliuawa kwa upanga, umeshawahi kujiuliza ni kwa sababu gani?


4) Kuna msemo unasema kuwa "Uislamu ulienea kwa ncha ya upanga", unaelewa maana yake nini?


5) Unafahamu ni sababu zipi zilizopelekea mgawanyiko wa kmadhahebu?
 


Watu wasijichanganye Kanisa katoliki kongelea swala la bandari wako sawa na sisi wakatoliki tunaunga mkono. Kikwete ni mwislaamu na wengine ni wasatabato hawajalazimishwa kuongelea. Kanisa katoliki linaongelea jamii pale ambako wanaona shida. Hata Papa anaongelea kila jumapili mambo mengi kama wakimbili, kutoa mimba, adhabu ya kifo, ubaguzi haya yote sehemu nyingine ni siasa!
 
Mb Mbona yeye kachanganya dini na siasa hapo tayali
Hiyo ni shughuli ya kidini yeye kaongea mambo ya kisiasa🤣🤣🤣
 
Ukiona hadi Rais uvumilivu ulimshinda akaamua kusema wazi kwamba!

"Baadhi ya wazee wastaafu waache viherehere vinaligharimu taifa!"

sasa ndiyo namuelewa!
Hakuna udini unaochanganywa! Viongozi wa dini wanatambua ugumu wa kuliombea taifa ambalo linaingia mikataba mibovu!

Tuwapunguzie mizigo ya kufanya maombi kwa taifa na viongozi wanaoliingiza taifa kwenye matatizo ya kiuchumi kutokana na mikataba mibovu.

Maonyo ya viongozi ni kama Aalama za barabarani zikipuuzwa ndiyo huwekwa matuta! Waraka ni matuta kwenye maamuzi ya viongozi!

lengo la matuta ili sote tubaki salama, lakini mpuuzi anaenufaika na speed anaweza kutoka hadharani kudai tusichanganye kilimo cha matuta na barabara!

wataoumia ni wananchi!

wastaafu wengine wanawashwa kweli kama Rais magufuli alivyosema
 
Kikwete kila akisimama lazima atolee mfano uongozi wake, kwamba kipindi chake alifanya bora kuliko wote, na inapaswa wengine wote wafanye kila kitu kwa marejeo ya uongozi wake.

Ukweli halisi kwa kipindi chetu hiki huyu mtu ni wa kumtahadhari sana, lugha rahisi ya kumuelezea ikitamkwa inakera, sio vizuri kumkera mtu au kutoa matamshi yanayokera ila yote ya yote ni mtu wa kuwa nae kwa tahadhari sana.
 
Hahahahaha. RIP JPM
 
Reasoning capacity ya Kikwete ni very low. Yaani haoni kasoro kenye mkataba wa bandari mpaka aanze kusema udini kwa vile anayekosolewa ni muislamu mwenzake!
 
Mkuu voicer hivi Mh Dr Jakaya Kikwete yupo upande upi kwenye hili jambo la Bandari?
Ninavyojua mimi huyu ndie Remote Controler wa hizi issue zote.
Yule tunaemlaumu naye yupo kama mateka fulani hivi.
Halafu watu hamuijui nguvu ya TEC!
Hao hao viongozi huwa hawakauki huko kwa maaskofu.
Ushauri wakati wanapokuwa kwenye njiapanda huwa wanakimbilia huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…