"Napenda kuchukua nafasi hii kukumbushana kuhusu tunu nyingine muhimu nayo ni kutokuchanganya dini na siasa. Tukiivunja tunu hii gharama yake tutaiona, na kama kuna viongozi wa dini wanataka kutuelekeza kuitumia dini kwa manufaa ya kisiasa, na kama kuna viongozi wa siasa wanataka kuitumia dini kwa manufa yao ya kisiasa, nawaombeni ndugu zangu tuwanyanyapae.
"Siku ikifika ambapo uwanachama wa chama cha siasa au uumini thabiti wa dini ukawianishwa na chama cha siasa kinachofuata ndio mwisho wa nchi yetu, mtakuwa na vyama vya siasa vya wakristu, waislamu, walokole nk. Kuwafanya Watanzania kuyatazama masuala ya kisiasa, kiserikali, utawala kwa mtazamo wa dini zetu ni jambo hatari, halkadhalika watu kuyatazama masuala ya dini kwa mtazamo wa siasa za vyama vyao si jambo lenye afya kwa taifa letu.
"Yote mawili yataathiri umoja na kutishia amani, usalama na utulivu tunaoufaidi hivi sasa. Mfano Zanzibar walifika mahali waisilamu wanamuona shehe ambaye ni mfuasi wa chama ambacho sio chake sio shehe sawa sawa, kwahiyo wakienda kusali kama shehe ni msuasi wa CUF wanangoja amalize kusalisha, halafu anaingia shehe wa waislamu na wafuasi wake.
"Nawaambia vitu halisi na ndio maana nilipokuwa Rais nilishughulika sana pale na kupata muafaka, niliahidi kwenye hotuba yangu ya kwanza ya Bunge 2005 Dec 30, kwamba nitafanya kila ninaloweza tujenge muafaka Zanzibar, haukuwa rahisi. Mkutano ule tuliufanyia Butiama NEC, ilikuwa moja ya kikao kigumu kwelikweli, lakini nikasema pamoja na ugumu wote lazima hapa tuvuke. Tukafika mahali nilipoona mambo yamekuwa makali, nikasema twendeni kwanza tukale, tulipokuwa tunakula ndio tukawa tunaweka mikakati ya namna gani tunalimaliza hili jambo. Tukajipanga nani ataanza kuzungumza, tukakubaliana kwamba tutakwenda Zanzibar kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na ndio imetusaidia Zanzibar tuna mazingira ya utulivu mpaka sasa, tungekwenda na utaratibu ule ule wa zamani tusingefika.
"…Tukianza kuchanganya dini na siasa tukageuza mimbari za dini na madhabahu kuwa sehemu ya kuhubiri kwishilia mbali nchi yetu. Lakini baba wa taifa ametuasa juu ya hatari ya kuchanganya dini na siasa. Nawasihi Watanzania wenzangu kuitunza tunu hii kama mboni ya jicho letu. Tukatae kuwasikiliza viongozi wa dini na waumini wao wanaofanya vitendo wa aina hii iwe kwa siri au kwa Dhahiri, vitendo hivi vinaweza kutupeleka kubaya."
Kikwete ameyasema hayo leo 20/8/2023 katika ufunguzi wa jengo Kanisa la Kiadventisti Wasabato Mara.
Mstaafu huyu ana 'moral authority' ipi kuanza kukemea viongzoi wa dini wanaotoa maoni kinzani dhidi ya uamuzi wa serikali kuhusu rasilimali za umma lakini anashindwa kukemea wanaosifia kila kitu kuhusu mkataba wa bandari wenye vifungu tata?
Maadamu yeye mwenyewe ametamka kwamba walipojitokeza kundi la wasabato masalia anajua namna alivyomalizana nao!!! Sasa swali ni kwamba aliwapeleka wapi hao waumini wa kanisa la wasabato malia 51 ambao aliamuru wapigwe picha na askari wa uwanja wa ndege tarehe 3 Septemba na tarehe 4 Septemba 2008?
"......KUNDI la waumini wa Dhehebu la Waadventista Wasabato Masalia, kwa mara
ya tatu limesambaratishwa na askari wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere, baada ya kurudi tena uwanjani hapo huku wakiwa
wameongezeka idadi yao kutoka 17 hadi kufikia
51.............
Baada ya kujibiwa hivyo, askari hao waliamua kuorodhesha majina ya
waumini hao na kuchukua jukumu la kuwapiga picha mmoja mmoja na
kuwaamuru watoweke katika viwanja hivyo.............
Waumini hao wakati wakiondoka kwa maandamano, walisindikizwa na kundi
la askari wa uwanja wa ndege, ambao walipofika barabara ya Nyerere,
askari hao walizuia magari kwa muda wa sekunde kadhaa ili kundi hilo la
waumini liweze kuvuka.........."
Kwa hiyo yeye ndio rais kwa sasa na anataka amalizane na TEC kwa mtindo upi?