Rais Mstaafu Jakaya Kikwete: Msijaribu Kuchanganya Dini na Siasa Hata Kidogo
Rais Mwinyi ni rais tofauti na watangulizi wake, rais Mwinyi yeye amejikita sana kuendeleza uisilamu kwani hivi sasa amekuja na ajenda ya " mwaka wa kiisilamu" kuuingiza kwenye kalenda, huko nyuma aliwahi kuja na serikali kuanzisha mfuko wa mahujaji.

Je, ushauri wa Kikwete kuhusu kuchanganya siasa na dini unawezekana wakati viongozi wa CCM ndio wachanganyaji wakubwa?
Nadhani inaruhusiwa kuchanganya siasa na dini lakini hairuhusiwi na ni marufuku kuchanganya dini na siasa! Upo hapo?!!
 
Jakaya Fundi sana wa Siasa

yeye hajamtaja mtu wala kikundi cha watu

katahadharisha tu tusichanganye Dini na Siasa

Wachanganyaji povu linawatoka

nayakumbuka sana maneno yake akiwa Mwenyekiti wa Ccm kupitia Katibu wake wa Uenezi Nape Nnauye

' Kazi yetu ya kisiasa sio kumtoa Nyoka kwny Mtungi …kazi yetu ni kuinamisha Mtungi na Nyoka atatoka mwenyeweee '

Mbona Wasabato Masalia au Washia hawajamaindi kuambiwa wasichanganye dini na Siasa? mbona sio mara ya kwanza Wanasiasa kusema hivyo? mbona safari hii kuna watu Povu linawatoka ?

kweli Hotuba za Jakaya huwa ni zaid ya Falsafa
Cha ajabu anatumia majukwaa ya dini kupinga kuchanganya dini na siasa,
 
Rais Mwinyi ni rais tofauti na watangulizi wake, rais Mwinyi yeye amejikita sana kuendeleza uisilamu kwani hivi sasa amekuja na ajenda ya " mwaka wa kiisilamu" kuuingiza kwenye kalenda, huko nyuma aliwahi kuja na serikali kuanzisha mfuko wa mahujaji.

Je, ushauri wa Kikwete kuhusu kuchanganya siasa na dini unawezekana wakati viongozi wa CCM ndio wachanganyaji wakubwa?
Tanganyika tumeipokea nchi kutoka kwa waingereza ambao wao dini yao kuu ni ukristo, hivyo wakristo wa nchi hii wamepata upendeleo wa kurithi kutoka kwa wakoloni waliyotutawala katika mambo mbalimbali, ndiyo maana hata siku za ibada za kikristo ni mapumziko ya mwisho wa juma, sikukuu nyingi za dini ya kikristo zimekuwa ni sikukuu za kitaifa na halikadhalika sikukuu za kislamu nazo zimekuwa ni za kitaifa pia baada ya uhuru kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wafuasi wa imani hiyo katika nchi.

Zanzibar ni nchi yenye idadi kubwa ya waislamu hivyo wao wakiamua kuwasikiliza watu wao (walipa kodi wao) katika mambo ya imani yao juu ya sikukuu zao hakuna ubaya. Tambua kuwa Zanzibar ni nchi yenye raisi wake na serikali yake wana maamuzi yao, ikiwa jambo halina tatizo kwenye mambo ya muungano wala tusihangaike. Zanzibar wakati wa Salmin Amour 1992 walipojiunga na OIC, kulizuka kelele nyingi kutoka bara. Mzee Kikwete kwa kuwa ameshawahi kuwa raisi wa nchi hii hivyo anajua nini anachokizungumza.
 
Rais Mwinyi ni rais tofauti na watangulizi wake, rais Mwinyi yeye amejikita sana kuendeleza uisilamu kwani hivi sasa amekuja na ajenda ya " mwaka wa kiisilamu" kuuingiza kwenye kalenda, huko nyuma aliwahi kuja na serikali kuanzisha mfuko wa mahujaji.

Je, ushauri wa Kikwete kuhusu kuchanganya siasa na dini unawezekana wakati viongozi wa CCM ndio wachanganyaji wakubwa?
Okay, imekaaje hii. Kwani kwa Sasa Mwaka wa Kiislaamu haupo kwenye kalenda?

Sasa mbona miaka yote tunatumia kalenda ya kikristo? Hii imekaaje?
Au hili liinchi ni la kikristo?

Nadhani na mapumziko ya wiki yawe pia siku ya alkhamisi na ijumaa ili mjue watu waliwavumilia sana,
Kila jambo lina mwanzo na mwisho na huu ndio mwanzo wa mwisho wa tabu zote
 
1692741302876.png

Wanangu wapendwa, naomba mnifundishe jambo. Hivi karibuni tumeona makundi mawili yakimgawana rais mama. Wakatoliki wamemuwasha bila woga. Walutheri wameamua kumvunga kujifanya wanamuunga mkono hasa kwa ukimya wao. Wakati wakimsifia Samia kwa ukimya kana kwamba kuna rais mwingine anayepaswa kutupa maelezo ya kina, rais Jakaya kikwete ameamua kuwaka dhidi ya wakatoliki. Je hapa tufanye nini kama wakubwa wetu wamechanganyikiwa kiasi hiki?

Je ni dhambi kwa maaskofu kuipinga serikali? Je Kikwete katumwa na Sami au kajituma? Kikwete anaonya tusichanganye dini na siasa wakati CCM ndiyo imeanzisha mchezo huu. Je Kikwete amepitiwa kusema au kutafuta kiki au hajui hata anachosema?

Kikwete anasifika kwa kuwa rais ambaye alikuwa fisadi na asiye na msimamo. Je leo Kikwete kaona mwanga au ndo vunga yenyewe? Je Walutheri walimsifia Samia ukimya kumsuta Kikwete au kumweka uchi? Unaweza kudurusu na kudadavua mengi ukiamua.

Hebu tufikiri na tujadili pamoja.
Naomba kuwasilisha.
 
Wakatoliki wamemuwasha bila woga. Walutheri wameamua kumvunga kujifanya wanamuunga mkono hasa kwa ukimya wao.
Walutheri wameona wakatoliki ndio wanafaidika na keki ya serikali kwahio wame waachia wenyewe goma lao.
 
Tusimshambulie Kikwete, alicho kinena ana maana kubwa japo amekosea timing. Na penyewe pengine ni sawa kwani angeongea kabla hata tusingelichukulia maanani.

Kauli yake inamlenga yeyote iwe kwa makusudi au bila kutarajia siasa kutumika kwenye dini ina matokeo ya aina nyingi.

Mheshimiwa Kikwete mwenyewe analijua hili lipo ama ndani ya CCM au nje. Hivyo ni jiwe kwa wanaojiita wafia vyama maana ndio wanaoratibu hii mipango namna ya kutumia propaganda za dini au ukanda ili waendelee kunufaika.

Watanzania tutumie akili kubwa tumbananishe afafanue zaidi alilenga nini kwenye hili. Vinginevyo hatutapata ya moyoni au udambwi dambi aliouona mzee wa Msoga.

Mimi naamini mh Kikwete ni veterani hivyo anayajua mengi kwa kufanya na kuyaona. Hivyo vyombo vyetu vya habari vimbane afafanue kauli yake hii.

Tusiwe wepesi wa kukonclude wakati kwanza ndio tupo kwenye intro.

Kikwete ana akili na anakijua alichosema maana na yeye amekitumia ila inawezekana alikuwa anakitumia ashinde mechi zake
 
Katika kitabu changu kipya kiitwacho 'Arm chair' nita explore juu ya 'utawala wa JK katika awamu ya sita'.
 
Back
Top Bottom