Ahsante Tundu Lissu!
Kuandaa kanuni za nini wakati sheria ipo na inajieleza vizuri?
Hicho kikao cha tarehe 15 -17 Dec 2021 Chadema hawakuwa na muwakilishi, mostly waliohudhuria walikuwa wale marafiki wa watawala.
Hapa sioni sababu ya kudanganyana, hizo kanuni Simbachawene anaandaa kwa malengo yapi? na wakina nani watakuwa waandaaji?
Nataka kuona mapendekezo watakayokuja nayo Chadema baada ya kukaa chamani yatafanyiwa kazi, vinginevyo hii serikali inaonekana bado haiko tayari kwa suluhu.
Kanuni za nini!!?? kwani KWA miaka HII 60 mikutano ya siasa haikuwa na kanuni!!??nini kiliharibika kwani!??waache ujinga Hawa jamaal!!
Inavoonekana mwendazake alizifuta kanuni kimya kimya,ndiyo maana haionekani kwenye katiba,vinginevyo Kama ameakiza kanuni zitungwe sasa,inavoonekana vyama vingi ndiyo vinaanzishwa sasa.Magufuri aliharibu Sana kwa hili
Kabisa bwashee!Tanzania tujifunze ya Ukraine
Hahahaaaa....... Unamaanisha Wagalatia?Hicho zamani hakikuwepo,Ila baada ya mihadhara ya waislam kuzidi,mkapa akakiweka,ilikua unatoa tu taarifa polisi ili waje kulinda...Kuna upande ulifurahia sana
Sasa kanuni si ndio zinakuja kupiga pin zaidi kuliko ambavyo hazikuwepo. Hivi sasa mikutano chama kinaweza kufanya kwa namna yoyote kitakavyo, sasa kanuni zinakuja ma kusema (mfano) mikutano itaanzia ukumbini tu, hakuna msafara wala maandamano.Hazikuwepo kanuni zinazoongoza ufanyaji mikutano zaidi ya sheria
Kanuni za kazi gani wakati Katiba ina maelekezo ?Waziri wa katiba na sheria ameagizwa atunge kanuni ambazo zitaratibu kufanya mikutano ya hadhara ya vyama. Vya siasa. Hivyo sasa ni ruksa.
Rais aagiza ziandaliwe kanuni zitakazoongoza mikutano ya siasa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo kwa Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene kuandaa kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.www.mwananchi.co.tz
Mbona utaratibu wa kufanya hayo upo!
Wengi wao ni wahanga wa kipindi cha giza, waliisha nogewa na uholela.Tunaongozwa na viongozi ama wasioijua katiba au ambao hawaiheshimu kabisa!
Kwani sheria ya vyama vya siasa inasemaje kuhusu haki na wajibu wa vyama vya siasa !#HABARI Rais @SuluhuSamia amemwagiza Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene, kuandaa kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge kwa kushirikiana na Tanganyika Law Society (TLS) pamoja na Zanzibar Law Society (ZLS) ameagizwa kuandaa kanuni zitakazoelekeza namna ya kufanya mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa.
Rais Samia ameelekeza hayo baada va kupokea maazimio ya awali ya Kikosi kazi kilichoteuliwa kufuatilia hoja zilizojitokeza katika mkutano wa wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa uliofanyika Desemba 2021.
Maazimio yamegawanyika katika makundi matatu ya muda wa utekelezaji; Azimio la muda mfupi ni uandaaji wa Kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya Mikutano ya Hadhara. Miongoni mwa maazimio ya muda wa kati ni Rushwa na Maadili katika Uchaguzi. Katiba mpya ni mpango wa muda mrefu.
View attachment 2148206