Tanzania tumebarikiwa kumpata Rais Samia Suluhu kama kiongozi wetu.
Wakati nchi zote mbili Tanzania na Kenya zikikumbwa na mafuriko yalisababisha maafa, majanga , vifo na huzuni. Hali hii imeonyesha ni aina gani ya viongozi tulionao.
Rais Samia Suluhu na Rais William Ruto wote walienda Dubai kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28), baada ya taarifa za maafa haya nchini mwao kila kiongozi alifanya uamuzi wake.
Rais Samia Suluhu alitanganza kusitisha zaiara yake Dubai na kurejea nchini ili kuungana na wananchi wa Hanang pamoja na kutoa maagizo ambayo tayari yameanza kutekelezwa.
Rais William Ruto ameendeleza ziara yake na sasa yupo nchini India akiendelea na shughuli zake.
Hadi sasa mafuriko ya Kenya yamesababisha vifo zaidi ya 140 huku Tanzania watu 63 wamepoteza uhai.
Kwa hili tu, unaweza kuona kwamba Afrika tuna viongozi wa aina gani, kuna wale ambao wanatanguliza maslahi ya wananchi wake na wengi sasa mmh.
Anyway , Najivunia kuwa Mtanzania. Najivunia kuongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.