Rais Samia afupisha ziara yake Dubai kurejea nchini haraka iwezekanavyo, Serikali kugharamia mazishi na matibabu ya majeruhi wa mafuriko ya Hanang

Rais Samia afupisha ziara yake Dubai kurejea nchini haraka iwezekanavyo, Serikali kugharamia mazishi na matibabu ya majeruhi wa mafuriko ya Hanang

Katika watu ambao.imani yangu imeshuka katika kutoa taarifa sensitive za serikali ni huyu..
Amedangany mara nyingi sana Sidhani kama atasema kitu ntakiamini hata akisema hii ni jf inabdi nipate uhakika..

Na huenda yeye angekaa kimya nisingekuwa na Doubt kubwa ila yeye kuongea ndo kinachoongeza wasiwasi zaidi tukumbuke Magu
Hahaha Usiwe na Mashaka ndio Ukweli Amerudi Ili Kulifanyia kazi Janga Hili kwa Ukaribu Mnoo
 
Tanzania tumebarikiwa kumpata Rais Samia Suluhu kama kiongozi wetu.

Wakati nchi zote mbili Tanzania na Kenya zikikumbwa na mafuriko yalisababisha maafa, majanga , vifo na huzuni. Hali hii imeonyesha ni aina gani ya viongozi tulionao.

Rais Samia Suluhu na Rais William Ruto wote walienda Dubai kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28), baada ya taarifa za maafa haya nchini mwao kila kiongozi alifanya uamuzi wake.

Rais Samia Suluhu alitanganza kusitisha zaiara yake Dubai na kurejea nchini ili kuungana na wananchi wa Hanang pamoja na kutoa maagizo ambayo tayari yameanza kutekelezwa.

Rais William Ruto ameendeleza ziara yake na sasa yupo nchini India akiendelea na shughuli zake.

Hadi sasa mafuriko ya Kenya yamesababisha vifo zaidi ya 140 huku Tanzania watu 63 wamepoteza uhai.

Kwa hili tu, unaweza kuona kwamba Afrika tuna viongozi wa aina gani, kuna wale ambao wanatanguliza maslahi ya wananchi wake na wengi sasa mmh.

Anyway , Najivunia kuwa Mtanzania. Najivunia kuongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

A30I4660.JPG
 
Pumbafu sana,

Af hawa ndo walio wengi kwenye serikali, walamba viatu
 
Tuache kulaumu serikali tu, hata mimi na wewe tunawajibika kusaidia wananchi wenzetu. Ndiyo tuna mamlaka isiyokidhi au kushughulikia vyema shida zetu, lakini ifike muda pia tuwe wawajibikaji.
 
COP28 siku ya mkutano wa viongozi wa nchi ilikuwa jumamosi tarehe mbili, wengi walishaondoka siku hiyo hiyo baada ya mkutano wao.

Watu waliobaki huko sasa ni policy advisors wa serikali, NGO’s na taasisi za kibiashara; labda na maraisi wa nchi za ovyo.

Akili za vijana wa CCM ni hatari kwa mustakabali wa taifa kwa sasa.
 
Ashakumu si matusi wandugu,baada ya taarifa ya maafa ya mafuriko huko wilayani Hananng,mkoa wa Manyara kullitoka taarifa rasmi kua rais ametoa maagizo kadha wa kadha huku tukiambiwa yeye mwenyewe binafsi hapo Jana alikatiza ziara yake huko Arabuni iliyokua na wajumbe zaidi ya 700 ili awahi kushughulikia janga la mafuriko.

Tangu tupewe taarifa,Rais hatujamuona akiwasili wala kwenye mkoa wa tukio,baadala yake tunamuona Waziri Mkuu akiongoza shughuli za kiserikali huko Hanang.

Tangu tupewe taarifa za ziara kusitishwa siku ya Jumapili, takribani siku 3 zinapita sasa,Je taarifa ya Rais kukatisha ziara yake ilikua fake?!! Ama anakuja kwa usafiri mwingine na wala sio dege letu lile?!
 
Back
Top Bottom