Rais Samia aitisha Baraza la Mawaziri kwa dharula, kujadili ajali ya ndege ya Precision

KWA statement hiyo!

The man is fired for real!

TOKA MAKTABA :

EDWARD LOWASSA MBUNGE WA MONDULI AJIUZULU UWAZIRI MKUU


 
aibu naona mimi

Sent from my SM-M305F using JamiiForums mobile app
 
Wasubiri ripoti ya kitaalamu unless kama wanajadili juu ya uboreshaji wa namna ya kukabiliana na majanga.
 
Mita 100 toka kiwanja cha ndege! Hata kwa kutembea mwendo wa kijeshi ni dk 1-2 tu, lakini hawakuwepo ktk uokoaji. Kikosi cha uokoaji ndio inabidi kibebe lawama zote, na sijaona maelezo ya kiongozi wao wala waziri wao yanayotosheleza.

Rubani alijitahidi sana, kimsingi abiria karibu wote wangeweza kuokolewa. Kweli dhamani ya maisha haipo Tanzania. Tukio kama hili si la kwanza wala si la mwisho, UZEMBE WETU UNATUGHARIMU.
 
Kuna kiongozi anakuwa mbuzi WA kafara
 
Sidhani kama watakuja na la maana
Tena katika nchi ambayo viongozi huteuana kwa misingi kujuana! Badala ya sifa za mtu za kielimu, uadilifu wake, na pia uzoefu wake katika utendaji wa kazi!!

Kwa kweli hata mimi sitegemei kusikia tamko lenye uwajibikaji ndani yake.
 
Ahsante sana mkuu

Tuletee na ya Wizara ya Mambo ya Ndani Jeshi la Zima moto na Uokoaji
 
Wataujenga tu ule wa kajunguti...uliokataliwa na mwendazake...


Bukoba ni mbali na miji mingi mikubwa hivyo ujenzi wa uwanja wa ndege mkubwa ni necessary...unless hawataki nchi hii ipige hatua...


Naskia hata hizo air Tz hazipaswi kutua uwanjani hapo...maana zinapaswa kwa uwanja 2.3 km nakuendelea...

Bk airport ni 1.5km na hauwezi kupanuliwa zaidi maana mbele kuna mlima na huku ziwa...na bado upande wa ziwani kuna kisiwa kilichokaa kama mlima..

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Wakatuletea na muokoaji wa mchongo wakazidi kujidhalilisha wakidhani wanapata sifa. Ule usanii ni wa kijinga sana
 
Tena katika nchi ambayo viongozi huteuana kwa misingi kujuana! Badala ya sifa za mtu za kielimu, uadilifu wake, na pia uzoefu wake katika utendaji wa kazi!!

Kwa kweli hata mimi sitegemei kusikia tamko lenye uwajibikaji ndani yake.
Shujaa angeshatumbua kitambo

Sema hili swala lina mambo mengi
 
08 November 2022

Engineer Mstaafu wa viwanja vya ndege, Bennie Muberwa Mushumbushi, ushauri wangu haujafayiwa kazi kuhusu kiwanja cha ndege Bukoba.

Mhandisi mstaafu viwanja vya ndege, Bennie Muberwa Mushumbushi katika Clouds 360 kuzungumzia sababu za ajali na usalama katika viwanja vya ndege
Source : cloudsmedia

PONGEZI KWA CLOUDSMEDIA KUFANYA MAHOJIANO NA MHANDISI WA VIWANJA VYA NDEGE KIMATAIFA

Mhandisi mstaafu wa viwanja vya ndege aliyefanya kazi kimataifa ikiwamo shirika la kimataifa la anga ICAO , Bennie Muberwa Mushumbushi katika Clouds 360 kuzungumzia sababu za ajali na usalama katika viwanja vya ndege.

Andiko la mhandisi Bennie Muberwa Mushumbushi mwaka 2015 lilipendekeza .... pia suala la mazingira yanayozunguka airport ya Bukoba ikiwemo viwanda vya minofu vinavyovutia ndege -kiumbe

Andiko hilo liliwakilishwa wizarani (wizara ya Ujenzi) mwaka 2017 ili kuepukana na matatizo ambayo yangetokea kwenye uwanja ule. Mimi ni Mzaliwa wa kule (Bukoba) ili kuona kuna kiwanja kizuri cha ndege kwa sababu kuna abiria wengi Sana kule. Sikupata majibu mazuri lakini walipokea andiko langu na kusema watalifanyia kazi.

Kuna wakati nilijiuliza sana na nikasema nafanya tu huduma kwa sababu nina ujuzi wa hivi vitu na hili jambo linaendelea na hakuna mtu anayejali. Nilikwenda makao Makuu ya Chama CCM, Kagera"

"Nilitaka kuzungumza na Mwenyekiti wa CCM, Kagera alikuwa anasafiri alinipatia Msaidizi wake ili anisaidie tulieleza hali halisi ya uwanja wakasema wao sio wataalamu, wakaniuliza kama nililipeleka hilo jambo mkoani nikasema hapana!

"Nilikwenda kwa Katibu Tawala wa Mkoa (wakati ule) akasema pia na yeye ana wasiwasi juu ya huo uwanja na walishauona na hawajui wafanye nini. Nilipata nafasi ya kuongea na wabunge wawili wa mkoa wa Kagera. Hili suala hadi leo halijafanyiwa kazi" Engineer Mstaafu wa viwanja vya ndege, Bennie Muberwa Mushumbushi

Ndege ya Bombadier ya ATCL inahitaji urefu wa kilometa 2 kutua salama bila changamoto .....

Additional info and source :

13 November 2017

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania - TAA

Uwanja wa ndege mjini Bukoba uliofanyiwa ukarabati wazinduliwa. Na mengi yamebainishwa kwa kirefu na viongozi wa juu wa TAA katika mahojiano haya exclusive
Source : Tekno Leo


 
Tena muokoaji mvuvi shujaa anapewa pesa sawa na AFTATU
 
Swis wamezi ground hizo Ndege since 2019, CCM mkawa mnazirusha na huenda walikuwa hawajui, wame react juzi baada ya ajali ya Precision Air
 
Sa hapo watakuwa wanajadili nn wakati yale (ajali ya ndege) ni mambo ya kitaalam zaidi?!.
Kama hicho kikao kina posho itakuwa ni wizi tu kama wizi mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…