Rais Samia aitisha Baraza la Mawaziri kwa dharula, kujadili ajali ya ndege ya Precision

Rubani hakuweza kuuona vizuri uwanja wa kutua ndege wa Bukoba kwa sababu ya giza lililosababishwa na hali ya hewa. Kwa nini taa za uwanja hazikuwashwa au umeme wa tanesco ulikuwa umekatika kama kawaida yake? Kama uwanja haukuwa na taa, ni wizara gani ilizembea?
 
.
 

Ajali ilitokea lini? Hicho kikao cha dharura ndo kinaitishwa leo? Ingekuwa dharura kwanza asingeenda Misri badala yake angeitisha hicho kikao wakati huo.

MaCCM ndo yalivyo!
 
Well Noted Mkuu....
 
Isambazwe katika mitandao yote. Ni muhimu kuiangalia hii klip kabla hujapanda ndege, na kurudia mara kwa mara kuiangalia.

Hata kwa wasiopanda ndege ni muhimu vilevile kuiangalia, hujui itakufaa lini pengine utakuwa muokoaji ajali inapotokea. Nawasilisha.
 
Uwanja hauna taa
 
Hakuna kitu kipya CCM inaweza kudeliver kwa nchi hii.. HAKUNAAA
 
Swala la ajali ya ndege yenye abiria 48 linapataje umuhimu kuliko swala la maji linalowatesa Watanzania ndani na nje ya Dar? Kwangu la maana ni kutoka na jibu la kutengeneza vyanzo vingine vya maji si kila siku Ruvu chini na Ruvu juu
Kwasababu hakuna takwimu za vifo/magonjwa vinavyosababishwa na ukosefu wa maji. Ni tatizo lililo nyuma ya pazia.
 

Mkuu kwani tuna;
1. Bombadia ngapi?
2. Dreamliner ngapi?
3. Airbus ngapi?

Nasikitika hizi ndege kuwa na engine mbovu kwani ukizipanda ni tamu sana pamoja na dreamliner.
Bombadia zina vikelele flani na kuyumba angani
 
Swala la ajali ya ndege yenye abiria 48 linapataje umuhimu kuliko swala la maji linalowatesa Watanzania ndani na nje ya Dar? Kwangu la maana ni kutoka na jibu la kutengeneza vyanzo vingine vya maji si kila siku Ruvu chini na Ruvu juu
Wanatuyumbisha tu akili.
 
Huu ni mwanzo mzuri wajadili pia na namna ya kukabiliana na majanga kwa haraka endapo yatatokea kama haya huko mbele.

Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
"Yaliyopita si ndwele tuganage yajayo "
kauli hii hawezi kuelewa mfiwa. waliopewa dhamana wawajibishwe
 
Mazingira ya wahuni kumuondoa waziri mkuu ili wamuweke mtu wao waendelee kula nchi yanaandaliwa. Bei ya bidhaa kupanda/Mgao maji/Umeme pia si dharura??

Waziri mkuu aliyeko madarakani kwa wizi wa kura sio muhuni? Bidhaa zimepanda yeye akiwa waziri mkuu, sasa kuna ajabu gani akitolewa?
 
Si wameshachukua hatua kupitia kipimajoto sijui malumbano ya hoja itv? Maana tumeona kina Kova sijui wana kampuni za uokoaji na kina Mbatia wataalamu wa majanga wakilumbana kwenye iko kipindi lakini hawakukimbilia eneo la tukio ili waokoe watu siku hiyo!
 
Huu ni mwanzo mzuri wajadili pia na namna ya kukabiliana na majanga kwa haraka endapo yatatokea kama haya huko mbele.

Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
Hatukujifunza kwenye ajali ya Mv Bukoba ikatokea tena ziwa Victoria ajali ya kivuko MV Nyerere.
Hatukujifunza kwa Ajali ya Treni Morogoro. Hagukujifunza kwenye ajali ya moto Idweli Mbeya, ikatokea ajali ya namna ileile Morogoro

Majanga yote haya na mengine mengi bado hayajaacha somo kwenye akili za viongozi wa nchi hii na sisiyemu yao. Kazi ulafi tu
 
Tena katika nchi ambayo viongozi huteuana kwa misingi kujuana! Badala ya sifa za mtu za kielimu, uadilifu wake, na pia uzoefu wake katika utendaji wa kazi!!

Kwa kweli hata mimi sitegemei kusikia tamko lenye uwajibikaji ndani yake.
Kwani Kuna kiongozi hapa duniani huteu Watendaji usio wajua?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muhimu Mawaziri waangazie na kujadili mambo yafuatayo:
1. Hali ilivyo kwa sasa kuhusu majanga na uokoaji. Wawe wakweli kuhusu hali halisi,weledi,vifaa, wataalam, magari na mfumo mzima na changamoto zake
2. Sera,sheria na kanuni,miongozo na mifumo waone kama inakidhi matarajio na inaenda na mabadiliko ya teknolojia na aina na ukubwa majanga na complexity zake.
3.tumejifunza nini kuhusu majanga mbalimbali 1961-2023,udhaifu na changamoto
4.uwezo wa kitaasisi kukabiliana na majanga
5.uwekezaji binafsi na kiserikali kwenye kukabiliana na majanga
6. Uratibu
7.elimu kwa wananchi
8. Predictions....Kwa baadaye nini kifanyike kuhusu majanga ya majini,ardhini, tetemeko,ajali za mageri,treni,moto migodini, ndege nk. Tuje na suluhisho pro active.
Vinginevyo tusikimbilie kufikiria nani anaachia ngazi PM,KAMISHNA ZIMA MOTO,MAMBO YA NDANI, UJENZI etc So far taarifa ya uchunguzi haijatoka tujue chanzo cha ajali hasa ni ndege, kiwanja,control tower, Tujikite kwenye mitigation zaidi na yanayoonaka kwa macho ya kiuzembe vinginevyo likiisha hili linakuja lingine utamaliza watu,tunahitaji mikakati ya muda mfupi na mirefu na yenye mbinu za kisasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…