Maisha yatapanda na yatazidi kupanda MILELE, na wala hayajawahi kuwa RAHISI, tatizo ni kwamba VIONGOZI wa NCHI hawana MIPANGO endelevu ya kuinua PATO la MTU mmoja mmoja. SERIKALI badala ya kupigana kuinua KIPATO cha yule MTANZANIA wa MWISHO kule ambaye anabeba MZIGO wote wa hizi BEI mnahangaika na BEI yenyewe.. Hiyo BEI siyo tatizo, bali NGUVU YA MANUNUZI ya WATANZANIA ndo TATIZO…
Jibu la haya yote ni SEKTA ya KILIMO ambayo mmeamua KUISIGINA kwa MAKUSUDI. Ni kweli kuna UWEKEZAJI wa SEKTA zingine kama UTALII, VIWANDA na MADINI unafanyika ila ni SERIKALI ndo inafaidika ZAIDI kwa KODI moja kwa moja lakini WANANCHI WENGI hawafaidiki moja kwa moja pamoja na ajira chache wanazopata ambazo haziwezi kuinua asilimia kubwa ya wananchi walio na hali duni kimaisha… Kwanini kwa dhati kabisa KILIMO kisifanyiwe MKAKATI kwenye UWEKEZAJI uliotukuka na siyo GERESHA kama zile za KILIMO KWANZA ambayo mpaka leo hatujawahi pewa mrejesho wowote?
KILIMO ndo SEKTA pekee duniani inayotoa ajira kwa WATU WENGI wa HALI zote za kimaisha bila kutegemea MAHALI husika,,,
Nchi yetu ina KANDA nyingi za KILIMO ambazo zinaweza kugawanywa kutokana na ZAO husika, halafu SERIKALI au WAWEKEZAJI wakatengeneza MIUNDOMBINU ya KUMWAGILIA tukaachana na KUTEGEMEA MVUA. MIPANGO mingi mizuri inaozea kwenye makabati na hii inasababishwa na 10% zinazopatikana kwenye UWEKEZAJI wa CHAP CHAP na RAHISI kufanyika kwenye SEKTA nyingine kwakuwa VIONGOZI hawataki kuhangaika na KILIMO ambacho kinaonekana KIGUMU kwenye UWEKEZAJI lakini kina MATUNDA mazuri kwa TAIFA hili..
Leo tunaagiza MAFUTA ya KULA wakati nchi hii ina ardhi ya CHIKICHI, SOYA na ALIZETI.. Tunaagiza SUKARI wakati tuna ardhi ya MIWA,, tunaagiza NGANO wakati tuna ardhi ya kuilima hiyo NGANO.. Hivi vyote vingekuwa vinalimwa kwa UKAMILIFU wake hakika vilio vyote hivi visingelikuwa kwa UKUBWA uliopo.. Kwasababu tusingukuwa tunaagiza bidhaa nyingi nje kwahiyo hela yetu ingekuwa na NGUVU sokoni…
Hivi VIKAO vya Saa 10 usiku mtakaa sana huko tuendako maana VIONGOZI ni wale wale wenye FIKRA zile zile za kuongeza KODI na TOZO kwenye MAFUTA yale yale na VITU vyenye URAHISI wa MALIPO badala ya kutafuta NJIA MBADALA.