Rais Samia aitisha kikao cha dharura usiku huu (Mei, 08 2022) Ikulu Dar Es Salaam kujadili mafuta

Rais Samia aitisha kikao cha dharura usiku huu (Mei, 08 2022) Ikulu Dar Es Salaam kujadili mafuta

Rais Samia ameitisha kikao ikulu udiku huu kujadili kupanda kwa bei ya mafuta , huku kikao hiko kikihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati January Makamba, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata na wajumbe wengineo

Tutarajie tamko la namna gani baada ya kikao hiko ndugu mdau wa jamii forums?

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

Naona mama keshaunga mkono juhudi kwa kuachana na kongwa la BARAKOA!! Hongera sana mama, furahia oxygen!!
 
Kuna masuala unatakiwa kujua wakati sahihi wa kushughulika nayo.
Nadhani hivi vikao vilipaswa kufanyika KABLA bei ya mafuta haijapandishwa.
Sasa hivi mnaweza kushusha bei ya mafuta sababu mna mfumo wa kudhibiti bei ya bidhaa hiyo,what about hizi bidhaa nyingine na masoko yake mitaani ambayo wafanyabiashara wamechukulia advantage na kupandisha bei zake,how can you regulate that area?Hivi mama ntilie akishapandisha bei ya ubwabwa wake can you come and tell her to lower the price again?!unaweza kirahisi kumwambia mangi ashushe bei ya mchele wake?
Narudia tena,kuna mambo mnapaswa kujua wakati sahihi (timing) wa kudeal nayo.
 
Waafrika tunapenda sana kula imagine kikao serious kama hicho kimejaa machupa na majuisi sijui makorosho kwani wangekula baada ya kumaliza ingekuwaje? Hatuko serious kabisa kila sehemu tunawaza kula kula hovyo tu.
Najiuliza hapo na usiku wote huo lazima kunna watu walisinzia tu😂😂😂🤣🤣
 
Hilo unalisema wewe. Hamna pakuhujumu zaidi ya maneno ya kijinga tu. Tunawafahamu, mlikuwa hivihivi wakati wa Mwinyi, mkayarudia tena wakati wa Kikwete na mtaendelea nayo kila ataposhika Muislam. Mwiso wa siku tukilinganisha tunaona kuwa hakuna viongozi bora wa nchi hii zaidi ya Waislaam.
Katika viongozi walifeli kitaifa kuongoza Basi ni Hawa waislàmu ..Yani humo ndio mabalaa yote hutokeaga, maufisadi, maajali, manjanga ..Yani ni shida tupu..Tena huyu mama anaupiga mwingi Ila uislamu wake na ukike wake wahujumu uchumi wanakula naye Shani moja.
 
Hahahah nchi ina raha hii, hivi hapa majuzi ni nani aliamuru kua ile mia iliyotolewa kupunguza ukali wa bei ya mafuta irudishwe hata kama yanapanda. Leo imekuaje tena anastuka anataka solution 😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃
 
Naona mama keshaunga mkono juhudi kwa kuachana na kongwa la BARAKOA!! Hongera sana mama, furahia oxygen!!

Hewa ya hapo chumbani itakuwa imechukuliwa vipimo vya covid na majibu ya kawa negative. Tanzania tunao uwezo wa kupima mpaka mananasi covid usisahau hilo.
 
Hahahah nchi ina raha hii, hivi hapa majuzi ni nani aliamuru kua ile mia iliyotolewa kupunguza ukali wa bei ya mafuta irudishwe hata kama yanapanda. Leo imekuaje tena anastuka anataka solution 😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃

Mia iliondolewa bila kufuata utaratibu wa vikao vya usiku nafikiri.
 
Maisha yatapanda na yatazidi kupanda MILELE, na wala hayajawahi kuwa RAHISI, tatizo ni kwamba VIONGOZI wa NCHI hawana MIPANGO endelevu ya kuinua PATO la MTU mmoja mmoja. SERIKALI badala ya kupigana kuinua KIPATO cha yule MTANZANIA wa MWISHO kule ambaye anabeba MZIGO wote wa hizi BEI mnahangaika na BEI yenyewe.. Hiyo BEI siyo tatizo, bali NGUVU YA MANUNUZI ya WATANZANIA ndo TATIZO…

Jibu la haya yote ni SEKTA ya KILIMO ambayo mmeamua KUISIGINA kwa MAKUSUDI. Ni kweli kuna UWEKEZAJI wa SEKTA zingine kama UTALII, VIWANDA na MADINI unafanyika ila ni SERIKALI ndo inafaidika ZAIDI kwa KODI moja kwa moja lakini WANANCHI WENGI hawafaidiki moja kwa moja pamoja na ajira chache wanazopata ambazo haziwezi kuinua asilimia kubwa ya wananchi walio na hali duni kimaisha… Kwanini kwa dhati kabisa KILIMO kisifanyiwe MKAKATI kwenye UWEKEZAJI uliotukuka na siyo GERESHA kama zile za KILIMO KWANZA ambayo mpaka leo hatujawahi pewa mrejesho wowote?

KILIMO ndo SEKTA pekee duniani inayotoa ajira kwa WATU WENGI wa HALI zote za kimaisha bila kutegemea MAHALI husika,,,

Nchi yetu ina KANDA nyingi za KILIMO ambazo zinaweza kugawanywa kutokana na ZAO husika, halafu SERIKALI au WAWEKEZAJI wakatengeneza MIUNDOMBINU ya KUMWAGILIA tukaachana na KUTEGEMEA MVUA. MIPANGO mingi mizuri inaozea kwenye makabati na hii inasababishwa na 10% zinazopatikana kwenye UWEKEZAJI wa CHAP CHAP na RAHISI kufanyika kwenye SEKTA nyingine kwakuwa VIONGOZI hawataki kuhangaika na KILIMO ambacho kinaonekana KIGUMU kwenye UWEKEZAJI lakini kina MATUNDA mazuri kwa TAIFA hili..

Leo tunaagiza MAFUTA ya KULA wakati nchi hii ina ardhi ya CHIKICHI, SOYA na ALIZETI.. Tunaagiza SUKARI wakati tuna ardhi ya MIWA,, tunaagiza NGANO wakati tuna ardhi ya kuilima hiyo NGANO.. Hivi vyote vingekuwa vinalimwa kwa UKAMILIFU wake hakika vilio vyote hivi visingelikuwa kwa UKUBWA uliopo.. Kwasababu tusingukuwa tunaagiza bidhaa nyingi nje kwahiyo hela yetu ingekuwa na NGUVU sokoni…

Hivi VIKAO vya Saa 10 usiku mtakaa sana huko tuendako maana VIONGOZI ni wale wale wenye FIKRA zile zile za kuongeza KODI na TOZO kwenye MAFUTA yale yale na VITU vyenye URAHISI wa MALIPO badala ya kutafuta NJIA MBADALA.

Kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji imekuwa ni hadithi za alifulela ulela katika taifa hili. Na ukweli wenyewe inaonesha uwekezaji huu hauna mrejesho wa haraka kama ule wa tehama Tanesco na kufatiwa na msd.
 
Yanaitishana usiku wa manane, halafu yanatoka bila suluhisho! Majitu mengine hayana mishipa ya aibu!
 
Nawaza tu ,

Baraza la mawaziri walipokaa mara ya mwisho wakiongozwa na waziri walikosa muarobaini. Rais, hawezi kutoa tamko? Wafanyabiashara wa mafuta na wahisani si wanafahamika ? Hivi vikao vinavyokosa suluhu vya nini ? Au umuhimu wa wabobezi wa uchumi haliwahudu ilihali tunajenga nyumba moja.
 
Rais Samia ameitisha kikao ikulu udiku huu kujadili kupanda kwa bei ya mafuta , huku kikao hiko kikihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati January Makamba, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata na wajumbe wengineo

Tutarajie tamko la namna gani baada ya kikao hiko ndugu mdau wa jamii forums?

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

sasa icho kikao cha usiku na kila mtu amepigilia Misuti si wangevaa Ma pajama tu

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Rais Samia ameitisha kikao ikulu udiku huu kujadili kupanda kwa bei ya mafuta , huku kikao hiko kikihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati January Makamba, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata na wajumbe wengineo

Tutarajie tamko la namna gani baada ya kikao hiko ndugu mdau wa jamii forums?

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

Bata limerudi rasmi. Enzi za awamu ya tano hapo mezani pangekuwa na maji tu kwa kila mtu. Maana yake tuishi kwa kutegemea mishahara yetu.
 
Katika viongozi walifeli kitaifa kuongoza Basi ni Hawa waislàmu ..Yani humo ndio mabalaa yote hutokeaga, maufisadi, maajali, manjanga ..Yani ni shida tupu..Tena huyu mama anaupiga mwingi Ila uislamu wake na ukike wake wahujumu uchumi wanakula naye Shani moja.
Aaah migodi aliyoirudisha Kikwete iliuzwa na nani na kwa nani? Unaelewa?? Mawaziri waliofungwa wakati wa Kikwete umewasahau, na kwanini? Nikukumbushe? Waziri Mkuu aliyeweka rekodi ya kufukuzwa? Wakati nani akiwa Rais?

Hayo machache yanakutosha kwa yaliyopita, sitaki kwenda mbali zaidi.

Kwa ya juzi tu hapa: Ni nani aliyekopa pesa za kujengea treni ya umeme akaenda kujenga eyapoti kijijini kwao?

Hayo yote yana ushahidi kamili, sasa wewe umeleta porojo zako tu bila chochote chenye mashiko. Ukitaka nikurudishe nyuma zaidi, nipo tayari. Upo hapo ulipo?
 
Aaah migodi aliyoirudisha Kikwete iliuzwa na nani na kwa nani? Unaelewa?? Mawaziri waliofungwa wakati wa Kikwete umewasahau, na kwanini? Nikukumbushe? Waziri Mkuu aliyeweka rekodi ya kufukuzwa? Wakati nani akiwa Rais

Hao waliofungwa wakati wa Kikwete ni kwasababu walimyima mgao katika ufisadi wao ; kuwaonesha yeye ni nani Ndio akawafanyia figisu wakafungwa! Kashfa ya Richmond ile Ilikuwa ni ya Kikwete mwenyewe lakini Lowassa akamsitiri bila kufahamu kuwa mwenzie ni nyoka wa mdimu!!
 
Hakuna kitakachobadilika mpaka Russia na Ukraine waache kupigana...
 
Back
Top Bottom