Rais Samia amteua Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF)

Rais Samia amteua Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF)

Taarifa inaeleza kwamba Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, ili kuziba pengo lililoachwa na na Venance Mabeyo anayestaafu kwa mujibu wa Sheria.

Kwangu mimi General Mkunda ni jina jipya kabisa, Naomba mwenye kuufahamu wasifu wa kiongozi huyu atuwekee hapa tumfahamu, japo kwa ufupi tu ili tusiingie ndani sana kwenye mambo ya Kijeshi.

Natanguliza shukrani
 
huwa sipendi kusikia Mkuu wa Majeshi anaitwa "Afande...Mkuu wa Majeshi" sielewi hili neno "afande" ni sahihi kulitumia kwa wenye vyeo vya juu?!

kwa uelewa wangu nilidhani kwa vyeo vya juu anatakiwa kuitwa "kamanda".
naomba ufafanuzi kwa wenye kujua maana huwa nahisi kumuita "afande" ni kama kudunisha cheo chake.
wataalamu naomba mtusaidie hapo.
Hata Rais ni Afande
 
Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali, na amemteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF).

Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi.

====

RAIS, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali na amemteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (Chief of Defence Forces – CDF).

Kabla ya Uteuzi huo, Mkunda alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi (Chief of Operations and Training).

Rais Samia pia amempandisha Cheo Meja Jenerali Salum Haji Othman kuwa Luteni Jenerali na amemteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (Chief of Staff – C of S).

Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Othman alikuwa Kamishna wa Utafiti na Maendeleo Jeshini (Commissioner for Research and Military Development) katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Vile vile amemteua Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Uapisho utafanyika tarehe 30/06/2022 saa saba mchana Ikulu, jijini Dar es Salaam.

View attachment 2276626

View attachment 2276683
Picha: Meja Jenerali Jacob John Mkunda
Uteuzi mzuri wenye dalili za kuijibu hii hoja, Je, Kuna Uhusiano wa Dini, Kabila na Ukakamavu?. Watu wa Dini, Kabila fulani, ni wazuri zaidi jeshini kuliko dini, kabila nyingine? Tangu kuanzishwa kwake JWTZ mwaka 1964, baada ya Luteni Generali mmoja tuu mwenye jina la Abdalah, ambaye alikuja kuwa CDF, leo ndio Luteni Generali wa mwingine mwenye jina la Salumu ameteuliwa, akiwa ndie Mzanzibari wa kwanza kufikia cheo hicho, na hivyo kuweka a possibility ya Tanzania kuja kupata CDF kutoka upande wa pili wa Muungano in future.
NB. Naomba kuweka caveats ya kutuhumiwa mbaguzi, makabila na mdini, amini usiamini my concern were bonafide genuine kuuliza mbona ma CDF wote ni kutoka upande mmoja na dini moja?. Unaweza kukuta no one noticed anything mpaka baada ya concern, ndio watu wakajiuliza, hivyo ikabidi kaji affirmative action kafanyike kumuondoa Luteni Generali aliyefuata kwenye normal progression ya kuja kuwa CDF, ili to create a room ya mtu wa kwanza wa upande wa pili naye aweze kuwa Luteni Generali!. Na kwa faida ya wanajukwa hili Pasco Mayalla kabla ya kuwa mtangazaji wa RTD, alipitia JKT Makotupora na MMJKT, kisha akajiunga straight na JWTZ Airwing na kuajiriwa with MT. Number, na sasa ni askari wa akiba, ikitangazwa vita sisi ndio tunatangulizwa mbele ili tuwe chambo.
P
 
Kwenye hili nimpongeze Raia Samia
 
Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali, na amemteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF).

Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi.

====

RAIS, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali na amemteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (Chief of Defence Forces – CDF).

Kabla ya Uteuzi huo, Mkunda alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi (Chief of Operations and Training).

Rais Samia pia amempandisha Cheo Meja Jenerali Salum Haji Othman kuwa Luteni Jenerali na amemteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (Chief of Staff – C of S).

Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Othman alikuwa Kamishna wa Utafiti na Maendeleo Jeshini (Commissioner for Research and Military Development) katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Vile vile amemteua Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Uapisho utafanyika tarehe 30/06/2022 saa saba mchana Ikulu, jijini Dar es Salaam.

View attachment 2276626

View attachment 2276683
Picha: Meja Jenerali Jacob John Mkunda
Tuna pokea ila huu uteuzi una siri kali... Let keep silence muda utatupa majibu japo tunaliomnea Taifa letu. Amen
 
Taarifa inaeleza kwamba Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi , ili kuziba pengo lililoachwa na na Venance Mabeyo anayestaafu kwa mujibu wa Sheria .

Kwangu mimi General Mkunda ni jina jipya kabisa , Naomba mwenye kuufahamu wasifu wa kiongozi huyu atuwekee hapa tumfahamu , japo kwa ufupi tu ili tusiingie ndani sana kwenye mambo ya Kijeshi .

Natanguliza shukrani
Wewe umeona nikawaida hata kabla yakuuliza huwo wasifu?
 
Back
Top Bottom