Rais Samia apende-asipende siku yaja atamfuta Uwaziri January kwa shinikizo la wananchi

Rais Samia apende-asipende siku yaja atamfuta Uwaziri January kwa shinikizo la wananchi

Huku mtaani jamaa anazungumziwa vibaya.

Na Rais naye bado ana mwamini.

Kwahiyo ni maneno ya watu mitaani ambao hao ndio wapiga kura dhidi ya imani ya Rais kwake.

Mwenye maamuzi ya mwisho ni mwenye mamlaka.

Anajua mwenyewe anafanya nini na serikali yake.
January ule mvuto umepotea kabisa, alifaa awe Waziri wa michezo
 
January nahisi nyota yake ina giza sana!

Haiwezekani yeye tu kutajwa na hata kusemwa kwa ubaya tuuuu!

Ukiona jamii inayokuzunguka haishi vigenge vya kukusema kwa ubaya tambua kutoboa kwako katika jambo fulani itakuwa vigumu sana.

Ukweli ni kwamba 75% ya Watanzania hawamweli na zaidi hawampendi January ama kwa kukalilishwa ubaya wake ama kwa hila.

Kwa chuki zilizo bayana kwa January kutoka Watanzania wengi hasa masikini wanaoendelea kuaminishwa kwamba jamaa ni mtesi wao basi tujiandae na mtikisiko mkuu ndani ya siasa za CCM huko mtaani.

Yatapotukia hayo basi mteule wake atakuwa hana chaguo jingine zaidi ya kumtoa kafala kwa maslahi mapana ya kisiasa kwake.

Ikumbukwe hata Kikwete alilazimika kumtosa rafiki yake Karamagi kwa kulazimishwa na sintofahamu ya kisiasa huko mtaani.

Hata isipokuwa mwaka huu lakini natabiri January hatoboi 2025.
kisiasa wizara ya nishati si wizara nzuri kuwepo mwanasiasa mwenye malengo, ni wizara ambayo inawagusa moja kwa moja wananchi na ukiboronga wanajua ata wasio na upeo wa utambuzi wakujua watajua, mfano umeme unakatika masaa kazaa msimu wa mvua nchi nzima yule mwanakijiji aliekuwa anaenda kusaga unga wake analala njaa akijua kabisa issue ni umeme. hitimisho January asisubiri kuondolewa ajiuzulu tu kuliko litokee la kutumbuliwa
 
Kama hatomfuta January ataendelea kusababisha skendo Hadi 2025 halafu wananchi watawafutilia mbali wote wawili...
 
Yaani wewe nani unampa Rais ultimatum?
Hakuna unachokijua wacha kujipandisha kwa kuleta chuki zisizokuwa na mbele wa nyuma na kujigeuza mtabiri.
 
Hivi January amewakosea nini? mbona anaandamwa Sana! mawaziri wapo wengi lkn January naona anaongoza kwa kutupiwa madongo! watanzania tupendane! maendeleo yetu hayawezi kuja kwa kumchukia aliyefanikiwa, tupige kazi wandugu, tupige kazi.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Hivi January amewakosea nini? mbona anaandamwa Sana! mawaziri wapo wengi lkn January naona anaongoza kwa kutupiwa madongo! watanzania tupendane! maendeleo yetu hayawezi kuja kwa kumchukia aliyefanikiwa, tupige kazi wandugu, tupige kazi.
Hatutaki ufalme akawe lecturer
 
Hawa ni kuwaangalia na kuwaambia heee ba ngosha vipi? Ujue pale Tanesco na Sgr ni miradi ya upigaji ya sukuma gang kwa hiyo January kakata ulaji kwenye Bwawa ndio maana unaona kelele..

Pili bado Kwa Kadogosa,kuwadi wa Yapi Merkez
Walipiga ngapi waliokuwepo??
 
Kwani Hawa wa Sasa unajua kiasi wanachopiga?

Kwenye upigaji hakuna hafla ya kualika watu.



Kama umefuatalia bunge na kusikiliza michango ya wabunge wakilalamikia TANESCO ifike mahala jiwekee mipaka ya kutetea kila ujinga.

TANESCO wana mafanikio gani ya kutumia hela kuzindua upuuzi kama huo hapo kwenye video na kukodi msanii wa kuwaburudisha.

Nchi inalia na umeme mkrugenzi na wafanyakazi wana muda wa kufanya sherehe na kukata muono.

Kama hizo sio dharau ni nini?
 



Kama umefuatalia bunge na kusikiliza michango ya wabunge wakilalamikia TANESCO ifike mahala jiwekee mipaka ya kutetea kila kitu.

TANESCO wana mafanikio gani ya kutumia hela kuzindua upuuzi kama huo hapo kwenye video na kukodi msanii wa kutumbuiza.

Kesi ya Tanesco haijaanza Jana bali ina matatizo ya msingi ambayo ya atokana na muundo wake na yanahitaji pesa nyingi..

Kulalamika ni sifa ya watzn lakini hawana majibu .

Chukua kopi ya Mwananchi ujielimidhe,Baadhi ya shida za Tanesco hizi hapa 👇

Screenshot_20220410-084440.png


Screenshot_20220410-084749.png
 
Nakukumbusha mwaka 2015,makamba,kinana ,nape
Walikuwa kwenye timu ya kufanya magumashi ili magufuli atoke.
Na hao wote wapo NDANI.
Samia anajiandaa
 
JM kawekwa kwenye wizara ile kimkakati. Bado yupo yupo sana tu kwa kuwa kuna Kingmaker mmoja kashika remote control kutokea miles kadhaa
 
Back
Top Bottom