Kuna uwezekano mkubwa Paul Makonda akaunganishwa kwenye tuhuma za uhujumu uchumi zinazomkabili Ole Sabaya ambaye Rais Samia Suluhu ameamuru achunguzwe. Sababu zinazopelekea kuunganishwa huku ni kwa sababu ya staili ya uporaji fedha kutoka kwa wafanyabiashara inayotumiwa na Sabaya kufananishwa na staili ya Makonda (Makonda style). Ukimsikiliza vizuri mfanyabiashara huyu hapa chini aliyeibua sakata la uporaji wa Sabaya utagundua kwamba Makonda na Sabaya huenda wapo kwenye kikosi kimoja na aina yao ya uhujumu uchumi inafanana pia:
Mfanyabiashara huyu ametamka kinagaubaga kwamba Sabaya alipokuwa akimtisha ampe fedha alisema anatumia ‘Makonda style’. Kwa maana hiyo, Sabaya anafahamu staili ya uporaji wa Makonda na kwa kuwa mwizi hushikwa na mwizi mwenzie, kuna uwezekano mkubwa wawili hawa walikuwa akishiriki uhujumu uchumi kwa namna moja.
Kuna ufanano mkubwa wa Makonda na Sabaya katika mambo mengi tu. Mosi, wote ni ‘watoto’ wa mwendazake kwa kuwa hata wafanye madudu kiasi gani mwendazake alikuwa hawezi kuwachukulia hatua zozote. Ishu ya Sabaya kupora fedha za wafanyabiashara kwa vitisho ilishawafikia mwendazake na Waziri Mkuu lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa. Jeuri hii iliwapelekea kufanya chochote watakacho bila hofu yoyote.
Pili, Makonda alishuhudiwa akiwadhalilisha wanaume wa Dar kupitia programu bubu ya kuwasaka wanaume waliowatelekeza wanawake zao na hali hii ilikwakera watu wengi lakini hakufanywa chochote na aliyemteua. Aidha, Sabaya amefanya madudu mengi sana wilayani Hai lakini mwendazake alikaa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea.
Tatu, Sabaya amekuwa akitembea na kikundi cha Mungiki (mabaunsa) ambao huwatumia kutimiza azma yake ya kuhujumu uchumi. Hali kadhalika, Makonda alikuwa anamiliki kikundi kama hicho (makirikiri) ambao walikuwa wakimsaidia kutimiza uhujumu wake. Mfano mzuri ni pale alipovamia studio za clouds TV akiwa na kikosikazi chake hicho na kufanya vurugu kubwa akitaka kipindi chake kirushwe hewani (utadhani yeye ndiye Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media):
Ukilinganisha mfanano wa wawili hawa kisha ukaunganisha nukta, utatengeneza mstari unaowaunganisha wote pamoja. Kuna ishu ya Sabaya kukutwa na kitambulisho kinachoonyesha kuwa yeye ni mtu anayefanya kazi kikosi maalumu (wengi mmekiona mitandanoni). Huenda Makonda na Sabaya wote wamo kwenye kikosi hiki kwa kuwa pia staili zao za uhujumu zinafanana.
Kwanini sasa DPP asimuunganishe Makonda kwenye ishu ya Sabaya ili suala hili lishughulikiwe kwa pamoja badala ya kusubiri kumkamata peke yake? Wakiunganishwa wote wawili hata gharama za kuwashughulikia zitakuwa ndogo kuliko kudeal na mmoja mmoja kwa nyakati tofauti.
Mimi namshauri DPP amuunganishe Makonda kwenye skendo hii ya Sabaya kwa kuwa tayari ametajwa na Sabaya kuwa wanatumia staili moja ya uhujumu (kupitia kwa mfanyabiashara huyo anayelalamika hapo juu).