Rais Samia atoe amri Paul Makonda naye akamatwe kwa Tuhuma zake zinazoendana na za Ole Sabaya

Huyo mmiliki wa hotel ya utalii k'manjaro Jambazi sabaya alimuacha salama kweli baada ya kuyasema hayo kwa Majaliwa?
Majaliwa asingeweza kumfanya chochote kwa kuwa alikuwa analindwa na mwendazake kwa gharama zozote zile. Ndio maana alilia kama mwanamke alipofariki mwendazake.
 
Aunganishwe tu.
Wote wezi hawa.
 

Ila si wanasema huyu jamaa……..[emoji38] ngoja nikaushe
 
Ni kwanini Rais anamchelewesha huyu?
Huyu mtu muhimu sana wewe hujui tu,naomba Mama amteue kuwa mbunge hatimaye waziri,Kama sijapoteza kumbukumbu alitekwa Mo/Roma RC Makonda akatoa tamko kwamba aliyetekwa atapatikana na akapatikana kweli ndani ya muda
 
Hahaha prof
 
Huyu mtu muhimu sana wewe hujui tu,naomba Mama amteue kuwa mbunge hatimaye waziri,Kama sijapoteza kumbukumbu alitekwa Mo/Roma RC Makonda akatoa tamko kwamba aliyetekwa atapatikana na akapatikana kweli ndani ya muda
Alitamka Roma na Mo wakarudishwa kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa mkuu wa kikosi cha utekaji kilichoanzishwa na mwendazake kwa malengo maalumu.
 
Na lazima apelekwe mahakamani kwa kosa lá kuharibu biashara ya Ngada.
 
Hivi makonda yupo town kweli? Aisee maisha unakwenda kasi saana....teh teh teh
Yupo anasubiri mama amuonee huruma amteue walau kuwa mkuu wa tarafa. Atasubiri sana kama fisi anayesubiri mkono wa binadamu udondoke ale!
 
Huyo Bashite hata sponsor wake alimchoka akampiga chini, cha maana wenye ushahidi au chochote kile kama wale wafanyabiashara wa Arusha waliofanyiziwa na nduli Sabaya waliojitoa mhanaga bila kuogopa waanze kurusha clip, msiogope coward Bashite is chicken toothless now alikuwa anaishi kutegemea wengine wamlinde, tuanze na uvamizi wa kutumia silaha pale Clouds ushahidi upo wazi, criminal Bashite asirudi tena kwenye siasa za hii nchi kaumiza watu wengi sana lazima aende jela mpuuzi huyu
 
Tuondolee upuuzi wako wa MENSA na fake IQ zako ulizodanganywa na wazungu koko
 
Kila mtu amekuwa mshauri wa rais[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Bukyanagandi kama unamshabikia Makonda kwa namna hiyo unastahili kupita Mirembe. Kama Mensa wana mwanachama mwenye IQ ambayo haijui kuwa Makonda alikuwa muuaji na dhulumati, basi Mensa ya misukule siku hizi
Here we go again, unatuletea majibu ya kitoto toto - si ajabu hii ndio mara yako ya kwanza kusikia kwamba kuna kitu kinaitwa MENSA!! Mtu ungetegemea ungetuleta hoja mbadala kinyume chake unatuletea mipasho ya taarabu - typical some skewed minded Tanzanians wamesheheni adithi nyingi za kutunga tu wakiwa na lengo la kuwaribia sifa wanadamu wenzao ambao wanawaona wanahinuka kisiasa - driven by wivu tu wa kwa nini, wako overly obsessed kusema sema vibaya mzalendo Makonda sijui kwa nini?
 
Sio kila kitu Rais Mama Yetu Samia Makonda yeye alifanya kosa la jinai kwa kujitambulisha kwa majina ambayo si yake yaani impersonalization aliyekuwa meya wa Ubungo kipindi hicho ndugu Boniface Jacob alilifikisha hili suala katika tume ya maadili ya viongozi wa umma sasa hapa ni kumkumbusha apunguze muda wake huko twitter akafuatilia hali jambo alilojinasibu nalo kipindi hicho kama alikuwa mkweli au alikuwa anatudanganya@Boniface Jacob
 
Boniface Jacob akafuatilia kule tume ya maadili hili suala limefika wapi kuliko kushinda twitter anapiga umbea
 
Basi kama Makonda ni mzalendo na maana ya neno mzalendo kwenye Kamusi ya BAKITA itakuwa imebadilika kumaanisha kuwa ni uhanithi, unyang'anyi na uuaji
 
Kijiji fulani vilitokea vita kati ya kabila X na kabila Y. Katika vile vita kabila X walionekana kushindwa. Basi maaskari wake watatu walifanikiwa kukimbia na kujificha kwenye shimo fulani ardhini.

Wakiwa chini wamejificha juu kuna majani wakapita wanajeshi wa kabila Y wakamkanyaga askari mmoja wa kabila X. Yule askari akang'aka kwa hasira.

Askari 1: "jamani kwa nini tunakanyagana?"
Wale askari wakagundua kuna mtu pale chini wakamchoma mkuki akafa.

Mwenzake kule chini akamfokea yule aliyechomwa mkuki

Askari 2: "kwa nini na wewe unasema?"

Wale askari Y wakagundua kuna mtu mwingine wakamchoma Mkuki. Akafa. Akabaki Askari mmoja aliyejificha naye akaropoka.

Askari 3: "Aheri ya mimi sijasema"

Naye wakamgundua wakamchoma mkuki akafa.

Ole Sabaya kilichomponza ni kule kusema. Kama angenyamaza watanzania walikuwa wameshasahau mabaya yake. Alipoenda kulalamika kwenye TV kuwa anakanyagwa ndipo alipo haribu.

Makonda amekuwa smart. Hajamwambia Sabaya "kwa nini na wewe unasema?" Maana angewashtua watu nao wakaanza kuchimbua yake. Makonda amenyamaza kimya.

Watanzania wamesahau zile shutma zooote zilizomhusu Makonda.wameridhika tu kuwa kwa sasa si Mkuu wa Mkoa.

Je hakuna ambaye amewaza kwenda kufungua kesi ili haya mambo kama yalikuwa kwel yakomeshwe? Je Makonda alikuwa anasingiziwa ule uhalifu na uhalamia?

Pongezi kwa Makonda. Pamoja na kukanyagwa ameendelea kunyamaza. Maana akisema tu kuwa "anakanyagwa" watu watagundua uwepo wake.

" Aheri ya mimi sikusema"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…