Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hoja dhaifu na za kitoto.Makonda naye kafaya haya haya ya Sabaya. Kuivamia clouds ni kielelezo cha nguvu ya ukatili/ukiukaji wa sheria aliokuwa nao. siyo kuwa aliishia hapo, amefanya mengi hasa ya kuchukua fedha kwa lazima kutoka wa wafanyabiashara. Akikamatwa watajitokeza wengi kutoa ushahidi.
Alifanya hayo ikaundwa kamati ya kuchunguza tukio, Jiwe akaizima. Means Jiwe alisimamia haya yote ya akina Sabaya. makonda alikuwa kipenzi cha Jiwe, hivyo alitenda atrocities nyingi.
nani alimtishia bastola Nape?
Bottomline wa kuwachunguza ni wengi sana
Hawezi kuwa na ushahidi wowote wa wauza ngada. Tume ya kudhibiti madawa ya kulevya ndiyo wana hizo details.N
Nasubiri kwa hamu litakapotokea Hilo ingawa siamini Kama litatokea...huyo dogo anaweza kuwa na ushahidi dhidi ya wabaya wake...ushahidi Kama majina makubwa ya wauza unga, majangili, na Siri nyingine..
Yuko arusha anaonekana kwa nadra sana,pesa zake za rushwa kajenga ghorofa limesimama kitambo mzigo umekataHatimaye Ole Sabaya ameingia Kingi, hiyo yaweza kuwa headline nzuri kwa magazeti ya kesho.
Nawapongeza sana watu wa mitandao ya jamii kwa kelele na sauti ambazo tulipaza mpaka huyu Dhalimu akapatikana.
Sasa napendekeza tulianzishe kwa Paul Makonda maarufu Kama Daudi Albert Bashite mpaka naye awajibishwe kwa matendo yake maovu. Kimsingi uovu wa Ole Sabaya haufikii hata robo ya uovu wa Makonda. Na kila alilokuwa anafanya Sabaya alikuwa anaiga na ku -consult kutoka kwa Makonda.
Tutumie silaha yetu ya "social media" kama wanavyotuita "key board warriors" mpaka Makonda akapate anachostahili. Tushambulie kila mahali kupitia JF, TWITTER na FB.
Hii kampeni ianze mara moja kutaja madhambi yake. Kama TAKUKURU au Polisi hawatachukua hatua, basi wanahatakati wa haki za binadamu wanaweza wakatushauri mamna ya kumfikisha Mahakamani
Tusubiri ....Kuna msemo was kiingereza unaosema ......."an ace up his sleeve"...politics is a dirty game...wakati sisi tuko mitandaoni na umbeya wetu , watu wako kazini wakipanga mikakati...utakuja kuniambia...huyo dogo mwingine hayuko peke yake..watu watamwaga ugali hapa na kuitikisa nchi..watch out...tehtehteh...Hawezi kuwa na ushahidi wowote wa wauza ngada. Tume ya kudhibiti madawa ya kulevya ndiyo wana hizo details.
Ile orodha yake ilikuwa ya kubambikiza matajiri wampe fedha baada ya kuwatishia
Arusha mjini wafanyabiashara wakubwa ni wachaga. Tambua hiloKUna kila dalili kwamba kinachofanyika ni ushabiki wa kikabila. Zomea zomea ya Sabaya inafanyika kikabila. Eti wachaga wooote walizulumiwa, na leo wanafurahia sana! Nimeona video clip za wachaga wanafurahia. Ingawa nasikia 'ujambazi' wake ulikuwa unafanyika hata Arusha, Sijaona watu wa Arusha wakiruka ruka kama ndugu zetu wa kichaga.
Ukabila hautawavusha kabila hili. Tulieni tusikie makosa, tusikie na adhabu itakayotolewa na pia tutajifunza jambo! Sasa kila mchaga akifurahia, munaturudisha kule kule tulikowastukia. Kweli munategemea Mbowe achaguliwe kuwa rais na atawale makabila mengine kwa mtindo huu?
Mimi nalifikiria lile sambwanda litakavyogombewa huko lupangoMakonda naye kafaya haya haya ya Sabaya. Kuivamia clouds ni kielelezo cha nguvu ya ukatili/ukiukaji wa sheria aliokuwa nao. siyo kuwa aliishia hapo, amefanya mengi hasa ya kuchukua fedha kwa lazima kutoka wa wafanyabiashara. Akikamatwa watajitokeza wengi kutoa ushahidi.
Alifanya hayo ikaundwa kamati ya kuchunguza tukio, Jiwe akaizima. Means Jiwe alisimamia haya yote ya akina Sabaya. makonda alikuwa kipenzi cha Jiwe, hivyo alitenda atrocities nyingi.
nani alimtishia bastola Nape?
Bottomline wa kuwachunguza ni wengi sana
Hapo ndio utashangaa kwa Nape kutojitokeza kutoa ushahidi! Nakuhakikishia Nape hawezi kupata ujasiri huo na badala yake kwa unafiki wake anaweza akamtetea Bashite. Unakumbuka alivyonyata asubuhi yote ile eti kwenda kuomba msamaha kwa baba? CCM ndivyo walivyo.Jiwe alisimamia haya yote ya akina Sabaya. makonda alikuwa kipenzi cha Jiwe, hivyo alitenda atrocities nyingi.
nani alimtishia bastola Nape?
Bottomline wa kuwachunguza ni wengi sana
[emoji3064][emoji3064][emoji2958][emoji2960]hahahaAkipelekwa mahabusu nitatafuta kosa mkoa ataokuwa niende mahabusu hiyo hiyo SANCHOKA[emoji24][emoji24][emoji24]
Wakati wananchi na wafuatiliaji wa mambo wakianza kujengewa imani ya kuwa Taifa letu linarudi kwenye utawala bora lakini pia tukielekea kwenye utawala wa sheria na Uwajibikaji kwa viongozi wetu mfano ni kufikishwa Mahakamani kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai , Ndugu Lengai Ole Sabaya.
View attachment 1808395View attachment 1808396
Katika kumbukumbu zetu wakati taifa la Marekani wakimpiga marufuku RC Paul Makonda kuingia nchini kwao kwa tuhuma mbalimbali walisema sababu kubwa ilikuwa wana taarifa na ushahidi wa uhakika kutoka vyanzo vyao kuwa kuna mambo ya kihalifu dhidi ya binadamu aliyokuwa akiyatenda. kwa kutumia nafasi yake ya ukuu wa mkoa.
Tunavyojua sisi kuwa vyanzo vyao ni CIA ikishirikiana na taasisi zingine kama MOSAD, MI6 na taasisi zao zingine kama NSA,FBI, n.k. Sasa Taarifa hizi na Ushahidi(INTEL) dhidi ya Makonda wanazo hawa ndugu zetu na tunadhani wako tayari kuzitoa kwa hatua zaidi. Ni wakati sasa wa vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama kuwasiliana na wenzetu wa USA na kupata hizi taarifa na ushahidi wao na kuzichunguza ili kuthibitisha au kumsafisha.
Yeye mwenyewe alijitetea na kusema sababu ni kupambana na ushoga lakini ikumbukwe Musevene alifosi kutunga sheria dhidi ya mashoga, Bingu wa Mutharika alishawishi mashoga wakafungwa jela,Waziri Mkuu wa Cambodia, Hun Sen aliwahi kuchochea raia kuua mashoga lakini wote hawa hawakuzuiwa kwenda USA, hivyo tusiwapuuze MABEBERU hili, tusiwadharau CIA kiasi hiki kwani lisemwalo lipo.
"Wizara ina taarifa za uhakika kuwa Makonda amehusika katika uvunjifu huo wa haki kupitia nafasi yake kama mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Katika nafasi yake hiyo, pia amelaumiwa kwa kukandamiza upinzani wa kisiasa, kukandamiza haki ya kujieleza, na kushambulia makundi yasiyo na sauti," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo ya wizara.
Pia Bwana Pompeo alisema ,"Leo tumetangaza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Christian Makonda kuwa hataruhusiwa kuingia Marekani kwa kushiriki kwake katika ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu. Tuna wasiwasi mkubwa juu ya kuporomoka kwa heshima ya haki za binadamu na utawala wa sheria nchini Tanzania," ameeleza aliyekuwa Secretary of state Ndugu Pompeo katika ujumbe wake huo.
Matamko ya jumuiya ya kimataifa kuhusu uhalifu dhidi ya binadamu yalikuwa mengi sana, ni wakati wa kujisafisha sasa na kujenga mahusiano na jumuiya hii, mfano haya hapa chini:
Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI
Serikali ya Marekani imemzuia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuingi nchini humo kutokana na kuhusika kwake kwenye uvunjifu wa Haki za Binadamu unaohusisha kunyima haki ya kuishi, uhuru na ulinzi wa watu. Katika uongozi wake, Makonda ameonesha uonevu kwa wapinzani, kuminya uhuru wa...www.jamiiforums.com
![]()
Tamko la Umoja wa Ulaya (EU) kufuatia ongezeko la matukio ya kisiasa yenye viashiria vya ukatili na vitisho Tanzania
Tamko la Umoja wa Ulaya (EU) kufuatia ongezeko la matukio ya kisiasa yenye viashiria vya ukatili na vitisho Tanzaniaeeas.europa.eu
![]()
Bunge la Ulaya laijadili Tanzania, upi mustakabali wake? – DW – 20.11.2020
Kamati ya mambo ya nchi za nje ya Umoja wa Ulaya ilijadili uchaguzi uliopita wa Tanzania na kutaja kuwa ulikiuka misingi ya kidemokrasia, na suala la kutokuwepo maambukizi ya virusi vya corona. Hakuna uamuzi wowote uliotolewa hadi sasa. Dotto Bulendu ni mwandishi habari na mchambuzi wamasuala...www.dw.com
Unaweza weka na mengine mdau tujikumbushe malalamiko kadhaa ya hawa wateule awamu iliyopita