Rais Samia atoe amri Paul Makonda naye akamatwe kwa Tuhuma zake zinazoendana na za Ole Sabaya

Rais Samia atoe amri Paul Makonda naye akamatwe kwa Tuhuma zake zinazoendana na za Ole Sabaya

Wakati wananchi na wafuatiliaji wa mambo wakianza kujengewa imani ya kuwa Taifa letu linarudi kwenye utawala bora lakini pia tukielekea kwenye utawala wa sheria na Uwajibikaji kwa viongozi wetu mfano ni kufikishwa Mahakamani kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai , Ndugu Lengai Ole Sabaya.
View attachment 1808395View attachment 1808396

Katika kumbukumbu zetu wakati taifa la Marekani wakimpiga marufuku RC Paul Makonda kuingia nchini kwao kwa tuhuma mbalimbali walisema sababu kubwa ilikuwa wana taarifa na ushahidi wa uhakika kutoka vyanzo vyao kuwa kuna mambo ya kihalifu dhidi ya binadamu aliyokuwa akiyatenda. kwa kutumia nafasi yake ya ukuu wa mkoa.
Tunavyojua sisi kuwa vyanzo vyao ni CIA ikishirikiana na taasisi zingine kama MOSAD, MI6 na taasisi zao zingine kama NSA,FBI, n.k. Sasa Taarifa hizi na Ushahidi(INTEL) dhidi ya Makonda wanazo hawa ndugu zetu na tunadhani wako tayari kuzitoa kwa hatua zaidi. Ni wakati sasa wa vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama kuwasiliana na wenzetu wa USA na kupata hizi taarifa na ushahidi wao na kuzichunguza ili kuthibitisha au kumsafisha.
Yeye mwenyewe alijitetea na kusema sababu ni kupambana na ushoga lakini ikumbukwe Musevene alifosi kutunga sheria dhidi ya mashoga, Bingu wa Mutharika alishawishi mashoga wakafungwa jela,Waziri Mkuu wa Cambodia, Hun Sen aliwahi kuchochea raia kuua mashoga lakini wote hawa hawakuzuiwa kwenda USA, hivyo tusiwapuuze MABEBERU hili, tusiwadharau CIA kiasi hiki kwani lisemwalo lipo.
"Wizara ina taarifa za uhakika kuwa Makonda amehusika katika uvunjifu huo wa haki kupitia nafasi yake kama mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Katika nafasi yake hiyo, pia amelaumiwa kwa kukandamiza upinzani wa kisiasa, kukandamiza haki ya kujieleza, na kushambulia makundi yasiyo na sauti," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo ya wizara.

Pia Bwana Pompeo alisema ,"Leo tumetangaza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Christian Makonda kuwa hataruhusiwa kuingia Marekani kwa kushiriki kwake katika ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu. Tuna wasiwasi mkubwa juu ya kuporomoka kwa heshima ya haki za binadamu na utawala wa sheria nchini Tanzania," ameeleza aliyekuwa Secretary of state Ndugu Pompeo katika ujumbe wake huo.

Matamko ya jumuiya ya kimataifa kuhusu uhalifu dhidi ya binadamu yalikuwa mengi sana, ni wakati wa kujisafisha sasa na kujenga mahusiano na jumuiya hii, mfano haya hapa chini:






Unaweza weka na mengine mdau tujikumbushe malalamiko kadhaa ya hawa wateule awamu iliyopita

Na majizi yanayoiba kwa kalamu myapigie kelele yadakwe.....
sio kina Manji mnapiga kelele waachiwe
alafu kina mako... Wadakwe mtakuwa kumbafu nyie
 
Paul Christian Makonda mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam aliyepumzishwa ashitakiwe? Ashitakiwe kwa kosa gani? Huyu alikuwa karibu sana na Magufuli na kila alilolifanya lilibarikiwa na Magufuli.

Unapomshitaki Makonda tafsiri yake ni kwamba umemshitaki marehemu Magufuli. Ashitakiwe kwa kosa la kuvamia Clouds na mabunduki? Magufuli alimlinda katika hili.

Ashitakiwe kwa kosa la kula fedha za Tasaf? Magufuli alimlinda katika hili.

Ashitakiwe kwa kosa la kuingiza yale Makontena yake bandarini kinyume na sheria na taratibu? Magufuli alimlinda katika hili.

Ashitakiwe kwa tuhuma za kumshambulia Mh.Tundu Lissu? Magufuli hakutaka na hakuweza hata kuthubutu kutaja jina la Tundu Lissu mpaka anakufa.

Ashitakiwe kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka likiwemo kosa la blackmail?
 
Nashangaaa kwa nini yupo uraiani Mpaka sasa , Magufuli ndio Alimtuma akawaibie na kuwatishia matajiri atawapa case ya uhujumu uchumi?

huo ni ujambazi kama wa sabaya, kaangalie nyumba yake ya Oysterbay ndio ujiulize. Huyu dogo hizi hela alitoa wapi ya kujenga na kununua kiwanja

range na magari ya kifahari anayoendesha yeye na mke wake yote aliwapokonya wafanyabiashara
 
Paul Christian Makonda mkuu wa mkoa wa Dar es salaam aliyepumzishwa ashitakiwe?
Ashitakiwe kwa kosa gani?....
Ukiona ya Sabaya ujue Ni mwendelezo wa wote waliofanya uovu uzuri jinai haifi.
 
Mimi nashauri watu wote washtakiwe Ile baadhi ya watu wafurahi.
 
Kwangu mimi kutokana na Tuhuma zao ( hasa walipokuwa katika Nyadhifa zao ) namfananisha Ole Sabaya ni Papa na Paul Makonda ni Nyangumi.

Unatoaje amri ya kuchunguzwa kwa Papa Ole Sabaya na ukamuacha Nyangumi Paul Makonda? Hapa Rais Samia Mimi Krav Maga sijakuelewa.

Rais Samia tafadhali hakikisha na hiki ulichokifanya kwa Ole Sabaya pia ukifanye kwa Paul Makonda kwani ana Madhambi yaliyomshangaza hata Shetani.
Waliodhurumiwa na huyo mtu wajitokeze wakafungue kesi mahakamani bila shaka utakuwa mwanzo mzuri wa haki
 
Hata Marehemu alimtimua, alimdanganya akagombee Ubunge kisha akamtosa na hakumrudisha tena.

Kwa hiyo tulia tu wewe mfuasi wake kama itahitajika atawajibika tu ana kesi za watu wengi, mwambie kukaa kwa masister huko Arusha sio kwamna watu hawajui, yeye aendelee tu na mipango ya kukimbilia Kenya ila ajue anaonekana.

Mwingine ni DPP huyu naye ni suala la muda. Kama ulitumwa si ulikubali na ukatekeleza? Utawajibika
Bashite alikua akifatwa na mtu mwenye case au aliyedhulumiwa haki yake unamfata kwa sababu ya kuomba msaada upate haki yako lakini anauliza kwanza una million 70 ya kunipa ? Yule Jambazi alikubuu
 
Kanyanyasa, Katesa na Kapora sana tu.

Kaua, katupa sana mahiti kwenye viroba coco beach kapora magari kwa matajiri

atuambie hela za kujenga ile nyumba anayoishi sasa oysterbay na kiwanja alipata wapi ? Range Rover aliyompa mke wake na magari anayoendesha ya kifahari ametoa wapi hela, mansion aliyojenga mwanza Katoa wapi hela bashite ni Nyangumi haki itendeke kwa wote sabaya na bashite

sabaya alikua akienda kutapeli na Kurdish’s wafanyabiashara alikua anasema hiyo ni Makonda style
 
Hakuna Ushahidi Wa Maandishi kwamba Magufuli alimtuma!
Abebe msalaba wake!
waswahili wanasema tumbo linaponzaga makalio...
 
Mimi nadhani ili haki ionekane kutendeka watu wote wanaotajwa tajwa mitandaoni washitakiwe.
 
Yani unajua hapa lazima tuelewe kwamba 95% ya ungoz wa serikari ya mwendazake haukua mzuri hasa hawa RC,DC eidha kwamakusudi waljua wanachofanya, point yangu nikua sabaya anawajibika Kwa makosa yaliyo tokana natuhuma za raia wa hai,sasa ili kuleta tafasiri nzuri ya uwajibikaji ilifaa nawenzake pia washitakiwe.
 
Back
Top Bottom