DustBin
JF-Expert Member
- Jun 3, 2021
- 609
- 604
Ninachokishukuru na kulitukuza jina la Mola wetu aliye juu ni kwamba Raisi wetu wa sasa hafanyi maamuzi kwa mihemko. Na bila shaka wasaidizi wake wanatimiza wajibu wao kisawasawa... Sio kila linalosemwa linafanyiwa kazi. Huyo anayetajwa kwa hili na lile huenda akawa ni ktk wanaofikiriwa kupewa majukumu fulani wayakamilishe kutokana na utendaji wao. Sisi binadamu hatujatimia kwa asilimia zote, ukifanya vizuri sehemu fulani kuna sehemu nyingine unakosea... Ndivyo tulivyo. Mwisho wa siku tutakupima kwa ukubwa wa faida na hasara uloisababisha. Faida ikipiku hasara tutaendelea kuwa nawe na harasa uloisababisha tutaipuuza kwani haina madhara. Na kama ni kinyume chake basi hatua stahiki zitachukuliwa juu yako. Hivyo mnaoimba mapambia kwenye hii single mtake note...!!
Nachotaka kusema ni kwamba Mama yupo makini, Hapangiwi.
Nachotaka kusema ni kwamba Mama yupo makini, Hapangiwi.